Saturday, December 29, 2012

DIEGO ALMANDO MARADONA ANAAMINI KUWA MOURINHO NI MIONGONI MWA MAKOCHA BORA DUNIANI

Diego Maradona anaamini kuwa kocha wa Real Madrid ni miongoni mwa makocha bora duniani.Mreno huyo aliiongoza Blancos mpaka kutwaa taji la ligi kuu nchini Hispania La Liga msimu uliopita na pia akiwa na rekodi ya kutwaa mataji katika nchi zenye ligi ngumu kama vile Ureno, England na Italia pamoja na kutwaa mataji mawili ya vilabu bingwa Ulaya.

Maradona, ambaye katika fani ya ufundishaji hakung’ara sana kama ilivyokuwa katika kipindi cha uchezaji wake, anaamini kuwa bosi huyo wa zamani wa Inter katika kipindi chote amefanikiwa kuwa juu.

Akinukuliwa nchini Dubai hapo jana Maradona amesema,

"matokeo aliyoyapata Mourinho yanaongeza nguvu ya sauti ya uwezo wake”

Ameendelea kwa kusema nimekuwa nikimuona akifundisha katika kiwango cha juu, amekuwa makini na kila mchezaji katika kikosi chake kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

"nilikuwa ni mchezaji niliyekuwa nataka kujulikana, lakini ni jambo jema kuona kocha hakujali peke yako lakini timu nzima kwasababu wao ndio wanao kusaidia uwanjani"

Maradona kwasasa hana timu ya kufundisha baada ya kuondoshwa katika klabu ya Al Wasl mapema mwaka huu wa 2012.

Nafasi kubwa aliyopata katika ufundishaji wake ni timu yake ya taifa ya Argentina mwaka 2010 katika fainali ya kombe la dunia, ambapo timu hiyo ya taifa kutoka Amerika ya kusini ilitolewa na Ujerumani katika robo fainali.

No comments:

Post a Comment