Wednesday, January 23, 2013

TIMU NDOGO YA DARAJA LA KWANZA ILIYOIFUNGA ARSENAL,WIGAN YATIGA FAINAL CAPITAL ONE CUP BAADA YA KUIONDOSHA ASTON VILLA KATIKA DIMBA LA VILLA PARK JANA SASA KUWASUBIRI SWANSEA CITY AU CHELSEA

>>KUIVAA WEMBLEY SWANSEA AU CHELSEA!!
CAPITAL_ONE_CUP-BEST>>WAMEZIFUNGA TIMU 3 ZA LIGI KUU KUTINGA FAINALI!!
Bradford City imekuwa Timu ya kwanza ya Daraja la 4, Ligi 2, kwa zaidi ya Miaka 50 kutinga Fainali ya Kombe la Ligi, sasa linaitwa CAPITAL ONE CUP, baada ya kuibwaga Timu ya Ligi Kuu England Aston Villa kwa Jumla ya Bao 4-3 katika Mechi mbili za Nusu Fainali.

MAGOLI:
Aston Villa 2
-Benteke Dakika ya 24
-Weimann 89
Bradford 1
-Hanson Dakika ya 55

Bradford City walishinda Mechi ya Kwanza 3-1 na jana kufungwa 2-1 na Aston Villa Uwanjani Villa Park na sasa wapo Wembley kucheza Fainali na Mshindi kati ya Swansea City na Chelsea wanaorudiana leo Usiku huku Swansea wakiwa na ushindi wa 2-0 katika Mechi ya Kwanza.

BRADORD WAMEZIFUNGA TIMU 3 ZA LIGI KUU KUTINGA FAINALI:
-Wigan
-Arsenal
-Aston Villa
**FAINALI NI WEMBLEY FEBRUARI 24: Bradford City v Swansea au Chelsea

Licha ya Aston Villa kutawala Kipindi cha Kwanza na kufunga Bao kupitia Christian Benteke Bradford walisawazisha kwa Bao la kichwa la James Hanson.
Andreas Weimann aliifungia Aston Villa Bao la pili Dakika ya 89 lakini walishindwa kupata Bao nyingi ambalo lingelazimisha Muda wa Nyongeza wa Dakika 30.
VIKOSI:
Aston Villa: Given, Lowton, Vlaar, Clark, Bennett, Ireland, Delph, Bannan, N'Zogbia, Benteke, Agbonlahor
Akiba: Guzan, Bent, Holman, Weimann, Stevens, Lichaj, Carruthers.
Bradford: Duke, Darby, McHugh, McArdle, Good, Hines, Gary Jones, Doyle, Atkinson, Hanson, Wells
Akiba: McLaughlin, Ravenhill, Reid, Thompson, Connell, Nelson, Turgott.
Refa: Phil Dowd 
RATIBA/MATOKEO:
NUSU FAINALI
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Jumla ya Magoli kwa Mechi mbili]
Jumanne Januari 22
Aston Villa 2 Bradford 1 [3-4]
Jumatano Januari 23
[Mechi kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Swansea City v Chelsea [2-0]
FAINALI
Jumapili Februari 24
Uwanja wa Wembley, London
Bradford City v Swansea/Chelsea

DONDOO MUHIMU za CAPITAL ONE CUP:
-KABLA LILIKUWA ni Carling Cup na Bingwa Mtetezi alikuwa ni Liverpool.
-Linaitwa CAPITAL ONE CUP kwa sababu Mdhamini wake ni Kampuni ya masuala ya Fedha, Capital One.
-Linashirikisha Timu za Ligi za juu England 92 kwa mtindo wa Mtoano [Timu 20 toka Ligi Kuu na 24 kila moja kutoka Madaraja ya Npower, Ligi 1 na 2.
-FAINALI itafanyika Uwanja wa Wembley Tarehe 24 Februari 2013
-Bingwa wa michuano hii hucheza EUROPA LIGI Msimu unaofuata kuanzia Raundi ya Tatu ya Mtoano.

No comments:

Post a Comment