Wednesday, January 23, 2013

KIPORO CHA BPL NI LEO KATI YA ARSENAL NA WAGONGA NYUNDO WEST HAM,PIA ANGALIA NA WANAOONGOZA KWA MABAO ENGLAND+++++++++++++++++++


>>WIKIENDI HII BPL HAMNA, KUPISHA FA CUP!!
JUMATANO, Januari 23, SAA 4 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu, Arsenal watatinga Uwanja wao wa Emirates Jijini London kucheza na West Ham katika Mechi pekee ya BPL, Barclays Premier League, ikiwa ni kiporo baada ya Mechi hii kuahirishwa kuchezwa Desemba 26 kufuatia mgomo wa Wafanyakazi wa Reli, London Underground.

BPL:
MSIMAMO-Timu zaJuu:
1 Man United Mechi 23 Pointi 56
2 Man City  Mechi 23 Pointi 51
3 Chelsea  Mechi 23 Pointi 45
4 Tottenham  Mechi 23 Pointi 41
5 Everton  Mechi 23 Pointi 38
6 Arsenal  Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 15] Pointi 34
7 Liverpool  Mechi 23 [Tofauti ya Magoli 12] Pointi 34
8 West Brom Mechi 23 [Tofauti ya Magoli 1] Pointi 34
9 Swansea  Mechi 23 Pointi 33
10 Stoke Mechi 23 Pointi 29
11 Sunderland Mechi 23 Pointi 28
12 West Ham Mechi 22 Pointi 27

WANAOONGOZA KWA UFUNGAJI MABAO


1. Robin VAN PERSIEManchester United18

2. Luis SUAREZLiverpool16

3. Demba BAChelsea14

4. MichuSwansea City13

5. Edin DZEKOManchester City10

6. Steven FLETCHERSunderland10

7. Jermain DEFOETottenham Hotspur10

8. Rickie LambertSouthampton10

9. Theo WALCOTTArsenal9

10. Gareth BALETottenham Hotspur9

11. Romelu LUKAKUWest Bromwich Albion9

12. Javier HERNANDEZManchester United8

13. Frank LAMPARDChelsea8

14. Marouane FELLAINIEverton8

15. Sergio AGUEROManchester City8

BPL_LOGOSambamba na Mechi hiyo ya BPL, pia Jumatano kutakuwa na Mechi ya Marudiano ya CAPITAL ONE CUP kati ya Swansea City na Chelsea itakayochezwa Uwanja wa Liberty na katika Mechi hiyo Swansea wanaingia wakiwa kifua mbele wakiwa wameshinda 2-0 katika Mechi ya kwanza walipocheza Stamford Bridge.
Wikiendi hii inayokuja BPL itakuwa haina Mechi kwa kupisha Mechi za Raundi ya 4 ya FA CUP na Mechi za Ligi hiyo zitachezwa katikati ya Wiki hapo Jumanne Januari 29 na Jumatano Januari 30.
TATHMINI: Arsenal v West Ham
Huku akiwa amekiri Timu yake haina mwelekeo mzuri wa ushindi mfululizo, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, amekuwa akihofia kuikosa nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao wakati sasa wapo nafasi ya 6 wakiwa Pointi 7 nyuma ya Timu ya 4 Tottenham ambayo ndio nafasi ya mwisho kucheza Ulaya.
Msimu huu, Arsenal, ambao wana Pointi 34 kwa Mechi 22 zikiwa ni Pointi chache kabisa kuwa nazo hatua kama hii katika himaya ya Wenger, wameifunga Timu moja tu iliyo juu yao na ni muhimu kuzifunga Timu zilizo chini yao kama vile West Ham ambao wako nafasi ya 12 na wana Pointi 27.
Mara ya mwisho kwa Arsenal kucheza na West Ham ilikuwa ni Oktoba ambapo West Ham walitangulia kufunga Bao lakini Arsenal waliibuka washindi kwa Bao 3-1 na kuendeleza wimbi la kutofungwa na West Ham katika Mechi 10 walizocheza mwisho.
HALI za WACHEZAJI
Baada ya kuugua, Arsenal inawakaribisha tena Lukas Podolski na Alex Oxlade-Chamberlain baada ya kukosa Mechi ya Jumapili iliyopita waliyofungwa na Chelsea.
Lakini Arsenal wana upungufu kwenye Kiungo kufuatia kuumia kwa Mikel Arteta, Abou Diaby na Francis Coquelin.
West Ham itawakosa Marouane Chamakh, ambae juzi amehamia hapo kwa Mkopo akitokea Arsenal na hivyo haruhusiwi kucheza, na pia Sentahafu James Collins ambae ni majeruhi.
USO kwa USO
-Arsenal hawajafungwa katika Mechi 10 za mwisho walizocheza na West Ham na wameshinda Mechi 8 kati ya hizo.
-Katika Mechi zao 5 za mwisho za Ligi walizokutana, Penati 5 zilipigwa katika Mechi hizo.
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumatano Januari 23
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal v West Ham
Jumanne Januari 29
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Aston Villa v Newcastle
QPR v Man City
Stoke v Wigan
Sunderland v Swansea
Jumatano Januari 30
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Liverpool
Everton v West Brom
Norwich v Tottenham
[SAA 5 Usiku]
Fulham v West Ham
Man United v Southampton
Reading v Chelsea
Jumamosi Februari 2
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
QPR v Norwich
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Stoke
Everton v Aston Villa
Newcastle v Chelsea
Reading v Sunderland
West Ham v Swansea
Wigan v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Fulham v Man United
Jumapili Februari 3
[SAA 10 na Nusu Jioni]
West Brom v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
Man City v Liverpool

No comments:

Post a Comment