Thursday, December 27, 2012

MENEJA WA LIVERPOOL BRENDAN RODGERS AKUBALIANA NA MATOKEO YA JANA DHIDI YA STOKE CITY


 Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesisitiza kuwa hawakuwa na la kujivunia katika mchezo ambao walipoteza kwa kuchapwa mabao 3-1 na Stoke City iliyocheza vema hapo jana kule katika dimba la Britannia jioni ya jana.

Wekundu hao walipata bao la mapema kupitia kwa nahodha Steven Gerrard kwa njia ya penati baada ya Luis Suarez kuangushwa katika eneo la hatari na Ryan Shawcross. 

Hata hivyo Stoke wakafanikiwa kusawazisha na baadaye kuandika bao la pili la uongozi kupitia kwa Jonathan Walters na kisha bao la kichwa la Kenwyne Jones.

Brendan Rodgers amekiri kikosi chake kuvurunda katika mchezo huo lakini pia akionekana kuhuzunishwa na aina ya magoli yaliyokuwa yakifungwa na kusema timu yake inapaswa kujifunza namna ya kulinda kama inataka kupata alama katika michezo ya ugenini.

“ulikuwa ni mwanzo mzuri kwetu kwa kupata goli la mapema kupitia njia ya penati, lakini tulishindwa kujilinda nadhani magoli yote matatu na makosa ya ulinzi, kiukweli hatukustahili chochote katika mchezo huu”

No comments:

Post a Comment