Newcastle na
Millwall huenda wakakumbana na adhabu ya shirikisho la soka duniani FIFA kufuatia
vilabu hivyo kugomea kuwaachia wachezaji wa kimataifa wa Nigeria Shola Ameobi na Danny Shittu kwa ajili ya
kulitumikia taifa lao katika michuano ya fainali za mataifa ya Afrika nchini
Afrika Kusini mwezi Januari
Bosi wa Newcastle
Alan Pardew anasema mshambuliaji wake Shola Ameobi hatasafiri kuelekea Afrika
katika fainali hizo.
Ameobi na Shittu
wote wanatarajiwa kujitoa rasmi katika uteuzi wao katika timu ya taifa ya
Nigeria (Super Eagles), jambo ambalo limeonekana kulikasirisha shirikisho la
soka la nchi hiyo (NFF).
Meneja wa Newcastle
Alan Pardew amesema Ameobi hatatokezea katika michuano hiyo ambayo inatarajiwa
kuanza January 19, wakati ambapo mlinzi wa Millwall er Shittu naye anatarajiwa
kutolea nje uteuzi wake kama ilivyo kwa Ameobi.
Sheria za FIFA
zinasema mchezaji yoyote ambaye atashindwa kuripoti katika timu yake ya taifa
baada ya kutajwa na nchi yake kwa ajili ya majukumu ya kimataifa , basi
mchezaji huyo atakuwa si halali kutumika katika kipindi chote kilichopendekezwa
wakati wa jukumu hilo pamoja na kuongezewa siku tano zaidi kama itawezekana vinginevyo
kuwepo na makubaliano mengine kati ya klabu yake na nchi husika.
Mjumbe wa
bodi ya shirikisho la soka la Nigeria Chris Green amesema watahakikisha klabu
za wachezaji hao zinaadhibiwa kama watagomea kuwaachia wachezaji hao.
No comments:
Post a Comment