MILANOV MCHEZAJI BORA WA MWAKA BULGARIA.
CHAMA cha Waandishi wa
Habari za Michezo nchini Bulgaria-PFC kimemteua mshambuliaji wa klabu ya
Litex Lovech, Georgi Milanov kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo
mbele ya wachezaji wengine nyota akiwemo Dimitar Berbatov anayecheza
katika klabu ya Fulham ya Uingereza. Milanov
mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni mchezaji mdogo kuwahi kushinda tuzo
hiyo na mchezaji wa kwanza ambaye anacheza soka chini humo kushinda tuzo
hiyo toka mwaka 2001. Kiungo
huyo amefunga mabao nane katika michezo 14 aliyocheza na kuwa mhimili
wa kuisaidia klabu yake kukwea mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa
Ligi Kuu nchini humo. Akihojiwa
mara baada ya sherehe hizo nyota huyo amesema ni heshima kubwa kwake
kupokea tuzo huyo na kuwashukuru waandaji, wachezaji wenzake pamoja na
kocha wake Hristo Stoichkov kwa kumsaidia kufikia kiwango alichonacho
hivi sasa.
No comments:
Post a Comment