Wednesday, January 9, 2013

DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE JANA ALIHUTUBIA WANANCHI WA MKOA WA TABORA KATIKA VIWANJA VYA CHIPUKIZI KATIKATI YA MJI W ATABORA NA KUZINDUA JUMLA YA MIRADI MIKUBWA MITATU


Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi la barabara ya Tabora-Ndono yenye urefu wa kilometa 42 yenye thamani ya shilingi bilioni 53.4,barabara ya Nyahua-Tabora yenye urefu wa kilometa 85 yenye thamani ya sh. bilioni 93.4



Amesema kuwa baada ya wakazi wa mkoa wa Tabora kusubiri kwa muda mrefu barabara ya lami itakayo iunganisha na mikoa mingine sasa ni wasaa wa mkoa huo kunufaika na barabara hiyo ambayo tayari imekwishaanza kutengenezwa
Raisi Kikwete akamtaka waziri wa ujenzi Mh.John Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa barabara zinazojengwa mkoani Tabora zinajengwa katika kiwango kizuri na kinachotakiwa
Raisi Kikwete ameweka mawe hayo ya msingi wakati akiwa katika ziara yake ya siku tano kikazi mkoani Tabora
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikilia maelezo ya Meneja wa TANESCO wa Nzega akielezea mikakati ya kuwapatia wakazi wa hapo nishati hiyo Jumatatu mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Uyui toka kwa mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Lucy Mayenga wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Tabora Mjini toka kwa mkuu wa Wilaya hiyo Mhe  Suleiman Kumchaya  wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya ujenzi wa barabara ya Tabora-Ndono kabla hajazindua rasmi ujenzi wa  barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akika utepe kuzindua rasmi  ujenzi wa barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
 

No comments:

Post a Comment