MILOVAN ASEMA AKUFFO TATIZO KIWANGO NDIO MAANA BENCHI
Daniel Akuffo mbele ya Mrisho Ngassa |
KOCHA Mkuu wa
Simba SC, Profesa Milovan Cirkovick amesema kwamba mshambuliaji mpya kutoka Ghana,
Daniel Akuffo anatakiwa aongeze juhudi na kupandisha kiwango chake, ili apate
nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini kwa sasa ataendelea kuanzia benchi kwa
kuwa anazidiwa uwezo na wachezaji wanaoanza.
Akizungumza baada
ya mechi dhidi ya JKT Oljoro juzi, Mserbia huyo alisema kwamba Akuffo anaanzia
benchi kwa sasa kwa sababu kuna wachezaji walio vizuri mno zaidi yake na ndio
wanapewa nafasi. “Ajitahidi, atakapokuwa vizuri atapata nafasi ya kuanza, ila
kwa sasa anazidiwa na wanaoanza,”alisema Milovan.
Daniel
Akuffo aliyesajiliwa msimu huu kutoka ASEC Mimosa ya Ivory Coast, aliingia kwa
kishindo Simba akifunga katika mechi
nne mfululizo, lakini baada ya hapo kasi yake imezimika na amefikisha jumla ya
mechi 10, akiwa amefunga mabao matano tu, katika ligi bao moja tu. Katika mabao
hayo matano aliyofunga jumla hadi sasa mshambuliaji huyo mrefu, mawili ni ya penalti.
Simba SC juzi
ilizidi kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia
ushindi wa mabao 4-1 ilioupata kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya
JKT Oljoro ya Arusha, ambayo ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya
kipa wake Shaibu Issa na mshambuliaji Meshack Nyambele kutolewa kwa kadi
nyekundu kipindi cha pili.
Katika mechi
hiyo iliyochezeshwa na refa Amon Paul wa Mara, aliyesaidiwa na Anold Bugabo wa
Singida na Charles Simon wa Dodoma, hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele
kwa mabao 2-1, mabao yake yote yakitiwa kimiani na kiungo Amri Ramadhan Kiemba
katika dakika za 16 na 44, wakati la Oljoro lilifungwa na Paul Nonga dakika ya
29.
Kiemba
alifunga bao la kwanza akiunganisha krosi pasi ya Christopher Edward, wakati
bao la pili lilitokana na krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, yote kutokana na
mashambulizi ya upande wa kulia.
Ilikuwa
rahisi kwa Kiemba kufunga mabao yote akiwa kwenye eneo la hatari, kutokana na
mabeki wa Oljoro kumuwekea ulinzi zaidi Felix Sunzu.
Nonga naye
alifunga bao lake baada ya kupewa pasi ndefu na kumpiga chenga kipa na Nahodha
wa Simba, Juma Kaseja upande wa kulia mwa Uwanja na kuutumbukiza mpira nyavuni
kiulaini.
Bao hilo
lilitokana na beki Paul Ngalema kupokonywa mpira wakati amepanda kusaidia
mashambulizi na Oljoro wakafanya shambulizi la haraka.
Kipindi cha
pili Simba walirudi vizuri zaidi uwanjani na kuuteka zaidi mchezo- jambo ambalo
liliwafanya Oljoro wawapunguze kasi kwa kuwachezea rafu. Hilo liliwagharimu
kupoteza wachezaji wao wawili kabla ya filimbi ya mwisho na kufungwa mabao
mawili zaidi.
Dakika ya 83
Mganda Emanuel Okwi aliifungia Simba bao la tatu na katika dakika ya tatu ya
muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za mchezo, Okwi akiwa anaelekea
kufunga tena, alikwatuliwa na kipa wa Oljoro Shaibu Issa na refa akaamuru
penalti sambamba na kumtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mlinda mlango
huyo.
Awali ya
hapo, Oljoro ilimpoteza mchezaji mwingine, Nyambele dakika ya 78, ambaye
alionyeshwa njano ya pili kwa rafu aliyomchezea Jonas Mkude. Nahodha Kaseja
alitaka kwenda kupiga, lakini akazuiwa na Felix Mumba Sunzu akaenda kufunga bao
la nne kwa mkwaju wa penalti.
