Wednesday, January 23, 2013

MAPOU YANGA MBIWA YUPO NEWCASTLE,CARLOS PUYOL NI BARCA MWISHO,SNEIJDER ATUA GALATASARAY WALIPOKUWA YANGA,NA BENITEZ ASEMA MARCO MATERAZZI NI MUONGO

NEWCASTLE UNITED imemnasa Beki wa France Mapou Yanga-Mbiwa kutoka Montpellier, nae Wesley Sneijder amekamilisha Uhamisho kutoka Inter Milan kwenda kwa Vigogo wa Uturuki Galatasaray huku Nahodha wa Barcelona Carles Puyol akiendeleza Ndoa yake kwa Barca hadi 2016 lakini Meneja wa Chelsea, Rafael Benitez, amefunguka na kudai Beki wa Italy Marco Materazzi ni mwongo wa kutupwa.

Mapou Yanga-Mbiwa yupo Newcastle United toka Montpellier

Newcastle United imemsaini Beki Mapou Yanga-Mbiwa kutoka Klabu ya France Montpellier kwa Ada ambayo haikutajwa lakini inasadikiwa kuwa £6.7m.
Beki huyo wa France mwenye Miaka 23 amesaini Mkataba wa Miaka 5 na nusu.
Na wakati huo huo, Yoan Gouffran, Fowadi wa Klabu nyingine ya France, Bordeaux, ametoboa kuwa yuko njiani kujiunga na Newcastle.

Carles Puyol

Nahodha wa Barcelona Carles Puyol amesaini nyongeza ya Mkataba ambayo itamweka Barcelona hadi Mwaka 2016.
Puyol, ambae ni Sentahafu, anaungana na Mastaa wengine wa Barca, Xavi na Lionel Messi, kwa kusaini Mikataba mipya.
Puyola, Miaka 34, alikuwa na Mkataba ambao ulikuwa umalizike Mwaka 2014.

Sneijder atua Galatasaray

Internazionale's Wesley Sneijder
Wesley Sneijder amesaini kuichezea Klabu ya Uturuki Galatasaray kwa Mkataba wa Miaka Mitatu na Nusu na kwa Dau la Pauni Milioni 8.4.
Sneijder alihamia Inter Milan Mwaka 2009 na kufanikiwa kutwaa Trebo Mwaka 2010, yaani Ubingwa wa Ulaya, Coppa Italia na Ubingwa wa Serie A.
Kutokana na mvutano na Inter Milan hasa kutaka kulazimishwa apunguzwe Mshahara, Sneijder hajaichezea Inter Milan tangu Septemba Mwaka jana.

Benitez v Materazzi
  rafa benitez
Meneja wa Liverpool Rafael Benitez amemwita Beki wa Italy Marco Materazzi kuwa ni mwongo baada ya Mchezaji huyo kudai himaya ya Benitez wakati akiwa Inter Milan ni kama kurudi Shule.
Benitez, aliekaa Inter Milan Miezi 6 tu baada ya kumrithi Jose Mourinho na kushinda Mechi 12 tu kati ya 25, amedaiwa na Materazzi kuwa alirubuniwa kuchukuliwa na Inter wakati hata Mourinho hajaondolewa na pia alimuamrisha kuondoa Picha zote za Mourinho kwenye Kabati lake binafsi Klabuni hapo.
Benitez amewaambia Wanahabari: “Anaongopa. Marco Materazzi anadanganya. Ni uongo, anadanganya tu. Akiongelea kuhusu Mourinho ni uongo, hakuna Mtu aliejua ntaenda Inter hata mie mwenyewe. Ni uongo”

No comments:

Post a Comment