>>NI OLD TRAFFORD, SAA 5 USIKU!
BAADA
ya kunusurika kutolewa nje ya FA CUP hapo jana kwa Robin van Persie
kusawazisha Bao Dakika ya 90 na kuifanya Manchester United itoke sare
2-2 na West Ham Uwanjani Upton Park, Mechi hii ya Raundi ya 3 itarudiwa
Uwanjani Old Trafford Jumatano Januari 16 kuanzia Saa 5 Usiku.
Mechi nyingine za Raundi ya 3 zilizotoka
sare hapo jana zimepangwa kurudiwa Jumanne Januari 15 na moja ipo
Jumatano Januari 16 kama ya Man United.
Leo, Raundi ya 3 inaenedelea kwa Mechi
mbili, Swansea v Arsenal [SAA 10 na Nusu Jioni] na Mansfield v Liverpool
[SAA 1 Usiku] na Mechi ya mwisho ya Raundi ya 3 ni kesho ya Cheltenham v
Everton [SAA 4 Dak 45 Usiku]
Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya 4 zitakazochezwa Wikiendi ya Januari 26 itafanyika baadae leo.
MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
Jumanne Januari 15
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Leeds
Bournemouth v Wigan
Brentford v Southend
Leyton Orient v Hull
Wimbledon v Sheffield Wed
Stoke v Crystal Palace
Sunderland v Bolton
[SAA 5 Usiku]
Blackpool v Fulham
Jumatano Januari 16
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham
West Brom v QPR
No comments:
Post a Comment