Sunday, December 30, 2012

WALCOTT ATABAKIA - WENGER.


MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa mshambuliaji wake nyota Theo Walcott atabakia klabuni hapo baada ya kuisaidia kupata ushindi mnono kwa mabao matatu aliyofunga katika Uwanja wa Emirates dhidi ya Newcastle. Arsenal ilifanikiwa kuisambaratisha Newcastle kwa mabao 7-3 ambao ushindi huo unakuwa watatu mfululizo baada ya kutolewa katika Kombe la Ligi na Bradford City inayoshiriki Ligi Daraja la pili. Walcott alionyesha kuimudu vyema nafasi ambayo anaitaka ya kuwa mshambuliaji wa kati akifunga bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza kabla ya kufunga mengine mawili katika kipindi cha pili na kukabidhiwa mpira baada ya mchezo huo kwa kufunga hat-trick. Nyota huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 23 bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo pamoja na kuahidiwa kuongezewa marupurupu. Lakini Wenger alionyeshwa kufurahishwa na kiwango cha nyota huyo na ana matumaini watafikia makubaliano kuhusu mkataba wake mpya.

No comments:

Post a Comment