Sunday, January 6, 2013

SERIE A & LA LIGA ZARUDI TENA KILINGENI! VIGOGO UWANJANI LEO!

>>LEO MIAMBA REAL, BARCA, JUVE, INTER MILAN, AC MILAN, DIMBANI!
BARCA_v_REALBAADA KUWA VAKESHENI, Ligi kali za Ulaya, Serie A huko Italy na La Liga huko Spain, zimeanza tena na hapo jana huko Italy, Lazio, ambayo ipo nafasi ya Pili, iliifunga Cagliari 2-0 na kuinyemelea Juventus iliyo kileleni na sasa kuwa Pointi 5 nyuma yao.
Huko Spain, La Liga ilianza tena juzi Ijumaa kwa Real Zaragoza kuchapwa nyumbani na Real Betis Bao 2-1 na kuendelea tena jana huku leo Vinara wake, Barcelona, watakuwa nyumbani kucheza Mechi yao ya kwanza ya Mwaka 2013 na Espanyol hii ikiwa Dabi ya Jiji la Barcelona.
Mabingwa watetezi, Real Madrid, walio nafasi ya 3, pia wapo nyumbani kucheza na Real Sociedad.
Huko Italy, Serie A itaendelea kunguruma leo kwa Mabingwa, ambao pia ni vinara, Juventus, kucheza na Sampdoria pamoja na kuwepo Mechi nyingine za Timu Vigogo kama vile AC Milan, Inter Milan huku Mechi ya mvuto ni kati ya Napoli na AS Roma.
SERIE A
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Januari 5
Catania 0 Torino 0
Lazio 2 Cagliari 0
Jumapili Januari 6
AC Milan v Siena
Chievo Verona v Atalanta
Juventus v Sampdoria
Parma v Palermo
Udinese v Inter Milan
Napoli v AS Roma
Genoa v Bologna
Fiorentina v Pescara
LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Januari 4
Real Zaragoza 1 Real Betis 2
Jumamosi Januari 5
Sevilla FC 1 Osasuna 0
Levante 3 Athletic de Bilbao 1
Granada CF 1 Valencia 2
Deportivo La Coruna 1 Malaga CF 0
Jumapili Januari 6
FC Barcelona v RCD Espanyol
Celta de Vigo v Real Valladolid
Real Mallorca v Atletico de Madrid
Real Madrid CF v Real Sociedad
Jumatatu Januari 7
Rayo Vallecano v Getafe CF

No comments:

Post a Comment