Kutoka kushoto, Juma Seif Kijiko, Obadia Mungusa, Shamte Ally na Ibrahim Job. |
Wachezaji
kiungo wa pembeni Shamte Ally, kiungo stadi wa kati Juma Seif Kijiko wa
Yanga, mlinzi wa kati Obadia Mungusa wa Simba na mlinzi wa pembeni wa
zamani wa Yanga Ibrahim Job, wanatarajiwa kuvaa jezi ya timu ya African
Lyon ya Temeke jijini Dar es Salaam katika mzunguko wa pili wa ligi kuu
ya soka Tanzania Bara.
Wachezaji
hao tayari wamekamilisha taratibu zote za kuhamia klabu hiyo katika
kipindi cha dirisha dogo kwa mkopo, na tayari wameanza mazoezi na klabu
hiyo katika uwanja wa Sigara ulioko Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Akiongea
na Rockersports katibu wa Afrikan Lyon Brown Elias amesema uongozi wa
Lyon umefurahishwa na ujio wa wachezaji hao ambao licha ya kwamba
walikuwa hawapewi nafasi katika vikosi vya kwanza katika vilabu vyao
lakini anaamini ni wazuri.
Amesema
ni ngumu kupata nafasi katika vilabu vikubwa vya Simba na Yanga hata
kama mchezaji ni mzuri kutokana na ushindani mkubwa wa kugombea namba
miongoni mwa wachezaji na hiyo haiondoi uzuri wa mchezaji na kwamba kama
mchezaji anajua kucheza basi atakuwa anajua tu jambo la msingi ni
mazoezi na kujituma uwanjan.
Hata
hivyo Brown amesema uongozi wa Lyon chini ya mkurugenzi wake Rahimu
Zamunda Kangezi "mmachinga" umesikitishwa na kumkosa mshambuliaji mrefu
kuliko wote katika ligi kuu ya soka Tanzania Bara Gaudience Mwaikimba
kufuatia ombi lao kutolewa nje na uongozi wa klabu hiyo.
Lyon
tayari imenza maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka
Tanzania Bara wakifanya mazoezi yao katika uwanja wa Sigara ulioko
Changombe jijini Dar es Salaam.
Kwasasa
klabu hiyo haina kocha mkuu mara baada ya aliyekuwa kocha mkuu Pablo
Ignacio Velez kutimka rasmi na sasa Afrikan Lyon inasaka kocha mrithi
wake kabla ya kuanza kwa ligi kuu mzunguko wa pili.
Pichani Pablo Ignacio Velez kulia, alipokuwa akitambulishwa kwa waandishi wa habari mwezi Agosti. kushoto ni Rahim Kangezi na Charles Otieno katikati. |
No comments:
Post a Comment