WENYEJI wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013,
Afrika Kusini wametangaza Kikosi chao cha Wachezaji 23 kwa ajili ya
Mashindano hayo yatakayochezwa Nchini kwao kuanzia Januari 19 hadi
Februari 10.
Akitangaza Kikosi hicho, Kocha Mkuu wa
Bafana Bafana Gordon Igesund, amesema ni bahati mbaya hawezi kuchukua
zaidi ya Wachezaji 23 lakini anaamini wale walioteuliwa wataiwakilisha
vyema Afrika Kusini.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Nahodha wa Kikosi hicho ni Bongani Khumalo.
Kabla ya kuanza rasmi AFCON 2013,
Bafana Bafana watacheza Mechi mbili za Kirafiki dhidi ya Norway Mjini
Cape Town, Afrka Kusini hapo Januari 8 na Januari 12 kucheza na Algeria
huko Soweto, Johannesburg.
Afika Kusini watacheza Mechi ya ufunguzi ya AFCON 2013 dhidi ya Cape Verde Januari 19 Uwanjani Soccer City Mjini Johannesburg.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Itemeleng Khune, Wayne Sandilands, Senzo Meyiwa
MABEKI: Bongani Khumalo, Siboniso Gaxa, Siyabonga Sangweni, Anele Ngcongca, Tsepo Masilela, Thabo Nthethe, Thabo Matlaba
VIUNGO: Lerato
Chabangu, Thulani Serero, Kagisho Dikgacoi, Dean Furman, Reneilwe
Letsholonyane, Siphiwe Tshabalala, May Mahlangu, Thuso Phala, Oupa
Manyisa
MASTRAIKA: Bernard Parker, Tokelo Rantie, Lehlohonolo Majoro, Katlego Mphela.
No comments:
Post a Comment