![]() |
Haruna Moshi 'Boban' akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa JKT jana |
WATAZAMAJI
12,984 walikata tiketi kushuhudia mechi ya namba 99 ya Ligi Kuu ya
Vodacom iliyochezwa jana (Februari 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 ambapo jumla ya sh. 73,532,000 zilipatikana. Kila klabu ilipata
mgawo wa sh. 17,443,752.45 ambapo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 11,216,745.76.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 8,869,704.64,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 5,321,822.78, Kamati ya Ligi
sh. 5,321,822.78, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,660,911.39 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,069,597.75.
Wakati
huo huo: Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu
Tanzania (FRAT) uliokwama kufanyika mara mbili, sasa utafanyika Februari
14 mwaka huu mjini Morogoro.
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa FRAT wanatakiwa kufika Morogoro siku moja kabla ya
tarehe ya uchaguzi. Pia wapiga kura na wagombea wanatakiwa kulipia ada
za uanachama kwa mwaka 2013 kabla ya uchaguzi.
Wagombea
ni Army Sentimea na Said Nassoro (uenyekiti) wakati wanaoomba nafasi ya
Makamu Mwenyekiti ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika Kambimtoni.
Abdallah
Mitole, Charles Ndagala na Hamis Kisiwa wanawania ukatibu mkuu, nafasi
ya Mhazini inagombewa na Jovin Ndimbo. Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Kamwaga Tambwe wakati
nafasi ya uwakilishi wanawake yupo Isabela Kapera.
Wagombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Emmanuel Chaula na Samson Mkotya.
No comments:
Post a Comment