Sunday, February 24, 2013

CAPITAL ONE CUP FAINALI JUMAPILI: BRADFORD CITY v SWANSEA CITY

CAPITAL_ONE_CUP-BESTUWANJA: Wembley
TAREHE : Jumapili Februari 24
SAA: 1 Usiku
Bradford City, Timu ya Daraja la chini, Ligi 2, Madaraja matatu chini ya wapinzani wao Swansea City,  inawania kutwaa CAPITAL ONE CUP na hivyo kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao.
ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU ZA FAINALI HIYO:
+++++++++++++++++++++++++++
HALI za TIMU:
Bradford City watamcheki Beki wao Rory McArdle kama yuko fiti baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kuumia enka lakini hawataweza kumchezesha Straika Andy Gray  kwa vile alishaichezea Leeds United kwenye Mashindano haya.
Swansea itamkosa Beki wao Chico Flores ambae ana tatizo la enka.
Meneja wa Swansea, Michael Laudrup, ameshatangaza kuwa Kipa wa Akiba Gerhard Tremmel ndia atakeacheza Fainali hii.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
WAMEFIKAJE FAINALI
SWANSEA CITY:
-RAUNDI ya 2: SWANSEA 3 BARNSLEY 1
-RAUNDI ya 3: CRAWLEY 2 SWANSEA 3
-RAUNDI ya 4: LIVERPOOL 1  SWANSEA 3
-ROBO FAINALI: SWANSEA 1 MIDDLESBROUGH 0
-NUSU FAINALI 1: CHELSEA 0 SWANSEA 2
-NUSU FAINALI 2 : SWANSEA 0 CHELSEA 0
BRADFORD CITY:
-RAUNDI ya 1: NOTTS COUNTY 0 BRADFORD 1 (Dakika 120)
-RAUNDI ya 2: WATFORD 1 BRADFORD 2
-RAUNDI ya 3: BRADFORD 3 BURTON ALBION 2 (Dakika 120)
-RAUNDI ya 4: WIGAN 0 BRADFORD 0 (Dakika 120, Penati 4-2)
-ROBO FAINALI: BRADFORD 1 ARSENAL 1 (Dakika 120, Penati 3-2)
-NUSU FAINALI 1: BRADFORD 3 ASTON VILLA 1
-NUSU FAINALI 2: ASTON VILLA 2 BRADFORD 1 (Bradford wapita 4-3]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
BRADFORD_CITYTATHMINISWANSEA_CITY
Ni Fainali inayokutanisha Timu ya Daraja la chini, Bardford City, ambayo iko Ligi 2, ikiwa ni Madara matatu toka walipo wapinzani wao Swansea City, ambao wako BPL, Barclays Premier League.
Bradford City, chini ya Kocha Phil Parkinson, wametinga Fainali hii kwa kushinda Mechi 4 kati ya 7 kwenye Mashindano haya kwa Mechi kuchezwa Dakika 120 na mbili kati ya hizo kwa Mikwaju ya Penati 5 walipozibwaga Timu kubwa toka BPL, Wigan na Arsenal.
MICHUPia, Bradford wana historia ambayo bila shaka itaitetemesha Swansea ikiwa Mechi itafikia hatua ya kuamuliwa Mshindi kwa Mikwaju ya Penati 5 kwani wao wameshinda hatua hiyo mara 9 mfululizo.
Msimu huu Swansea, chini ya Meneja Michal Laudrup na wakiwa na Straika hatari kutoka Spain Michu, wamekuwa wakicheza Kandanda safi na kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu England wakiwa nafasi ya 7.
USO kwa USO:
-Hii itakuwa Mechi ya kwanza kwa Bradford na Swansea kukutana katika Kikombe kikubwa.
-Swansea hawajafungwa katika Mechi 4 za Ligi walizokutana mwisho na Bradford, zote zikiwa ni za Ligi 1, lakini tatu kati ya hizo zilikuwa ni sare.
-Mara ya mwisho Bradford kuifunga Swansea ilikuwa ni Bao 5-1 Uwanjani Valley Parade kwenye Ligi 1 hapo Machi 30 Mwaka 1996.
REKODI:
Bradford City
Bradford ni Timu ya pili kutoka Darala chini, Ligi 2, kufika Fainali ya Kombe la Ligi.
Timu nyingine ilikuwa ni Rochdale Mwaka 1962 ambayo ilifungwa na Norwich iliyokuwa Daraja la Pili.
Ikiwa Bradford itanyakua Kombe, itakuwa ni Timu ya 6 kufanya hivyo bila kuwa Ligi ya juu kabisa nyingine zikiwa ni Norwich (Daraja la 2, 1962), QPR (Daraja la 3, 1967), Swindon (Daraja la 3, 1969), Aston Villa (Daraja la 2, 1975) na Sheffield Wednesday (Daraja la 2, 1991).
Swansea City
Hii ni mara ya kwanza kwa Swansea City kutinga Fainali ya Kombe hili na kabla walikuwa hawajawahi kuvuka Raundi ya 4 ya Mashindano haya.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Bradford (Mfumo: 4-4-2): Duke; Darby, Nelson, McArdle, McHugh; Hines, G Jones, Doyle, Reid; Wells, Hanson.
Swansea (Mfumo: 4-5-1): Tremmel; Rangel, Monk, Williams, Davies; Dyer, Hernandez, Ki, De Guzman, Routledge; Michu.
Refa: Kevin Friend [Mechi: 23 Kadi Nyekundu: 1 Kadi Njano: 74]
WASHINDI WA LIGI CUP WALIOPITA:
1961 Aston Villa 0–2
1963 Birmingham City
1964 Leicester City
1965 Chelsea
1966 West Bromwich Albion
1967 Queens Park Rangers
1968 Leeds United
1969 Swindon Town
1970 Manchester City
1971 Tottenham Hotspur
1972 Stoke City
1973 Tottenham Hotspur
1974 Wolverhampton Wanderers
1975 Aston Villa
1976 Manchester City
1977 Aston Villa
1978 Nottingham Forest
1979 Nottingham Forest
1980 Wolverhampton Wanderers
1981 Liverpool
1982 Liverpool
1983 Liverpool
1984 Liverpool
1985 Norwich City
1986 Oxford United
1987 Arsenal
1988 Luton Town
1989 Nottingham Forest
1990 Nottingham Forest
1991 Sheffield Wednesday
1992 Manchester United
1993 Arsenal
1994 Aston Villa
1995 Liverpool
1996 Aston Villa
1997 Leicester City
1998 Chelsea
1999 Tottenham Hotspur
2000 Leicester City
2001 Liverpool
2002 Blackburn Rovers
2003 Liverpool
2004 Middlesbrough
2005 Chelsea
2006 Manchester United
2007 Chelsea
2008 Tottenham Hotspur
2009 Manchester United
2010 Manchester United
2011 Birmingham City
2012 Liverpool

No comments:

Post a Comment