Sunday, February 24, 2013

BPL: MAN CITY YAICHAPA CHELSEA, YAIKARIBIA UNITED POINTI 12 NYUMA!


>>MAN CITY 2 CHELSEA 0, LAMPARD AKOSA PENATI, YAYA & TEVEZ WAUA!!
>>CHELSEA 4 BORA HATARINI, SPURS WAKO POINTI 1 NYUMA, ARSENAL 2 NYUMA!!
BPL_LOGOMABINGWA watetezi wa BPL, Barclays Premier League, Manchester City, wakicheza kwao Uwanja wa Etihad, leo wameichapa Chelsea Bao 2-0 na kujichimbia nafasi ya pili na kuwasogelea Vinara wa Ligi Man United kwa kuwa Pointi 12 nyuma yao Mechi zikiwa zimebaki 11 lakini Chelsea sasa wapo hatarini kwenye 4 bora kwani wako nafasi ya 3 na nyuma yao kwa Pointi 1 tu ni Tottenham walio na Mechi 1 mkononi na wanafuatia Arsenal walio nafasi ya 5 Pointi 2 nyuma ya Tottenham.

MATOKEO:
Jumapili Februari 24
Manchester City 2 Chelsea 0
Newcastle United 4 Southampton 2

NEWCASTLE 4 SOUTHAMPTON 2
PAPISS_CISSENewcastle walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuishinda Southampton, iliyo nafasi za hatari za kushushwa Daraja, Bao 4-2 katika Mechi iliyochezwa St James Park.
Ushindi huu umeipandisha Newcastle nafasi kadhaa katika Msimamo wa Ligi Kuu England na sasa wapo nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 30 zikiwa ni Pointi ni Pointi 6 juu ya zile Timu 3 za mkiani ambayo ni sehemu ya hatari kwani ni eneo la kuporomoka Daraja mwishoni mwa Msimu.

MAGOLI:
Newcastle 4
-Sissoko Dakika ya 33
-Cisse 42
-Cabaye 67 (Penati)
-Hooiveld 79 (Kajifunga mwenyewe)
Southampton 2
-Schneiderlin Dakika ya 3
-Lambert 50

Morgan Schneiderlin aliifungia Southampton Bao la kwanza na  Moussa Sissoko kusawazisha kisha likaja shuti kali la Papiss Cisse liliowafanya Newcastle waongoze lakini Rickie Lambert akaifanya Mechi iwe 2-2.
Newcastle walipachika Bao la 3 kwa Penati iliyofungwa na Yohan Cabaye kufuatia Danny Fox kuunawa mpira na Bao la 4 alijifunga mwenyewe Jos Hooiveld ambae sasa ameifikia rekodi ya Ligi Kuu England ya kujifunga mwenyewe Bao 3 katika Msimu mmoja.
VIKOSI:
Newcastle: Elliot, Debuchy, Coloccini, Steven Taylor, Santon, Tiote, Cabaye, Sissoko, Gutierrez, Gouffran, Cisse
Akiba: Alnwick, Anita, Yanga-Mbiwa, Perch, Marveaux, Shola Ameobi, Obertan.
Southampton: Boruc, Clyne, Hooiveld, Yoshida, Shaw, Steven Davis, Schneiderlin, Cork, Lallana, Rodriguez, Lambert
Akiba: Kelvin Davis, Fonte, Ramirez, Fox, Ward-Prowse, Mayuka, Puncheon.
Refa: Chris Foy
MAN CITY 2 CHELSEA 0
Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0 licha ya Man City kuitawala na Kipindi cha Pili Chelsea MANCINI_ALIAwalipata Penati katika Dakika 52 baada ya Kipa Joe Hart kumwangusha Demba Ba lakini Frank Lampard alishindwa kufunga kwa Kipa Joe Hart kuokoa.
Kwa mshangao wa wengi, licha ya Refa Andre Marriner kutoa Penati, Kipa Joe Hart hakupewa hata Kadi ya Njano.
Hiyo ilikuwa changamoto kwa Man City na Yaya Toure alifunga Bao zuri katika Dakika ya 63 akiwa katikati ya msitu wa Mabeki na Carlos Tevez, aleingizwa Kipindi cha Pili, alipachika Bao la pili katika Dakika ya 85.
VIKOSI:
Man City: Hart, Zabaleta, Toure, Nastasic, Clichy, Javi Garcia, Toure, Rodwell, Milner, Aguero, Silva
Akiba: Pantilimon, Lescott, Nasri, Dzeko, Sinclair, Kolarov, Tevez.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Mikel, Lampard, Ramires, Hazard, Mata, Ba
Akiba: Turnbull, Torres, Oscar, Moses, Terry, Azpilicueta, Bertrand.
Refa: Andre Marriner

RATIBA
BPL: BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Jumatatu Februari 25
[Saa 5 Usiku]
West Ham United v Tottenham Hotspur
Jumamosi Machi 2
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v West Bromwich Albion
Everton v Reading
Manchester United v Norwich City
Southampton v Queens Park Rangers
Stoke City v West Ham United
Sunderland v Fulham
Swansea City v Newcastle United
[Saa 2 na Nusu Usiku]
Wigan Athletic v Liverpool
Jumapili Machi 3
[Saa 1 Usiku]
Tottenham Hotspur v Arsenal
Jumatatu Machi 4
[Saa 5 Usiku]
Aston Villa v Manchester City

MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 27 isipokuwa inapotajwa]
1 Man United Pointi 68
2 Man City 56
3 Chelsea 49
4 Tottenham Mechi 26 Pointi 48
5 Arsenal 47
6 Everton 42
7 WBA 37
9 Liverpool 39
9 Swansea 37
10 Stoke 33
11 Fulham 32
12 Norwich 32
13 West Ham Mechi 26 Pointi 30
14 Newcastle 30
15 Sunderland 29
16 Southampton 27
17 Wigan 24

18 Aston Villa 24
19 Reading 23
20 QPR 17

No comments:

Post a Comment