Sunday, January 6, 2013

FA CUP LIVER POOL YAPETA 2-1 KWA BAO LA UTATA KWA MZEE WA KUSHIKA MPIRA LUIS SUAREZ LAKINI ARSENAL HALI TETE YATOA DROO SASA KURUDIANA KAMA ILIVYO KWA MASHETANI WEKUNDU

FA_CUP-NEW_LOGO++++++++++++++++++++++
FA CUP
MATOKEO:
Jumapili Januari 6
Swansea 2 Arsenal 2
Mansfield 1 Liverpool 2
++++++++++++++++++++++
MANSFIELD 1 LIVERPOOL 2
Luis Suarez aliifungia Liverpool Bao la pili la utata kwa kuudhibiti mpira kwa mkono na kufunga walipoipiga Mansfield Bao 2-1 na kutinga Raundi ya 4 ya FA CUP.
Mansfield, Timu ambayo haipo kwenye Mfumo ‘rasmi’’ wa Ligi huko England, walikuwa nyuma kwa Bao moja mfungaji akiwa Mchezaji mpya wa Liverpool Daniel Sturridge, lakini walikuwa wakitawala, kuleta presha kubwa na kosakosa nyingi, ndipo Suarez akapiga Bao la pili kwa Liverpool ambalo lilikuwa na walakini mkubwa.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Mansfield 1
-Green Dakika ya 79
Liverpool 2
-Sturridge Dakika ya 7
-Suarez 59
+++++++++++++++++
Matt Green aliifungia Mansfield Bao moja lakini walishindwa kupata Bao la kusawazisha licha ya kuiletea Liverpool kashikashi kubwa.
VIKOSI:
Mansfield: Marriott, Thompson, Dempster, Geohaghon, Beevers, Meikle, Clements, Murray, Howell, Briscoe, Green. Subs: Sutton, Speight, Wright, Rhead, Hutchinson, Stevenson, Daniel.
Liverpool: Jones, Wisdom, Coates, Carragher, Robinson, Lucas, Allen, Shelvey, Suso, Sturridge, Downing. Subs: Gulacsi, Suarez, Henderson, Sterling, Coady, Skrtel, Flanagan.
Refa: Andre Marriner
SWANSEA 2 ARSENAL 2
Swansea na Arsenal itabidi warudiane baada ya kutoka sare ya Bao 2-2 kwenye Uwanja wa Liberty katika Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Swansea 2
-Michu Dakika ya 58
-Graham 87
Arsenal 2
-Podolski Dakika ya 81
-Gibbs 83
+++++++++++++++++
Michu alitoka Benchi na kuipa Swansea Bao la kuongoza lakini, ndani ya Dakika mbili, Arsenal walisawazisha kwa Bao la Lukas Podolski na kupiga la pili kupitia Kieran Gibbs.
Swansea walisawazisha Dakika 3 kabla Mechi kwisha kwa Bao la Danny Graham.
Timu hizi zitarudiana Januari 15 au 16 Uwanjani Emirates.
VIKOSI:
Swansea: Vaum, Tiendalli, Chico, Bartley, Davies, Dyer, Britton, de Guzman, Ki, Routledge, Graham
Akiba: Tremmel, Michu, Hernandez, Monk, Shechter, Rangel, Agustien.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Wilshere, Ramsey, Walcott, Giroud, Cazaula
Akiba: Martinez, Vermaelen, Rosicky, Podolski, Andre Santos, Oxlade-Chamberlain, Coquelin.
Refa: Howard Webb
++++++++++++++++++++++
FA CUP
RATIBA:
Jumatatu Januari 7
Cheltenham v Everton [SAA 4 Dak 45 Usiku]
++++++++++++++++++++++
MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
**FAHAMU: Kwa Timu zilizoenda sare kwenye Raundi ya 3 Mechi zake zitachezwa Januari 15 na 16.
Marudiano ya Swansea na Arsenal yatapangwa katika Tarehe hizo.
Jumanne Januari 15
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Leeds
Bournemouth v Wigan
Brentfaud v Southend
Leyton Auient v Hull
Wimbledon v Sheffield Wed
Stoke v Crystal Palace
Sunderland v Bolton
[SAA 5 Usiku]
Blackpool v Fulham
Jumatano Januari 16
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham
West Brom v QPR
RAUNDI YA 4
[KUCHEZWA WIKIENDI YA JANUARI 26]
Nauwich City v Luton Town
Oldham Athletic v Liverpool 
Macclesfield Town v Wigan Athletic au Bournemouth
Derby County v Blackburn Rovers
Hull City au Leyton Auient v Barnsley
Middlesbrough v Aldershot Town
Millwall v Aston Villa
Leeds United au Birmingham City v Tottenham Hotspur
Brighton & Hove Albion v Swansea City au Arsenal
Crystal Palace au Stoke City v Manchester City
West Ham United au Manchester United v Fulham au Blackpool
Southend United au Brentfaud v Chelsea
Reading v Sheffield United
Huddersfield Town v Leicester
QPR au West Brom v Sheffield Wednesday au MK Dons
Bolton au Sunderland v Cheltenham au Everton

No comments:

Post a Comment