Thursday, December 27, 2012

YANGA KUPAAA KESHO KUTWA JUMAPILI KWENDA UTURUKI



 YANGA inaondoka Jumapili alfajiri kwenda mjini Antalya, Uturuki kwa kambi ya wiki mbili itakayomalizika Januari 13 bila wachezaji Salum Telela, Shamte Ally, Ibrahim Job, Yaw Berko na Rashid Gumbo waliopelekwa kwa mkopo timu mbalimbali.

Uongozi umethibitisha kwamba kambi itakuwa Antalya ambao ni mji ulioko kilomita 490 kutoka Instanbul yalipo makao makuu ya nchi hiyo yenye baridi kali muda mwingi.

Umbali kutoka Dar es Salaam mpaka Instanbull kwa ndege ni kilomita 5,394.5 ambao ni mwendo wa saa saba kwa ndege.
Lakini kocha wake Ernest Brandts alisema: "Lengo letu ni kutwaa ubingwa kwenye ligi kuu, tupo kileleni hivi sasa tutang'ang'ania hapo hapo."

"Kila kitu katika soka ni nidhamu, iwe ndani ya uwanja au hata nje, mazoezi na hata kwenye mechi. Kama mchezaji hana nidhamu hawezi kuwa bora, ninachoshukuru wachezaji wangu wanafuata kile ambacho mimi ninataka.

"Mimi ni mkali wakati mwingine ninapoona mchezaji anakwenda tofauti nampa adhabu."

Yanga inaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kesho Jumatano itacheza na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment