Sunday, February 24, 2013

CAF SUPER CUP: AL AHLY YATWAA KOMBE!


CAF_LOGOAL AHLY ya Misri jana ilitwaa CAF SUPER CUP kwa kuifunga AC Leopards ya Congo Brazzaville Bao 2-1 katika Mechi ilitochezwa Uwanja wa Borg El Arab uliopo Ukanda wa Kitalii kando kando mwa Bahari ya Mediterranean.
Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Jeshi na kushuhudiwa na Washabiki, kitu ambacho hivi sasa huko Misri ni cha nadra, kwa vile Watazamaji hawaruhusiwi kwa sababu ya kiusalama tangu yatokee mauuaji Uwanjani Port Said Februari Mwaka jana.
Hii ni mara ya 5 katika Miaka 11 kwa Al Ahly kutwaa CAF SUPER CUP ambalo hushindaniwa na Washindi wa CAF CHAMPIONS LIGI, safari hii Al Ahly, na Mshindi wa Kombe la Shirikisho, safari hi AC Leopards.
Bao za Al Ahly zilifungwa na Chipukizi Rami Rabiea, Dakika ya 55, na Mkongwe Mohamed Barakat, Dakika ya 72.
Bao pekee la AC Leopards lilifungwa Dakika ya 77 na Nahodha wao Rudi Ndey ambae pia nusura asawazishe Dakika za mwishoni lakini shuti lake likaokolewa kwenye mstari wa goli.
Al Ahly, licha ya kutwaa Kombe, pia walipewa kitita cha Dola 75,000 na AC Leopards kupewa Dola 50,000.
WASHINDI WALIOPITA:
1993 Africa Sports National
1994 Zamalek SC
1995 ES Tunis
1996 Orlando Pirates FC
1997 Zamalek SC
1998 ES Sahel
1999 ASEC Mimosas
2000 Raja CA Casablanca
2001 Hearts of Oak SC
2002 Al Ahly SC
2003  Zamalek SC
2004 Enyimba International FC
2005 Enyimba International FC
2006 Al Ahly SC
2007 Al Ahly SC
2008 ES Sahel
2009 Al Ahly SC
2010 TP Mazembe
2011 TP Mazembe
2012 Maghreb AS Fez

No comments:

Post a Comment