FOMENKO KOCHA MPYA UKRAINE.
SHIRIKISHO la Soka nchini Ukraine-FFU limemtaja kocha Mikhail Fomenko kama kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo. Nafasi
hiyo ambayo iliachwa wazi toka Septemba mwaka huu baada ya aliyekuwa
kocha wa timu hiyo Oleg Blokhin kuondoka na kwenda kuifundisha klabu ya
Dynamo Kiev baada ya michuano ya Ulaya kumalizika. Kocha
wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester Ciy,
Sven-Goran Eriksson ndio alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa kocha wan
chi hiyo lakini mwishoni Fomenko ndio amethibitishwa kuchukua nafasi
hiyo. Fomenko
aliwashukuru maofisa FFU kwa kumwamini kumpa kibarua hicho na kwamba
anatambua jukumu lake na changamoto zinazoikabili timu ya taifa ya nchi
hiyo ambapo kazi yake ya kwanza itakuwa ni kuhakikisha wanafuzu michuano
ya Kombe la Dunia 2014. Kocha
wa zamani wa Tottenham Hotspurs aliwahi kukiri kuitaka nafasi hiyo
kabla ya kukubali kuinoa Queens Park Rangers wakati mshambuliaji nyota
wa zamani wa nchi hiyo Andriy Shevchenko alikataa nafasi ya kuifundisha
nchi yake.
No comments:
Post a Comment