Thursday, October 18, 2012

SIMBA NA KAGERA WACHANGA MILIONI 58

Benjamin Effe wa Kagera Sugar akimdhibiti Mrisho Ngassa wa Simba katika mechi ya jana

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Kagera Sugar iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 limeingiza sh. 58,505,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, watazamaji 9,842 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 11,013,785.54 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,924,491.53.
Amesema mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 440,000, mtathimini wa waamuzi sh. 254,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Amesema umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,183,890. Gharama za mchezo sh. 3,671,261.85, uwanja sh. 3,671,261.85, Kamati ya Ligi sh. 3,671,261.85, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,202,757.11 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,468,504.74.
Katika mechi hiyo, Simba ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Ngassa tangu ajiunge na Simba katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja, akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.

TFF YAFUNGA NDOA NA FKF YA KENYA

Rais wa TFF, Tenga

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Kenya (FKF) wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuinua kiwango cha mpira wa miguu katika nchi hizo.
Akizungumza baada ya mkutano uliowakutanisha vinara wa mashirikisho hayo Dar es Salaam jana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema wameamua kurejesha uhusiano huo uliokuwepo zamani baada ya kuwepo utulivu katika uendeshaji mpira wa miguu nchini Kenya.
Amesema maeneo ya ushirikiano ambayo wameagiza yafanyiwe kazi na sekretarieti za pande zote (TFF na KFF) ili baadaye yaingizwe katika Hati ya Makubaliano (MoU) ni mafunzo, waamuzi, mechi za timu za Taifa za wakubwa, vijana na wanawake, na Ligi Kuu.
Rais Tenga pia amesema wameamua kuwepo ziara za mafunzo (study tours) katika maeneo mbalimbali ambapo kwa Kenya wao Ligi Kuu yao iliingia katika mfumo wa kampuni mapema, hivyo itakuwa fursa nzuri kwa Bodi ya Ligi Kuu ambayo iko kwenye mchakato wa kuanzishwa kupata uzoefu kwa wenzao wa Kenya.
Naye Rais wa FKF, Sam Nyamweya aliyefuatana na Makamu wake wa Rais, Robert Asembo amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya ni wa kihistoria, hivyo wameamua kuuanzisha upya kwa faida ya nchi hizo.
Amesema hivi karibuni FKF ilichukua waamuzi kutoka Tanzania waliochezesha mechi ya kirafiki kati ya Kenya (Harambee Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana), hivyo wameamua kubadilishana waamuzi kwa lengo la kuwaongezea uzoefu.
“Waamuzi wa Tanzania walichezesha vizuri mechi ile. Unajua kwetu kuna upinzani mkubwa katika klabu kama AFC Leopards na Gor Mahia, ukipanga refa utasikia wengine wanalalamika, mara huyo ni Mjaluo. Hata akichezesha vizuri bado watalalamika tu kutokana na upinzani uliopo katika klabu hizo,” amesema.
Rais Nyamweya ameongeza kuwa ili kuondoa malalamiko katika mechi za aina hiyo wanaweza kuchukua waamuzi kutoka Tanzania, na vilevile waamuzi kutoka Kenya wakachezesha mechi za aina hiyo nchini Tanzania.
Amesema vilevile wamepanga kuangalia uwezekano wa kuwa na mechi za kuandaa timu kabla ya kuanza Ligi Kuu za nchi hizo ambapo washindi watatu au wanne wa kwanza katika ligi hizo kushindana.
Kwa upande wa mafunzo, wamekubaliana kuwa kwa vile kila nchi ina wakufunzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na la Afrika (CAF) watawatumia kuandaa mafunzo ya mara kwa mara kwa waamuzi, makocha, madaktari wa tiba ya michezo na viongozi badala ya kusubiri mafunzo ya aina hiyo kutoka kwa mashirikisho hayo ya kimataifa.

UEFA YAMTUNUKU TUZO RONALDO KWA MECHI 100

Ronaldo
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amepewa tuzo na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), baada ya kufikisha mechi 100 za kuichezea timu yake ya taifa, Ureno.
Katika mechi zake 100, Ronaldo amefunga mabao 37; bao lake la kwanza akifunga katika ushindi wa 2-1 timu yake ikifungwa na Ugiriki katika hatua ya makundi ya Euro 2004. 
Akiwa ana umri wa miaka 27, Ronaldo anakuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kufikisha idadi hiyo ya mechi, baada ya Wajerumani Lukas Podolski na Estonia's Kristen Viikmäe.
Nyota huyo wa Real Madrid amesema katika taarifa yake kwenye ukurasa wake wa Facebook, akizungumzia mechi zake 100. 
"Nakumbuka ilikuwa Agosti 20, mwaka 2003 dhidi ya Kazakhstan kwa mara ya kwanza nilipovaa jezi ya Ureno ya timu ya taifa ya wakubwa,"alikumbushia.
Mabao 11 zaidi yatamfanya Ronaldo ampiku Pauleta kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Ureno na anahitaji mechi 28 zaidi kumpiku Luis Figo. 
Kwa sasa, Ureno ina pointi tano katika Kundi F ikichuana na Urusi kileleni katika kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014. 

