Monday, January 7, 2013

MASHALI KUTETEA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI.


Mabondia nane wanatarajiwa kupambana katika mapambano ya utangulizi katika mpambano wa kutetea Ubingwa wa afrikia mashariki na kati kati ya Mtanzania Thomas Mashali na Bernad Mackoliech wa Kenya katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Januari 12 siku ya Mapinduzi.Akizingumza na Waandishi wa habari mratibu wa pambano hilo Aisha Mbegu aliwataja mabondia hao kuwa ni Amadu Mwalimu atakayepambana na Cosmas Chibuga Bakari Dunda na Godfrey Pancho, Shadrack Juma na Nasoro Juma wakati Abdul Awilo atapambana na Six Juma.“ Tumueamua kuwa na mapambano machache ya utangulizi ili kutoa fursa kwa watu kuangalia mapema pambano amabalo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi kutokana na tambo za Mashali kuahidi ushindi kwa K.O, aslisema Aisha.Aisha alisema mapamnabo ya utangul;izi yatakuwa ya raundi nne na mpaka sasa maandalizi yako vizuri na Mashali amesharejea Jijini Dar es salaam na anaendelea na mazoezi kwa ajili ya pambano hilo litakalofanyika siku ya Mapinduzi.Kwa upande wake rais wa TPBO Yaasin Abdalah alisema maandalizi yamekamilika na Tiketi kwa Ajili ya bondia mackoliech na kocha wake imeshatumwa na kupokelewa kinachosubiriwa ni wao kuwasili nchini kwa ajili ya pambano.Bondia Thomas Mashali anatetea ubingwa huo alioupata Oktoba 14 baada ya kumpiga bondia Medi Sebyala wa Uganda kwa pointi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese.

No comments:

Post a Comment