Tuesday, December 25, 2012

UBUTU PENATI: HODGSON ATAKA SARE KIRAFIKI ZIAMULIWE NA MATUTA!

 

>>ENGLAND IMESHINDA PENATI MARA MOJA TU KATI YA 6!!
ENGLAND_IN_WEMBLEYMeneja wa England Roy Hodgson amependekeza Mechi za Kimataifa za Kirafiki ambazo zitamalizika kwa Sare Mshindi wake apatikane kwa Mikwaju Mitano ya Penati hiyo ikiwa njia mojawapo kuisaidia Timu yake ambayo ina rekodi mbovu kwenye Penati katika Mashindano makubwa.
England imeshinda mara moja tu kati ya Mashindano 6 makubwa ambayo walilazimika kupata Mshindi kwa Mikwaju ya Penati kufuatia Sare katika muda wa kawaida rekodi mbovu ambayo ilianzia Mwaka 1990 walipofungwa kwa Penati na Germany kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia.
Pendekezo la Hodgson ni kuwa Wachezaji watakuwa kwenye Presha kubwa kwa vile wapo mbele ya umati mkubwa wa Mashabiki mwishoni mwa Mechi tofauti na wanavyofanya mazoezini na hilo litawapa uzoefu mzuri kuzikabili kwenye Mashindano makubwa.
Amesema: “Labda kwenye Mechi za Kirafiki, ikiwa Mechi itamalizika kwa Sare, Timu zikubaliana Mshindi apatikane kwa Penati!”
+++++++++++++++++++++++
ASILIMIA YA USHINDI KWENYE MIKWAJU YA PENATI:
-Argentina 73%
-Germany 71%
-Brazil 64%
-France 50%
-Sweden 50%
-Uruguay 50%
-Italy 33%
-Holland 20%
-England 17%

"Si wazo baya, litaleta ushindani mbele ya Mashabiki tofauti na kuzipiga mazoezini Siku hadi Siku huku wakicheka!."
Hodgson, akijua fika Rekodi mbovu ya Penati kwa England, inawafanya Wachezaji wao wawe kwenye woga ikifika hatua ya Penati kwenye Mechi na hilo huwazidishia Presha inayowafanya wazikose kirahisi.
Mara pekee ambayo England walishinda Mikwaju ya Penati ni kwenye Mashindano ya EURO 1996 walipoitoa Spain kwenye Robo Fainali lakini Nusu Fainali ya Mashindano hayo hayo walitolewa kwa Penati na Germany.
Mechi walizotolewa kwa Penati ni zile za Miaka ya 1990 na 1996 mikononi mwa Germany, mara mbili kubwagwa na Portugal, kwenye EURO 2004 na Kombe la Dunia Mwaka 2006, na EURO 2012 kutolewa na Italy kwenye Robo Fainali.

No comments:

Post a Comment