Wednesday, January 9, 2013

KIPINDI CHA MWANAMAMA OPRAH WINFREY KUFANYA MAHOJIANO NA MWENDESHA BAISKELI ARMSTRONG.


MWENDESHA baiskeli kutoka Marekani, Lance Armstrong anatarajia kufanya mahojiano katika kipindi maarufu cha mazungumzo cha mwamama Oprah Winfrey huku kukiwa na ripori kuwa nyota huyo anaweza kukiri hadharani kutumia madawa ya kuongeza nguvu. Armstrong alivuliwa mataji yake yote saba ya Toure de France na Shirikisho la Waendesha Baiskeli Duniani kufuatia taarifa iliyotolewa na kitengo cha kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni. Winfrey ambaye anaendesha kipindi cha OWN network aliandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wake wa kijamii wa twitter kuwa atafanya mahojiano ya dakika 90 na Armstrong kuzungumzia tuhuma za matumizi ya dawa za kuongeza nguvu zilizokuwa zikimkabili miaka mingi. Pamoja na kufungiwa maisha kushiriki mchezo mashindano ya baiskeli Armstrong amekuwa akiendelea kukana tuhuma hizo lakini kuna ripoti iliyotolewa Ijumaa iliyopita na gazeti la New York Times imedai kuwa nyota huyo mwenye miaka 41 anafikiria kukiri hadharani kufanya hivyo ili aweze kupunguziwa adhabu aliyopewa.

No comments:

Post a Comment