DJOKOVIC ANYAKUWA TAJI LA MUBADALA.
MCHEZAJI tenisi nyota
anayeshika namba moja duniani, Novak Djokovic ameanza msimu mpya wa
michuano ya tenisi baada ya kumfunga Nicolas Almagro kwa 6-7 6-3 6-4
katika fainali ya mashindano ya maonyesho ya Mubadala iliyofanyika
jijini Abu Dhabi. Djokovic
ambaye alionyesha kiwango kizuri katika mchezo wa nusu fainali baada ya
kumtoa David Ferrer anayeshika namba tano wakati Almagro ambaye aliziba
nafasi ya Rafael Nadal aliyejitoa alimfunga Janko Tipsarevic. Akihojiwa
mara baada ya ushindi huo Djokovic alifurahia kunyakuwa taji la
michuano hiyo ya Abu Dhabi kwa mara nyingine na kuwasifu wapinzani wake
aliokutana nao kwamba walimpa changamoto kubwa ambayo itamsaidia katika
michuano iliyo mbele yake. Wachezaji
wote wanne walioshirki michuano hiyo wanatarajiwa kuelekea nchini
Australia kwa ajili ya michuano ya wazi itakayoanza Januari 14 jijini
Melbourne huku Djokovic akiwa bingwa mtetezi.
No comments:
Post a Comment