Thursday, January 10, 2013

LICHA YA JANA KUSHINDA BAO 4-0 HALI YA HEWA REAL NI MBAYAMASHABIKI WADAI MOURINHO AMEVURUGA MVUTO WA REAL

>>KUMBWAGA CASILLAS KWAMLETEA CHUKI!!
>>KLABUNI HALI SI SHWARI!!
>>MPASUKO WA WACHEZAJI, WA SPAIN NA URENO!!
IKER_CASILLASKUFUATIA Kura ya Maoni huko Madrid na kuchapishwa na Gazeti maarufu, Marca, Mashabiki Asilimia 62 wa Real Madrid wametoa msimamo wao kuwa Kocha wa Klabu hiyo, Jose Mourinho, ameuharibu mvuto wa Klabu hiyo maarufu.
Kura hiyo ya Maoni iliyohusisha Wanachama 704 na Asilimia 54.4 wametaka aendelee kubaki lakini Asilimia 41.8 wametaka aondoke huku mafanikio yake kiutendaji yakishuka kutoka 8.82 kati ya 10 aliyopata Machi 2011 hadi 6.68 kati ya 10.JOSE_MOURINHO-poa
Kura hiyo ya Maoni iliendeshwa na Sigma Dos na ni ushahidi tosha hali si shwari ndani ya Real Madrid ambao ndio Mabingwa watetezi wa La Liga lakini hadi sasa wako Pointi 16 nyuma ya Vinara Barcelona na pia wapo hatarini kutupwa nje ya Copa del Rey ambako walifungwa 2-1 na Celta Vigo katika Mechi ya kwanza na leo ni marudio yake Uwanjani Santiago Bernabeu.
Hali hii ya sasa ndani ya Real Madrid pia itamletea matatizo makubwa Rais wao Florentino Perez ambae Mwaka huu anakabiliwa na Uchaguzi katika nafasi yake.
Mashabiki wengi wa Real wanachukizwa na tabia ya Jose Mourinho ya ‘kiugomvi ugomvi’ na Siku zote kudai Timu yake inaonewa wakati Mashabiki hao wana msimamo kuwa Klabu yao ni ya Kiungwana ambayo Siku zote inakubali kushinda na kushindwa kiungwana.
Hivi karibuni, Mourinho alishutumiwa sana kwa kumpiga Benchi Kipa na Nahodha wao Iker Casillas huku kukiwa na tuhuma kuwa hali si njema miongoni mwa Wachezaji ikidaiwa kuna mgawanyiko upande mmoja ukiwa wa Wachezaji wa Spain na mwingine Wachezaji kutoka Ureno.

No comments:

Post a Comment