Kwa ushindi
huo, Simba imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, hivyo kuendelea
kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 13, ingawa imecheza mechi
tano.
YANGA WAWASHIKA 'UCHAWI' SIMBA SC KIPIGO CHA KAGERA
Yanga SC katika moja ya mechi zao, ambazo wanadai eti Simba wanatia mkono |
YANGA
SC imesema kwamba wamegundua Simba SC ‘wanatia mkono’ kwenye mechi zao
na ndio maana zinakuwa ngumu, ila kuanzia sasa na wao wanaanza ‘fitina’.
Madai
hayo yanakuja, baada ya jana kuchapwa bao 1-0 na Kagera Sugar katika
mchezo wake wa sita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa
Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
“Simba
ilituma watu Bukoba watie mkono mechi yetu, sisi tuliwashitukia hao
watu baadaye sana, lakini tunashangaa kwa nini wanafanya hivi, wakati
sisi tulizungumza nao tukakubaliana haya mambo tuyaache, tucheze mpira,
sasa wao wanatuzunguka wanaendeleza mchezo mchafu,”alisema kiongozi
Mjumbe mmoja wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, ambaye hakutaka kutajwa
jina.
Mjumbe
huyo alisema kwamba wao walijua baada ya makubaliano na Simba
kutofanyiana fitina, waliamini mambo hayo hayatakuwapo, lakini baada ya
kugundua wenzao wamewageuka sasa na wao wanaanza ‘mchezo huo’.
“Na
sisi sasa tunaanza kuzicheza mechi zao, wakumbuke tu wao ndio
walichokoza nyuki, sasa subirini kuanzia mechi yao na Coastal,
wakishinda wao wanaume, na pamoja na kuzicheza mechi zao, tunajizatiti
katika mechi zetu. Uzuri watu wote wanaowatumia tumekwishawajua, ni wale
wale waliokuja Morogoro, na wale wale waliokuja Bukoba.
Tumekwishawajua,”alisema Mjumbe huyo.
Bao
pekee la Themi Felix katika dakika ya 67, jana liliwapa Kagera Sugar
ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Felix
aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnigeria, Enyinna
Darlington kwa kumtungua bao hilo, kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko,
ameendeleza rekodi yake kuvifunga vigogo, Simba na Yanga katika Uwanja
huo.
Hiyo
inakuwa mechi ya pili Yanga kufungwa ndani ya mechi sita walizocheza
hadi sasa na mbili wametoka sare- maana yake inabaki na pointi zake nane
na kuzidi kujipunguzia matumaini ya ubingwa msimu huu, ikiwa sasa
inazidiwa pointi nane na vinara wa ligi hiyo Simba SC.
Aidha,
hii ni mechi ya pili Yanga inacheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi
Ernie Blandts aliyerithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet na katika
mechi hizo mbili ameambulia pointi moja kutokana na sare dhidi ya Simba
Jumatano.
Kwa
ujumla Yanga haijashinda hata mechi moja ya ugenini kati ya tatu
ilizocheza hadi sasa, ilitoka 0-0 na Prisons, ikafungwa 3-0 na Mtibwa na
jana imechapwa 1-0 na Kagera Sugar, wakati Alhamisi itacheza na Toto
African mjini Mwanza.
Katika
mechi hiyo ya jana, Yanga ilipata pigo dakika ya 23 baada ya
mshambuliaji wake mahiri na tegemeo, Said Bahanuzi ‘Spider Man’
kuchanika nyama za paja dakika ya 23, baada ya kugongana na beki
Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi
yake ikichukuliwa na Jerry Tegete.
Tangu
ajiunge na Yanga akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, leo Bahanuzi amecheza
mechi ya 13 kwa dakika hizo 23 na ameifungia timu hiyo jumla ya mabao
12, matatu kati ya hayo kwa penalti.
Katika
mechi zilizochezwa juzi za ligi hiyo, Simba SC ilizidi kujiimarisha
kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 ilioupata kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, ambayo ilimaliza pungufu
ya wachezaji wawili baada ya kipa wake Shaibu Issa na mshambuliaji
Meshack Nyambele kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.
