Wednesday, January 23, 2013

COPA del REY: BARCA HATARINI UGENINI NA MALAGA! NA ITALIAN CUP JUVE NA LAZIO NGOMA NZITO DROO 1-1


>>BARCA KUIKOSA EL CLASICO NUSU FAINALI??
>>COPPA ITALIA: NI NUSU FAINALI!!
MABINGWA watetezi wa COPA del REY Barcelona Ijumaa wanatinga La Rosaleda kurudiana na Malaga kwenye Robo Fainali ya Kombe hili la Mfalme huku wakiwa wametoka sare 2-2 na Malaga katika Mechi ya kwanza na huku wakiwa wametoka katika kipigo chao cha kwanza kwenye La Liga walipofungwa 3-2 na Real Sociedad Jumamosi iliyopita wakijua fika wakiteleza wanaweza kuikosa EL CLASICO kwa kukutana na Real Madrid kwenye Nusu Fainali.

COPA del REY
ROBO FAINALI-MARUDIANO
[Matokeo Mechi za Kwanza katika Mabano]
Jumatano Januari 23
[SAA 3 NA Nusu Usiku]
Sevilla FC v Real Zaragoza [0-0]
[SAA 5 na Nusu Usiku]
Valencia v Real Madrid CF [0-2]
Alhamisi Januari 24
[SAA 4 Usiku]
Real Betis v Atletico Madrid [0-2]
Ijumaa Januari 25
[SAA 6 Usiku]
Malaga v Barcelona [2-2]

LIONEL_MESSI-HUZUNIMahasimu wa Barcelina, Real Madrid, wao wanatinga ugenini Mestalla kurudiana na Valencia Timu ambayo waliipiga 2-0 katika Mechi ya kwanza ya  COPA del REY Uwanjani Santiago Bernabeu na Jumapili iliyopita waliitwanga 5-0 kwenye La Liga Uwanjani Mestalla.
Atletico Madrod nao wanarudiana na Real Betis huku nao wakiwa mbele kwa Bao 2-0 walizopta katika Mechi ya kwanza lakini wataingia kwenye Mechi hii bila ya Straika wao Nyota Radamel Falcao ambae ni majeruhi.
Robo Fainali nyingine ni kati ya Sevilla na Real Zaragoza na zinarudiana Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan, nyumbani kwa Sevilla, wakiwa walitoka sare 0-0 katika Mechi ya kwanza.
Huko Italy, Kombe la Nchi hiyo, COPPA ITALIA, linaingia hatua ya Nusu Fainali.

COPPA ITALIA
NUSU FAINALI:
Jumanne Januari 22
Juventus 1 v SS Lazio 1
Jumatano Januari 23
AS Roma v Inter Milan
Jumanne Januari 29
SS Lazio v Juventus
Jumatano Aprili 17
Inter Milan v AS Roma

No comments:

Post a Comment