RONALDINHO ATAMANI MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA 2014.
MSHAMBULIAJI nyota wa
kimataifa wa Brazil, Ronaldinho Gaucho ameeleza kuwa anahitaji kuwamo
katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitashiriki
michuano ya Kombe la Dunia 2014. Nyota
huyo wa zamani wa Barcelona ana matumaini kuwa atakuwa sehemu ya kikosi
kitakachoshiriki michuano hiyo katika kipindi cha miezi 18 ijayo ambayo
itaandaliwa nchini kwake. Ronaldinho
amesema hakuna kitu kinacholeta furaha kama kucheza michuano ya Kombe
la Dunia mbele ya mashabiki wa nyumbani na hapendi kupoteza nafasi hiyo
muhimu. Kwasasa
nyota huyo ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Atletico Mineiro
amekuwa akipambana kurejesha makali yake ya zamani ili aweze kuitwa
katika kikosi hicho na anaamini katika kipindi cha miezi 18 ijayo
atakuwa amefikia kiwango hicho. Luiz
Felipe Scolari ambaye ameisaidia Brazil kunyakuwa Kombe la Dunia mwaka
2002 wakati huo Ronaldinho akiwa ndio nyota nchi hiyo ndio amekabidhiwa
tena mikoba ya kuinoa timu ya taifa Novemba.
No comments:
Post a Comment