Katika
mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Amon Paul wa Mara, aliyesaidiwa na
Anold Bugabo wa Singida na Charles Simon wa Dodoma, hadi mapumziko Simba
walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-1, mabao yake yote yakitiwa kimiani
na kiungo Amri Ramadhan Kiemba katika dakika za 16 na 44, wakati la
Oljoro lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 29.
Kiemba
alifunga bao la kwanza akiunganisha krosi pasi ya Christopher Edward,
wakati bao la pili lilitokana na krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, yote
kutokana na mashambulizi ya upande wa kulia.
Ilikuwa
rahisi kwa Kiemba kufunga mabao yote akiwa kwenye eneo la hatari,
kutokana na mabeki wa Oljoro kumuwekea ulinzi zaidi Felix Sunzu.
Nonga
naye alifunga bao lake baada ya kupewa pasi ndefu na kumpiga chenga
kipa na Nahodha wa Simba, Juma Kaseja upande wa kulia mwa Uwanja na
kuutumbukiza mpira nyavuni kiulaini.
Bao
hilo lilitokana na beki Paul Ngalema kupokonywa mpira wakati amepanda
kusaidia mashambulizi na Oljoro wakafanya shambulizi la haraka.
Kipindi
cha pili Simba walirudi vizuri zaidi uwanjani na kuuteka zaidi mchezo-
jambo ambalo liliwafanya Oljoro wawapunguze kasi kwa kuwachezea rafu.
Hilo liliwagharimu kupoteza wachezaji wao wawili kabla ya filimbi ya
mwisho na kufungwa mabao mawili zaidi.
Dakika
ya 83 Mganda Emanuel Okwi aliifungia Simba bao la tatu na katika dakika
ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za mchezo, Okwi
akiwa anaelekea kufunga tena, alikwatuliwa na kipa wa Oljoro Shaibu Issa
na refa akaamuru penalti sambamba na kumtoa nje kwa kadi nyekundu ya
moja kwa moja mlinda mlango huyo.
Awali
ya hapo, Oljoro ilimpoteza mchezaji mwingine, Nyambele dakika ya 78,
ambaye alionyeshwa njano ya pili kwa rafu aliyomchezea Jonas Mkude.
Nahodha Kaseja alitaka kwenda kupiga, lakini akazuiwa na Felix Mumba
Sunzu akaenda kufunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti.
Kwa
ushindi huo, Simba imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita,
hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 13,
ingawa imecheza mechi tano.
Katika
mechi nyingine za jana, Mgambo imepata ushindi wake wa kwanza baada ya
kuichapa Polisi Morogoro 1-0, wakati Toto African imeichapa JKT Ruvu 2-1
na Prisons imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar.
ZANZIBAR YAJITOA MICHUANO YA CAF 2012
WAWAKILISHI
wa Zanzibar katika michuano ya Afrika mwakani, Super Falcon waliofuzu kucheza Ligi
ya Mabingwa Afrika na Jamhuri waliofuzu kucheza Kombe la Shirikisho wamejitoa
kwenye michuano hiyo.
Habari
zilizopatikana na kuthibitishwa na Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Aman
Ibrahim Makungu, zimesema kwamba timu hizo zimeamua kujitoa katika michuano
hiyo kwa sababu hazina fedha, ambapo kila timu ilihitaji kiasi cha dola za
Kimarekani 30,000, zaidi ya Sh. Milioni 45 kwa ajili ya maandalizi ya ushiriki
wa michuano hiyo.
Kufuatia
hatua hiyo ZFA, iko katika mazungumzo na baadhi ya klabu za Ligi Kuu ili kuona
kama kuna uwezekano wa kupata timu zitakazochukua nafasi hizo.
Mwaka huu
Zanzibar iliwakilishwa na timu ya Mafunzo katika ligi ya Mabingwa Afrika, huku
Jamhuri wakipata nafasi ya kushirki katika kombe la Shirikisho.
Hata hivyo
timu zote zilishindwa kufanya vizuri baada ya kuondolewa katika hatua ya mwanzo
katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment