Sunday, February 24, 2013

BAYERN YAFUMUA, BARCA, REAL ZOTE USHINDI 2-1, DABI MILANO LEO!!


>> DABI MILANO: JUMAPILI NI INTER MILAN v AC MILAN
MESSI_ASHANGILIA_GOLIVINARA wa La Liga, Barcelona, wamezidi kujongelea Ubingwa, baada ya kuichapa Sevilla kwa Bao 2-1 hii ikiwa ni Mechi yao ya kwanza toka wapokee kichapo kule San Siri mikononi mwa AC Milan katika UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Sevilla ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Botid, Dakika ya 42, na Barca kusawazisha Dakika ya 51, kwa Bao la David Villa, na Lionel Messi kufunga Bao la pili, Dakika ya 60.
Bao 2 za Kipindi cha Pili, za Gonzalo Higuain na Kaka, zimewapa ushindi Real Madrid wa ugenini dhidi ya Deportivo La Coruna.
Deportivo ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 34 la Riki na Real kupiga Bao Dakika ya 73, Mfungaji Kaka, na Dakika ya 88 la Higuain.
Winga wa Real, Angelo Di Maria, alitolewa kwa Kadi Nyekundu Dakika ya 90 kufuatia Kadi za Njano mbili mfululizo.
Kwenye, Bundesliga, vinara, Bayern Munich, waliifumua Werder Bremen Bao 6-1 na kujichimbia kileleni wakiwa Pointi 18 mbele ya Mabingwa Borussia Dortmund ambao leo wanacheza ugenini na Borussia Mönchengladbach.
BAADA ya kuwachapa FC Barcelona, AC Milan Jumapili wana kibarua kipya kwenye Serie A watakapocheza Dabi ya Jiji la Milano “ugenini” na Mahasimu wao wakubwa Inter Milan Uwanjani San Siro, Uwanja ambao kwa Mahasimu hao wote wawili ndio Nyumbani, huku AC Milan wakikamata nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 44 na Inter wapo nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 43.
RATIBA/MISIMAMO:
LA LIGA
Ijumaa Februari 22
Athletic de Bilbao 1 Real Sociedad 3
Jumamosi Februari 23
Real Mallorca 1 Getafe CF 3
Real Zaragoza 2 Valencia 2
Deportivo La Coruna 1 Real Madrid CF 2
FC Barcelona 2 Sevilla FC 1
Jumapili Februari 24
Rayo Vallecano v Real Valladolid
Celta de Vigo v Granada CF
Atletico de Madrid v RCD Espanyol
Real Betis v Malaga CF
Jumatatu Februari 25
Levante v Osasuna
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 25 isipokuwa inapotajwa]
1 Barcelona 68
2 Atletico Madrid Mechi 24 Pointi 53
3 Real Madrid 52
4 Malaga Mechi 24 Pointi 42
5 Valencia 41
6 Real Sociedad 40

SERIE A
Jumamosi Februari 23
Palermo 0 Genoa 0
Jumapili Februari 24
Sampdoria v Chievo Verona
Atalanta v AS Roma
Bologna v Fiorentina
Juventus v Siena
Parma v Catania
Cagliari v Torino FC
Inter Mila v AC Milan
Jumatatu Februari 25
Udinese v Napoli
SS Lazio v Pescara
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 25]
1 Juventus Pointi 55
2 Napoli 51
3 AC Milan 44
4 Lazio 44
5 Inter Milan 43
6 Fiorentina 42
7 Catania 39

BUNDESLIGA
Ijumaa Februari 22
SC Freiburg 0 Eintracht Frankfurt 0
Jumamosi Februari 23
Bayern Munich 6 SV Werder Bremen 1
Hannover 5 Hamburger SV 1
VfB Stuttgart 1 FC Nuremberg 1
FSV Mainz 1 VfL Wolfsburg 1
FC Augsburg 2 TSG Hoffenheim 1
Schalke 2 Fortuna Dusseldorf 1
Jumapili Februari 24
Borussia Mönchengladbach v BV Borussia Dortmund
SpVgg Greuther Furth v Bayer 04 Leverkusen
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 23 isipokuwa inapotajwa]
1 Bayern Munich Pointi 60
2 Borussia Dortmund Mechi 22 Pointi 42
3 Bayer Leverkusen Mechi 22 Pointi 41
4 Eintracht Frankfurt 38
5 Freiburg 35
6 Hamburger 34
7 Hannover 33
8 Mainz 32
9 Schalke

No comments:

Post a Comment