Thursday, January 10, 2013

SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA LATOA TAHADHARI KWA WALE WALIOANZA KAMPENI LASEMA MARUFUKU KUFANYA KAMPENI !!!


Shirikisho la soka nchini (TFF) limewaonya watu walioanza kampeni za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo kabla tarehe haijatangazwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, baadhi ya watu wenye nia ya kugombea tayari wameanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo wakati bado kamati inayosimamia uchaguzi haijatoa ruhusa.

Uchaguzi huo ambao rais wa shirikisho hilo, Leodegar Tenga, hawezi kugombea tena kwa mujibu wa katiba, umepangwa kufanyika mwezi ujao katika sehemu ambayo itatangazwa.

 Katibu wa TFF, Angetile Osiah, amesema ruhusa ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo bado haijatolewa na kamati inayosimamia uchaguzi.

Alisema watu wenye nia ya kugombea walioanza kampeni hizo wanakwenda kinyume na taratibu za uchaguzi mkuu.
 Osiah amesema hakuna ruhusa kwa mtu yeyote kuanza kampeni kabla ya tarehe ya uchaguzi kutangazwa na kwamba anayefanya hivyo anakiuka sheria za uchaguzi.

 Amesema kampeni ni hatua za mwisho za uchaguzi na zinaruhusiwa kufanyika baada ya kutangazwa na kuongeza huwezi kuanza kampeni wakati tarehe za uchaguzi na utoaji fomu bado hazijajulikana.

 Amesema kuwa  TFF itawachukulia hatua kali watakaobainika kuanza kampeni hizo huku akisisitiza wasubiri muda sahihi ufike ndiyo waanzae kampeni zao.

 TFF itatoa  taarifa kamili kuhusiana na uchaguzi huo zitajulikana kesho baada ya kamati ya utendaji kumaliza kikao chake na kutoa tamko rasmi la lini na wapi uchaguzi mkuu utafanyika.

Viongozi wa kuchaguliwa wa TFF waliopo madarakani tayari wamemaliza muda wao, huku rais Tenga hatagombea tena mwaka huu, kwa mujibu kamati ya uchaguzi mkuu.

No comments:

Post a Comment