Thursday, December 27, 2012

TIMU YA BLACKBURN ROVERS YAMTIMUA KOCHA WAKE HENNING BERG NA MAAFISA WATATU WA TIMU HIYO

 Blackburn Rovers imemfukuza kazi meneja wake Henning Berg na maafisa wengine watatu katika safu ya makocha ikiwa ni hatua ambayo imefuatia klabu hiyo kutereza katika vibaya katika msimamo wa ligi ndogo ya nchini England, Championship.

Meneja huyo raia wa Norway, ambaye aliajiriwa mwezi  October, katika jumla ya michezo 10 amefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu katika kipindi chake cha utumishi wake wa siku 57.

Berg, ambaye alikuwa mchezaji wa Rovers mwaka 1995 wakati huo Rovers ilishinda taji la ligi kuu ya England “Premier League”  na baadaye akishinda taji la “League Cup” akiwa nahodha wa kikosi mwaka 2002, alirejeshwa katika klabu hiyo kama meneja mwezi Oktoba.

Baada ya Blackburn kuanza kwa kusuasua chini ya meneja wake wa zamani Lyn Oslo na Lillestrom klabu hiyo ikaamua kumpa Berg jukumu la kukinoa kikosi hicho katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Middlesbrough jana Boxing Day kilipelekea Rovers kujikuta katika nafasi ya 17 ikifanikiwa kukusanya alama 7 ndani ya uwezo wake wa kukusanya alama 30 kama wangeshinda michezo yote chini ya meneja Henning Berg.

Meneja msaidizi, Eric Black, kocha wa namba moja Iain Brunskill kocha wa makipa Bobby Mimms nap wamekumbwa na dhahma hiyo ya kufukuzwa kazi pamoja na Berg kutoka katika viunga vya Ewood Park.

No comments:

Post a Comment