
Chama cha Soka England, FA,
kimethibitisha kuwa Sir Alex Ferguson, hatapewa adhabu yeyote kwa
kitendo chake cha kabla Kipindi cha Pili kuanza, cha kumvaa Refa Mike
Dean na kumlalamikia kisha kumkabili Refa wa Akiba Neil Swarbrick na pia
Refa Msaidizi Jake Collin, kwa vile Refa Dean hakuzungumza lolote
kuhusu tukio hilo katika Ripoti ya Mechi.
Hata hivyo, Mameneja wa Man City na QPR,
Roberto Mancini na Harry Redknapp, wako matatani kufuatia kauli zao
baada ya Mechi zao za kulalamika kuhusu Marefa na kudokeza uchezeshaji
usio wa haki kitendo ambacho ni kinyume cha Kanuni za FA.
Mancini, Meneja wa Man City, alilalamika
kuhusu Refa Kevin Friend baada kufungwa 1-0 na Sunderland kwenye Mechi
ya Ligi Kuu England iliyochezwa Desemba 26 kwa Refa huyo kutopiga
Filimbi ya Faulo aliyochezewa Mchezaj wake Pablo Zabaleta na badala yake
kuachia mpira uchezwe na kuzaa Goli la Adam Johnson, Winga wa zamani wa
Man City, lililowaua City 1-0.
Mancini alidai: “Pengine Refa alivimbiwa na Mlo wa Krismasi! Haiwezekani Waamuzi wawili wasione tukio hilo! [Akimaanisha Refa Na Msaidizi wake]”
Nae Harry Redknapp, Bosi wa QPR, yuko
matatani baada ya kuhamaki na maamuzi ya Refa Chris Foy ambayo alidai ni
‘Skandali!’ wakati walipofungwa 2-1 na West Brom na kutupwa mkiani mwa
Ligi Kuu England Siku ya Boxing Dei.
Refa Chris Foy alilikubali Goli la
kujifunga mwenyewe Kipa Robert Green ambae alionekana akibanwa waziwazi
na Mchezaji wa WBA, Marc-Antoine Fortune, na pia aliwayima Penati ya
wazi mwishoni baada ya Beki Liam Ridgewell kuunawa mpira.
Redknapp amewaka: "Ile ni Faulo ya wazi kwa Kipa wetu na ile ni Penati ya wazi! Hii ni kashfa!”
Msimamo wa FA kwa Mameneja ni kwamba
hawatakiwi kuwalaumu Marefa kuhusu maamuzi yao na wakifanya hivyo
wanaandikiwa Barua kutaka maelezo yao na kama hayaridhishi hufunguliwa
Mashitaka.
Wakati huo huo, FA imetangaza kuwa Rufaa
za Everton na West Ham kupinga Kadi Nyekundu kwa Wachezaji wao, Darron
Gibson wa Everton na Carlton Cole, zimekubaliwa na Adhabu za kufungiwa
Mechi 3 kila mmoja kwa Wachezaji hao zimefutwa.
Wachezaji hao wote wawili walitolewa
katika Mechi moja na Refa Mark Anthony Uwanjani Upton Park Wikiendi
iliyopita ambako Everton walishinda 2-1 baada ya kutoka nyuma kwa kwa
Bao la Carlton Cole na kutolewa kwa Mfungaji huyo kuliwapa mteremko
kusawazisha na kushinda huku Mchezaji wao Gibson akitolewa Dakika za
majeruhi.
Wachezaji hao wote wawili sasa wako huru kuziwakilisha Klabu zao Mechi za Ligi Wikiendi hii
No comments:
Post a Comment