KIIZA DIEGO AREJEA KUONGEZA NGUVU YANGA

Kiiza

HAMISI Friday Kiiza maarufu Diego Milito, amerejea jana Dar es Salaam na leo anaingia kambini, Uplands Hotel, Changanyikeni kuungana na wenzake kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiiza alikuwa Uganda, kuichezea timu yake ya taifa, The Cranes katika mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini.
Uganda ilitolewa na Zambia kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, Zambia wakianza kushinda nyumbani 1-0 na Uganda wakashinda kwao 1-0 pia mwishoni mwa wiki, hivyo mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti, ambako timu ya Kiiza ilitolewa.
Pamoja na kuweka kambi Changanyikeni, lakini Yanga inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Beki Kevin Yondan aliyeumizwa na kiungo wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ katika mechi baina ya wapinzani hao wa jadi, Oktoba 3, mwaka huu, anaendelea vizuri na mazoezi mepesi sawa na mshambuliaji Said Bahanuzi aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Bahanuzi ‘Spider Man’ alichanika nyama za paja la mguu wa kulia katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba Jumatatu wiki iliyopita.
Bahanuzi aliumia dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete katika mechi ambayo Yanga ililala 1-0, beo pekee la Themi Felix.
Bahanuzi ndiye tegemeo la mabao la Yanga kwa sasa, kwani tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, ameifungia mabao 12 katika mechi 13, ikiwemo ile dhidi ya Kagera aliyocheza kwa dakika 23 kabla ya kuumia na kutoka. 
Yanga kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 11, baada ya kucheza saba, kushinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili.
Simba iliyocheza mechi nane, inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 18, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 17, iliyocheza mechi saba.

MILOVAN: IMENISIKITISHA, LAKINI NDIYO SOKA, TUNAGANGA YAJAYO

Simba na Kagera jana

PROFESA Milovan Cirkovick, amesema sare mbili mfululizo ambazo timu yake imezipata katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni kweli zimemsononesha, lakini hayo ni mambo ya kawaida katika soka.
Akizungumza baada ya sare ya jana dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam alisema matokeo hayo yamemsikitisha kwa ujumla na hana jinsi zaidi ya kukubali kwa kuwa hiyo ndiyo soka.
Alipotoka 0-0 na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga alisema ni kwa sababu ya Uwanja mbaya na kuwakosa nyota wake kadhaa, wakiwemo Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa, lakini jana alikuwa katika Uwanja mzuri na alikuwa na nyiota wake hao pia.
“Ni soka, katika soka yanatokea mambo haya, sasa najipanga kwa ajili ya mchezo ujao, ili tusiendelee na matokeo haya,”alisema Milovan, ambaye Jumapili anarudi kwenye Uwanja mbaya, Mkwakwani kukipiga na JKG Mgambo katika mfululizo wa ligi hiyo.
Simba jana ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Ngassa tangu ajiunge na Simba katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja, akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.
Katika mechi nyingine, Mgambo imeshinda mechi ya tatu mfululizo, baada ya kuifunga Toto African 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. JKT Ruvu imezinduka baada ya kuifunga Polisi Morogoro 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na JKT Oljoro imetoka 0-0 na African Lyon.
Simba SC; Juma Kaseja (Nahodha), Nassor Masoud ‘Chollo’/Uhuru Suleiman, Amir Maftah, Paschal Ochieng, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi/Jonas Mkude, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa.
Kagera Sugar; Andrew Ntala, Salum Kanoni, Martin Muganyizi, Amandus Nesta (Nahodha), Benjamin Effe/Themi Felix, Malegesi Mwangwa, Daudi Jumanne/Kamana Salum, George Kavilla, Shijja Mkinna, Enyinna Darlington na Wilfred Ammeh/Paul Nwai.
Katika mchezo wa awali, Simba B iliifunga Moro United mabao 3-0 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   
Mabao ya Simba B inayofundishwa na Suleiman Matola, akisaidiwa na Amri Said ‘Stam’ yalipatikana yote kipindi cha pili, wafungaji Ramadhan Salum dakika ya 65 na 70 na Miraj Athumani dakika ya 85.  Moro United inajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza, inayotarajiwa kuanza Oktoba 24, mwaka huu.

KIBADENI AFICHUA SIRI YA KUWAKAMATIA MBAVUNI SIMBA

Kibadeni

Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA wa Kagera Sugar, Abdallah Athumani Seif ‘Kibadeni’ amesema kwamba alijua ataifunga Simba jana, lakini bahati mbaya ikawa sare na ameridhika na matokeo hayo pia kwa ilikuwa mechi ya ugenini.
Kibadeni alisema kwamba katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kilichompa matumaini ya kuifunga Simba ni kwa sababu anamjua vizuri kocha wa timu hiyo, Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick kwa kuwa alifanya naye kazi.
“Mimi nilijua tu nitawapa tabu Simba, kwa sababu Milovan ninamjua, nimefanya naye kazi mimi Simba, ufundishaji wake naujua,”alisema Kibadeni.    
Kagera jana ilitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2 na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Ngassa tangu ajiunge na Simba katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja, akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.
Katika mechi nyingine, Mgambo imeshinda mechi ya tatu mfululizo, baada ya kuifunga Toto African 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. JKT Ruvu imezinduka baada ya kuifunga Polisi Morogoro 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na JKT Oljoro imetoka 0-0 na African Lyon.
Simba SC; Juma Kaseja (Nahodha), Nassor Masoud ‘Chollo’/Uhuru Suleiman, Amir Maftah, Paschal Ochieng, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi/Jonas Mkude, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa.
Kagera Sugar; Andrew Ntala, Salum Kanoni, Martin Muganyizi, Amandus Nesta (Nahodha), Benjamin Effe/Themi Felix, Malegesi Mwangwa, Daudi Jumanne/Kamana Salum, George Kavilla, Shijja Mkinna, Enyinna Darlington na Wilfred Ammeh/Paul Nwai.
Katika mchezo wa awali, Simba B iliifunga Moro United mabao 3-0 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   
Mabao ya Simba B inayofundishwa na Suleiman Matola, akisaidiwa na Amri Said ‘Stam’ yalipatikana yote kipindi cha pili, wafungaji Ramadhan Salum dakika ya 65 na 70 na Miraj Athumani dakika ya 85.  Moro United inajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza, inayotarajiwa kuanza Oktoba 24, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment