Thursday, December 20, 2012

KUELEKEA MZUNGUKO W APILI WA FDL RHINO RANGERS WAENDELEA KUJIIMARISHA KIUCHUMI

 

TFF_LOGO12

Timu ya jeshi ya mkoani tabora RHINO RANGERS imeendelea kujiimarisha kiuchumi kuelekea mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza FDL baada ya jana wadau wa mpira wa miguu wa mkoa wa tabora kukutana na kujadili mambo mbali mbali  na mkuu wa mkoa wa tabora   

Wadau waliohudhuria hiyo jana katika ukumbi wa isike mwanakiyungi kwa mkuu wa mkoa waliamua kuchangia kila mmoja kwa moyo wake pesa za saidia rhino ishinde  na zilipatikana shilingi laki nane ikiwemo pamoja na jezi za sh.millioni tano  ,jezi alizotoa mbunge wa tabora mjini na mwenyekiti wa simba ALHAJ ISMAIL ADENI RAGGE .

Wakati huo Wadau hao walijadili mambo mengi kuhusiana na timu ya RHINO RANGERS ili iweze kutinga ligi kuu ya vodacom VPL mwaka wa 2013.baadhi ya mambo waliyojadili ni pamoja na kuiwezesha timu ya rhino rangers kiuchumi ili iweze kumaliza mzunguko wa pili ikiwa inaongoza ligi daraja la kwanza katika kundi c.

RHINO RANGERS kwa sasa bado wanaongoza ligi daraja la kwanza FDL kwa pointi 17 wakiwa wamecheza michezo saba wakifuatiwa na JKT kanembwa ya kigoma kw apointi 16 na sasa  wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mzunguko huo w apili na katika mahitaji yao wnahitaji shilingi millioni hamsini na moja ili waweze

  Baadhi ya vitu walivyopatiwa jana ni pamoja na

--jezi zenye thamani ya shilingi millioni tano

--mchango wa wadau wapenda soka wa mpira wa miguu mkoa wa tabora wa shilingi laki nane

--gunia moja la karanga,kilo 100 za mchele,lita ishirini za mafuta ya kupikia,dazon 20 za maji ya kunywa,gunia moja la maharage nk.

 

MWAIKIMBA ATAKA KUMSAIDIA USHINDI KIM POULSEN STARS

Mwaikimba DRC

MSHAMBULIAJI mrefu, Gaudence Exavery Mwaikimba anayeng’ara kwenye michuano ya Kombe la Hisani hapa DRC, amesema kwamba bado ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu yake ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, lakini hawezi kuingilia maamuzi ya kocha Kim Poulsen.
Akizungumza  mjini kishansa  jana, Mwaikimba alisema kwamba uwezo wake siku zote upo juu kwa sababu ana kipaji na anajituma mazoezini, lakini hajui Kim anamfikiria vipi.
“Tangu mimi nimeibuka katika soka ya nchi hii, hakuna kocha ambaye alikuja kufundisha timu ya taifa akaacha kuniita kwenye kikosi, nadhani hata huyu Kim bado hajaniona tu, lakini mwenzake Jan Borge Poulsen aliniita,”alisema.
Mwaikimba alisema hawezi kulazimishwa kuitwa timu ya taifa kwa sababu ile ni timu ya Watanzania wote na Tanzania ina wachezaji wengi, ila roho itaendelea kumuuma kila timu itakapokuwa ikifanya vibaya wakati yeye ana uwezo wa kuisaidia.
“Ni kweli Tanzania ina washambuliaji wengi, lakini mimi ni wa kipekee, kama ninakuwa kwenye timu na kocha akanitumia vizuri, lazima nitakuwa tishio. Sema tu tatizo makocha wengi wa hapa hawajiamini na wanashindwa kufanya kazi zao vizuri,”alisema.
“Angalia Stewart (Hall, kocha wa Azam) huyu hapa, ndiye kanisajili hapa Azam na hadi kesho ananitumia na ananielekeza vizuri. Yaani mimi nauona umuhimu wangu kwake, inakuwa rahisi mtu kufanya kazi,”alisema.   
Katika mechi tatu za mashindano ya Kombe la Hisani, Mwaikimba amefunga mabao mawili hadi sasa.
Mwaikimba alikuwa mchezaji wa timu ya taifa kuanzia mwaka 2006 hadi 2010, ingawa wakati fulani mwaka 2009 aliwahi kutemwa na kocha Mbrazil, Marcio Maximo baada ya kiwango chake kushuka.
Na kushuka kwa kiwango chake kulichangiwa na migogoro na kocha wa klabu yake ya zamani, Profesa Dusan Savo Kondic raia wa Serbia, kiasi cha kufikia kuhama timu.   

AZAM YAPIGISHWA KWATA DRC

Benchi la Ufundi la Azam, kutoka kulia Daktari Mjerumani, Paulo Gomez, Kocha wa Makipa Mzalendo Iddi Abubakar, Kocha Msaidizi Muingereza Kali Ongala na Kocha Mkuu, Mungereza pia, Stewart Hall 

SHIRIKISHO la Soka Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC), limeigeuzia kibao Azam FC na sasa linaitaka icheze mechi moja zaidi ili kuwania Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Hisani inayoendelea hapa.
Hatua hiyo, inafuatia timu ya Diables Noirs ya Kongo Brazzaville kutofika kwenye mashindano haya na kufanya Kundi A libaki na timu tatu sawa na B.
Kwa mantiki hiyo, Azam kesho itashuka tena dimbani kumenyana na FC MK ya hapa mchezo ambao itatakiwa lazima kushinda ili kurudi Nusu Fainali.   
Kabla ya mabadiliko haya, Azam jana ilifanikiwa kuingia Nusu Fainali baada ya kuilaza Real de Kinshasa kwenye Uwanja wa Martyrs.
Shukrani kwao, washambuliaji Gaudence Mwaikimba na Seif Abdallah waliofunga mabao hayo, moja kila kipindi.
Ikiongezewa nguvu na nyota wake watatu, Kipre Tchetche, Kipre Balou raia wa Ivory Coast na Mkenya, Joackins Atudo waliochelewa mechi mbili za awali, Azam leo ilitawala mchezo na kama si rafu za wapinzani wao, ingevuna ushindi mtamu.
Hadi mapumziko, tayari Azam walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na Mwaikimba dakika ya 21, ambaye aliunganisha pasi nzuri ya Kipre kutoka wingi ya kushoto.
Hilo linakuwa bao la pili kwa Mwaikimba, mshambuliaji wa zamani wa Kahama United, Ashanti United, Yanga, Prisons na Kagera Sugar katika mechi tatu za mashindano haya alizocheza, awali alifunga katika sare ya 1-1 na Dragons.
Kipre Tchetche alilazimika kutoka nje ya Uwanja dakika ya 43 kutokana na rafu za wachezaji wa Real, nafasi yake ikichukuliwa na Samih Hajji Nuhu.
Real walikuwa wakipiga kiatu haswa na kiungo Waziri Salum aliungana na Kipre Tchetche kuuacha Uwanja kabla ya filimbi ya kuugawa mchezo, ingawa nafasi yake ilichukuliwa na Uhuru Suleiman dakika ya kwanza ya kipindi cha pili.
Awali ya hapo, refa Madila Achille alimtoa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 43 beki Muipalayi Igongo kwa kumchezea rafu mbaya Gaudence Mwaikimba, ambayo chupuchupu naye imtoe nje, kiasi  cha kulazimika kumalizia mechi akichechemea.
Kipindi cha pili, Azam waliendelea kuwafundisha soka Real na katika dakika ya 73, kazi nzuri ya Mwaikimba ilisaidia kupatikana bao la pili. Mpira mrefu uliopigwa na kipa Mwadini Ally, Mwaikimba aliumiliki vema, akatoa pasi pembeni kushoto kwa Hajji Nuhu ambaye aliingia ndani kidogo na kukata krosi maridadi iliyounganishwa kimiani na Seif.
Humphrey Mieno alikuwa mwathirika mwingine wa rafu za Real, baada ya kulazimika kutoka nje dakika ya 77, akimpisha Abdi Kassim ‘Babbi’.
Azam walionekana kuridhika baada ya kuwa wanaongoza mabao 2-0 na wakafanya uzembe uliowapa bao la kufutia machozi Real, lililofungwa na Bisole Panzu dakika ya 78.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall aliwapongeza vijana wake, lakini akasema anakabiliwa na wakati mgumu katika hatua inayofuata kutokana na wachezaji wake wanne kuumia leo.
Kocha wa Real, Sandra Makombele aliwasifu Azam ni timu nzuri na akasema anakubali matokeo, ingawa aliwapiga kijembe. “Wachezaji wangu wana mazoezi mengi, Azam hawana mazeozi, wakiguswa kidogo wanaumia, hakukuwa na rafu, ule ni mchezo wa nguvu kama Ulaya, kocha wao inabidi awape mazoezi mengi wawe wagumu,”alisema mwanamama huyo.
Katika mechi zake mbili za awali za Kundi B, Azam ilitoka 1-1 na Dragons na ikafungwa 2-0 na Shark FC.
Azam ilicheza mechi zote mbili bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivory Coast, kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Watano hao, waliwasili mjini Kinshasa juzi na beki Joackins Atudo naye aliwasili jana na wote walishiriiki mchezo wa jana kikamilifu.
Nusu Fainali zitachezwa Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu. 

 

AZAM NA MTIBWA NUSU FAINALI KOMBE LA UHAI


TIMU ya Mtibwa Sugar imekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) kuzamisha African Lyon mabao 3-1.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam,  hadi mapumziko Mtibwa Sugar ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 22 na Hillary Kasela. Hassan Kabunda aliisawazishia African Lyon katika dakika ya 53.
Mabao mengine ya washindi yalifungwa na Godfrey Mohamed dakika ya 64 na Juma Lazio akapachika la mwisho dakika ya 87. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar sasa itacheza mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Azam ambayo nayo leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) iliilaza JKT Ruvu bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Chamazi. Bao la Azam lilifungwa dakika ya 46 na Mudathiri Yahya.
Mechi hiyo ya kwanza ya nusu fainali itachezwa Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Nusu fainali ya pili nayo itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10 kamili jioni.
Robo fainali ya tatu kati ya Oljoro JKT na Simba, na robo fainali ya nne zinachezwa leo saa 10 kamili jioni (Desemba 19 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam

BRANGSTS AUGUA ASHINDWA KUSIMAMIA MAZOEZI YANGA


KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts, yupo hoi baada ya jana kushindwa kutokea katika mazoezi huku klabu hiyo ikibebeshwa mzigo wa kuwatema wachezaji ambao hawatakuwemo katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama Dar es Salaam, imeelezwa Brandts anaumwa malaria na kusababisha kushindwa kuendelea na programu ya kuwanoa wachezaji wa timu hiyo.
Daktari wa timu hiyo, Juma Sufiani alithibitisha, Brandts kushindwa kuendelea na majukumu yake kutokana na kuumwa ugonjwa huo.
Yanga ambayo inajiandaa kwenda kuweka kambi ya wiki moja Uturiki katika mazoezi ya jana yalisimamiwa na Kocha Msaidizi, Fred Minziro, ambayo yalifanyika kwa saa tatu.
Wakati huo huo, Uongozi wa klabu hiyo, umempa rungu Brandts kuhakikisha anawakata wachezaji ambao hawakuwamo katika kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema wameamua kurejesha suala hilo kwa Brandts kutokana na awali alipendekeza baadhi ya wachezaji wapelekwe mkopo ama waache katika usajili mdogo wa ligi hiyo.
Sanga alisema kwa kuwa Brandts alipendekeza majina ya wachezaji wa kuachwa kwa Kamati ya mashindano ya klabu hiyo, wamemtaka achague kutokana na wengine, bado wana mikataba na klabu hiyo.
Alisema wachezaji wengine hawatakiwi kuachwa kutokana na wana mikataba, kwani anatakiwa aangalie upya.
Sanga alisema usajili huo unatarajia kukamilika wiki hii.

TANZANIA YAPAA NAFASI NNE VIWANGO VYA UBORA FIFA

TANZANIA imepanda nafasi nne kutoka 134 hadi 130 kwenye orodha ya viwango bora vya soka vilivyotolewa jana na Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA) huku wakiwa nafasi ya 38 miongoni mwa nchi za Afrika
Mwezi uliopita, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Tanzania kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro, ilicheza mchezo moja wa kimataifa wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.
Taifa Stars ilicheza na Harambee Stars ya Kenya katika Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na beki wa kati Aggrey Moris.
Uganda ambao walifanikiwa kutetea ubingwa wa michuano ya Chalenji mwezi huu ikiwa ni ushindi wao wa 13, wanafunga mwaka wakiwa miongoni mwa nchi 100 bora.
Mabingwa hao wa CECAFA ambao wamepanda nafasi mbili wapo katika nafasi ya 84 ambapo Afrika wapo nafasi ya 22 wakifwatiwa na Sudan ambao wamepanda nafasi moja hadi 101.
Burundi ndiyo taifa lililofanya vyema ambapo imepanda nafasi 24 na kumaliza mwaka ikiwa nafasi ya 104 kimataifa na 27 Afrika huku wawakilishi pekee wa CECAFA michuano ya Kombe la Afrika mwezi ujao, Ethiopia ikishika nafasi ya 110 baada ya kushuka nafasi nane.
Kenya imeshuka nafasi nne na kumaliza mwaka ikiwa nafasi ya 134, huku Rwanda pia ikiwa nafasi ya 134 baada ya kushuka nafasi 12 ikifuatiwa na Somalia ambao imeshuka nafasi mbili na kushika nafasi ya 195. Eritrea ni ya 196 baada ya kushuka nafasi nne, Sudan Kusini ni ya 199 na Djibouti ipo nafasi ya 202.
Kimataifa Hispania ndiyo inaongoza kwa ubora duniani ikifuatiwa na Ujerumani na Argentina wakati nchi tatu za juu Afrika ni Ivory Coast, Algeria na Mali.

HARUNA MOSHI "BOBAN" AANZA MAZOEZI TENA NA SIMBA



KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban,’ leo ameanza mazoezi rasmi katika kikosi cha timu hiyo, kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Boban aliungana na wachezaji wenzake katika mazoezi yaliyofanyika Ufukwe wa Coco Beach, Dar es Salaam, yaliyosimamiwa na Meneja wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Kiungo huyo alisimamishwa na Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo, kutokana na madai ya utovu wa nidhamu, baada ya mchezo wao dhidi ya Mgambo Shooting, uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Boban amerejea kimya kimya kwenye kikosi hicho, baada ya suala lake kumalizwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage.
Hata hivyo, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga, alipoulizwa leo, kuhusu kurejea kwa kiungo huyo, alisema hajui lolote, ingawa suala hilo lilikuwa chini ya mwenyekiti wake.
Boban alisimamishwa siku 21 na kutakiwa kuandika barua ya kujieleza kabla ya kuchukuliwa hatua nyingine

YANGA YAMTEMA KOCHA WA MAKIPA, MWENYEWE AWASHUKURU WANAYANGA KWA USHIRIKIANO WALIOMPA


YANGA imemtema Kocha wa makipa, Mfaume Athumani na kumrejesha Mkenya Razak Siwa, baada ya kumaliza mkataba wa kuifundisha timu hiyo.
Siwa aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, anatarajia kusaini mkataba mpya baada ya Yanga kurejea kutoka Uturuki.
Akizungumza leo, Mfaume alisema kuwa hataambana na kikosi cha timu hiyo kutokana na kumaliza mkataba wake na klabu hiyo ambayo alishawahi kuitumikia katika miaka ya nyuma.
Alisema kuwa, mkataba wake na Yanga umefikia ukingoni, hivyo ameamua kupumzika kwa muda katika masuala ya soka.
 “Nashukuru Wanayanga kwa ujumla wao kwa sababu kwa muda wote ambao nimekuwepo hapa kama mchezaji, niliporejea kama kocha wa makipa wamenipa ushirikiano wa hali ya juu,” alisema Mfaume.
“Kwa sababu hiyo sina sababu ya kutofurahi kutokana na mafanikio ambayo niliyapata nikiwa na Yanga, naamini ni mengi licha ya changamoto nyingi nilizokutana nazo kama kocha,” alisisitiza Kocha huyo.
Alisema kuwa jambo ambalo anaweza kujivunia ni kumfanya kipa Ally Mustapha ‘Barthez’ kuwa namba moja kwenye kikosi cha Yanga lakini zaidi ni kuunda nguvu kazi ya makipa bora Tanzania kwa sasa.
“Nasema hivyo kwa sababu ukiangalia Berko ambaye ameondoka, amekuwa ni moja ya tunda la kujivunia kwa Wanayanga kwa muda mrefu, pia alikuwepo Shaban Kado pamoja na Said Mohamed ambao wote naamini wanaweza kuwa makipa wa timu za taifa,” alisema Mfaume.
Hadi mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizika, Yanga imefungwa mabao 12 katika mechi 13 ilizocheza na kujikuta ikipata pointi 29,  jambo lilionyesha kuwa Mfaume alifanya kazi kubwa katika kuwanoa makipa hao.

MBWANA SAMATTA,THOMAS ULIMWENGU NA JOHN BOCCO KUIKOSA ZAMBIA


NYOTA watatu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars,' wanatarajia kukosa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Zambia, utakaochezwa siku ya jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni washambuliaji John Bocco, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya DR Congo, ambao ni wagonjwa.
Akizungumza leo Daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa alisema Bocco hataweza kucheza kutokana na kuumia goti katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Desemba 8, mwaka huu Kampala Uganda.
Mwankemwa alisema, pamoja na kukosa mchezo huo, ataendelea kuwepo kambini kwani aliumia akiwa kwenye timu hiyo.
Akifafanua kuhusu Samatta na Ulimwengu, alisema wao waliumia wakiwa na timu yao ya TP Mazembe na wamekuja na vyeti vinavyoonyesha kuwa wagonjwa.
Mwankemwa alisema, cheti cha Ulimwengu kinaonyesha aliumia goti la mguu wa kulia na Samatta yeye kinaonyesha aliumia bega.
Wachezaji hao ambao waliwasili nchini na kuendelea kukaa nyumbani, juzi walipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyiwa kipimo cha MRI ili wapate tiba sahihi.
Alisema wanasubiri vipimo vya daktari kutoka Muhimbili ila  kweli wachezaji hao ni majeruhi na wataendelea kuwatibu ili waweze kupona.
"Tunawatibu ili tutakapoingia kambini Januari 6, mwakani kujiandaa na  mashindano ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), wawe wamepona kabisa', alisema Mwankemwa.
Wapinzani wa Stars walitua leo jioni nchini kwa ajili ya mchezo huo, ambao utachezwa kuanzia saa 10 kwenye uwanja wa Taifa.

LINA MHANDO AREJEA TENA TWFA

Lina Kessy
MGOMBEA Lina Kessy leo ameweza kutetea nafasi yake ya Uenyekiti katika uchaguzi  wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) uliofanyika kwenye hoteli ya Midlands mjini Morogoro.
Akizungumza jijini Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema kuwa Lina amewashinda wenzake Isabela Kapera na Joan Minja katika uchaguzi huo kwa kukusanya kura 25 kati ya 50 zilizopigwa, huku Isabela akipata kura 13 na Joan 11.
Wambura alisema kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Rose Kissiwa aliweza kupita katika kinyanganyiro hicho kwa kujikusanyia kura 35  huku 13 zikisema hakuna na kura 2 zikiharibika.
Ofisa huyo alisema kuwa Amina Karuma ameshika nafasi ya Ukatibu mkuu na kumshinda mpinzani wake  Cecilia Mkafum baada ya kupata kura 35 huku mpinzani wake akipata kura 15.
Mwandishi mwaandamizi Zena Chande ambaye alikuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo katika nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF aliweza kupata kura 24 huku kura 22 zikimkataa na 4 zimeharibika.
Huku nafasi ya mjumbe wa kamati ya Utendaji wa chama hicho ikienda kwa Triphonia Temba baada ya kumshinda mpinzani wake Sophia Charles baada ya kukusanya kura 39 huku Sophia akipata kura 30

AKINA MORRIS, CANNAVARO KWENDA KAMATI YA NIDHAMU

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ikieleza kuwafungia wachezaji kadhaa Wazanzibari wanaochezea klabu mbalimbali za timu za Tanzania Bara na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Suala hilo limepelekwa kwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF kwa hatua zaidi, hivyo kwa sasa Shirikisho litasubiri uamuzi wa kamati hiyo. Baadhi ya wachezaji hao ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars, Aggrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassoro Masoud Cholo, Mcha Khamis, Seif Abdallah na Selemani Kassim Selembe
 

AZAM YATINGA NUSU FAINALI DRC

Wachezaji wa Azam wakipongezana kwa ushindi leo.
AZAM FC imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Hisani mjini hapa, baada ya kuilaza Real de Kinshasa kwenye Uwanja wa Martyrs, katika mchezo maalum wa kutafuta timu ya kutinga Nusu ya michuano hiyo inayoandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka DRC.
Shukrani kwao, washambuliaji Gaudence Mwaikimba na Seif Abdallah waliofunga mabao hayo, moja kila kipindi.
Ikiongezewa nguvu na nyota wake watatu, Kipre Tchetche, Kipre Balou raia wa Ivory Coast na Mkenya, Joackins Atudo waliochelewa mechi mbili za awali, Azam leo ilitawala mchezo na kama si rafu za wapinzani wao, ingevuna ushindi mtamu.
Hadi mapumziko, tayari Azam walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na Mwaikimba dakika ya 21, ambaye aliunganisha pasi nzuri ya Kipre kutoka wingi ya kushoto.
Hilo linakuwa bao la pili kwa Mwaikimba, mshambuliaji wa zamani wa Kahama United, Ashanti United, Yanga, Prisons na Kagera Sugar katika mechi tatu za mashindano haya alizocheza, awali alifunga katika sare ya 1-1 na Dragons.
Kipre Tchetche alilazimika kutoka nje ya Uwanja dakika ya 43 kutokana na rafu za wachezaji wa Real, nafasi yake ikichukuliwa na Samih Hajji Nuhu.
Real walikuwa wakipiga kiatu haswa na kiungo Waziri Salum aliungana na Kipre Tchetche kuuacha Uwanja kabla ya filimbi ya kuugawa mchezo, ingawa nafasi yake ilichukuliwa na Uhuru Suleiman dakika ya kwanza ya kipindi cha pili.
Awali ya hapo, refa Madila Achille alimtoa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 43 beki Muipalayi Igongo kwa kumchezea rafu mbaya Gaudence Mwaikimba, ambayo chupuchupu naye imtoe nje, kiasi  cha kulazimika kumalizia mechi akichechemea.
Kipindi cha pili, Azam waliendelea kuwafundisha soka Real na katika dakika ya 73, kazi nzuri ya Mwaikimba ilisaidia kupatikana bao la pili. Mpira mrefu uliopigwa na kipa Mwadini Ally, Mwaikimba aliumiliki vema, akatoa pasi pembeni kushoto kwa Hajji Nuhu ambaye aliingia ndani kidogo na kukata krosi maridadi iliyounganishwa kimiani na Seif.
Humphrey Mieno alikuwa mwathirika mwingine wa rafu za Real, baada ya kulazimika kutoka nje dakika ya 77, akimpisha Abdi Kassim ‘Babbi’.
Azam walionekana kuridhika baada ya kuwa wanaongoza mabao 2-0 na wakafanya uzembe uliowapa bao la kufutia machozi Real, lililofungwa na Bisole Panzu dakika ya 78.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall aliwapongeza vijana wake, lakini akasema anakabiliwa na wakati mgumu katika hatua inayofuata kutokana na wachezaji wake wanne kuumia leo.
Kocha wa Real, Sandra Makombele aliwasifu Azam ni timu nzuri na akasema anakubali matokeo, ingawa aliwapiga kijembe. “Wachezaji wangu wana mazoezi mengi, Azam hawana mazeozi, wakiguswa kidogo wanaumia, hakukuwa na rafu, ule ni mchezo wa nguvu kama Ulaya, kocha wao inabidi awape mazoezi mengi wawe wagumu,”alisema mwanamama huyo.
Katika mechi zake mbili za awali za Kundi B, Azam ilitoka 1-1 na Dragons na ikafungwa 2-0 na Shark FC.
Azam ilicheza mechi zote mbili bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivory Coast, kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Watano hao, waliwasili mjini Kinshasa jana na beki Joackins Atudo naye amewasili leo na wote wameshiriiki mchezo wa leo kikamilifu.
Nusu Fainali zitachezwa Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu. 
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum/Uhuru Suleiman dk46, Omar Mtaki/Joackins Atudo dk46, David Mwantika, Jabir Aziz, Kipre Balou/Malika Ndeule dk85, Seif Abdallah, Kipre Tchetche/Samih Hajji dk43, Humphrey Mieno/Abdi Kassim dk77 na Gaudence Mwaikimba. 
 

SUNZU HUYOOO READING


Stopilla Sunzu (kulia) akiwa na washkaji zake jijini Lusaka, juzi. 
BEKI nyota wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na timu ya taifa ya Zambia “Chipolopolo”,  Stopilla Sunzu amesema kuwa ameamua kwenda kuichezea klabu ya Reading inayoshiriki Ligi Kuu ya England na sio Arsenal  kwa sababu kocha Arsene Wenger amemueleza kuwa ni lazima afuatiliwe kwa muda mrefu zaidi kabla ya kupewa mkataba.Beki huyo mwenye miaka 23,  ambaye amepaa kwenda Ghana pamoja na kocha Herve Renard na Rainford Kalaba kuhudhuria hafla ya kesho ya utoaji wa tuzo za wanasoka bora wa mwaka za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), amekaririwa na vyombo vya habari vya Zambia akisema kwamba amepata mwaliko kutoka Reading na kwamba, safari yake ya kwenda England imeiva.
“Nitasafiri kwenda England baada ya mechi yetu dhidi ya Tanzania lakini sitakwenda Arsenal. Arsenal wanataka nijaribiwe kwanza,” alisema Sunzu kabla hajaondoka kwenda Accra, Ghana jana.” 
“Badala yake, nitakwenda Reading ambako nitasajiliwa tu na siyo kufanyiwa majaribio.

Mario Balotelli AKUBALI KULIPA FAINI

Mshambulijai wa Manchester city  Mario Balotelli amefuta kesi yake mahakani dhidi ya klabu yake ya city baada ya kukubali kulipa faini ya mshahara wa majuma mawili kama adhabu ya kinidhamu dhidi yake kutokana na Takwimu mbaya ya Nidhamu msimu uliopita .

 Kesi hiyo ilitakiwa kusikizwa leo lakini kutokana na mazungumzo yaliyofanyika jana usiku kati ya pande zote mbili , Taarifa zinasema kuwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 amefanya maamuzi hayo kama kumheshimu kocha mkuu wa klabu yake Roberto Mancini, na Mashabiki kwa ujmla ".

 "Mario ataendelea kuwemo katika mechi inayofuata dhidi ya Reading klabu hiyo" imesema
Mshambuliaji huyo aliipinga klabu yake kwa kumkata mshahara mara baada ya kukosa mechi 11 na za kimataifa  baada ya kukabiliwa na adhabu hiyo.

Mshambuliaji huyo alitarajiwa kwenda mahakani pamoja na Mwanasheria wake kutoka italia na mwakilishi kutoka chama cha wachezaji wa kulipwa huku City ilitarajiwa kuwakilishwa na wanasheria wa timu hiyo Mshahara wa wiki mbili ni adhabu sahihi kwa wachezaji wote wa kulipwa 

  City ilianza kumtuhumu mchezaji huyu Mara baada ya kupewa kadi nyekundu mechi dhidi ya arsenal mwezi April 2012  na alipewa kadi za njano Tisa na Nyekundu tatu katika msimu  mmoja .
 
 
 
MASHABIKI WA ZENIT ST PETERSBURG NI WABAYA NA WABAGUZI 

Mlinzi wa klabu ya Anzhi Makhachkala Christopher Samba. Amewatuhumu mashabiki wa klabu yake kwa kusema ni wabaya na wabaguzi na wanaishi katika karne nyingine kabisa na sio hii ya ishirini na moja , Mashabiki hao ambao hawataki kuona mchezaji mweusi na shoga wakizitumikia klabu za urusi ,Anasema "Sishwangazi sana , Kila mtu anajua kuwa  Mashabiki wa  Zenit sio wazuri  na ni wabaguzi . 

 "Wanaishi katika sayari nyingine Ni siku mbaya  katika soka ya Urusi aliongeza  : " katika wakati huu ambapo jamii tofauti katika nchi tofauti wanatengeneza timu . Kama hawawezi kukubaliana na hili basi kamwe hawataendelea ." 

 Zenit Ndio timu pekee iliyokuwa haina mchezaji mweusi mpaka pale aliposajiriwa Raia wa Brazil Hulk na kiungo wa Ubeligi   Axel Witsel. 

 Klabu iliwahi kupigwa faini ya Shirikisho  la soka la Urusi baada ya mashabiki kumrushia Ndizi mchezaji wa  Anzhi Makhachkala -na mlizni wa Kushoto wa klabu hiyo  Roberto Carlos kabla ya mechi dhidi ya Lokomotiv Moscow   March 2011. 

 Wachezaji weusi hupigiwa  miruzi ya kama ishara ya kumwita nyani  
  Samba amesema kuwa Tabia hiyo inaweza kuathiri maandalizi ya ya Kombe la Dunia mwaka 2018 kwani itakuwa ngumu kucheza hasa kwa timu kutoka afrika na za ulaya ambazo zinawachezaji weusi 

Benzema TUPO TAYARI KUPIGANA  MACHO YAPASUKE 

Mshabuliaji wa Real Madrid  Karim Benzema amewaonya Viongozi wa La liga   Barcelona kuwa timu yao haitaachana na mbio za ubingwa japokuwa wapo nyuma  kwa alama kumi na tatu baada ya kwenda sare na Espanyol  huku vijana wa  Tito Vilanova' wakiiibamiza  Timu inayoshika nafasi ya tatu  Atletico Madrid 4-1 katika Dimba la Nou Camp.

Kocha wa Madrid  Jose Mourinho alinukuliwa akisema kuwa  kwa vitendo haiwezekani kwa sasa kutetea ubingwa wa la liga huku Barca wakiwa wamepoteza alama moja tu Ni vigumu kwa Mabingwa Mara tisa wa ulaya kutetea taji hili tena na kupigana alama kumi na tatu hii ni tofauti kubwa sana  

,Kama hatuta Endelea kufungwa hatuwezi kukubali kuwaachia   Barça,wachukue kila hisi namna hiyo  . Benzema ALILIAMBIA Jarida la Kifaransa 
 

GERMAN CUP: Goetze aipigia Dortmund Hetitriki, yatinga Robo Fainali!

BORUSSIA_DORTMUND_JUKWAAMario Goetze amefunga Hetitriki na kuifanya Borussia Dortmund, ambao ndio Mabingwa watetezi, watinge Robo Fainali ya German Cup baada ya kuifunga Hannover Bao 5-1 Jumatano Usiku.
Mario-Goetze
Wolfsburg nao wametinga Robo Fainali baada ya kuifunga Bayer Leverkusen 2-1 na VfB Stuttgart iliifunga Timu ya Daraja la Pili Cologne 2-1.
Mabingwa wa Bundesliga Borussia Dortmund waliitawala Mechi hii na Hanover na Bao pekee la Hanover lilifungwa na Mame Biram Diouf, Mchezaji wa zamani wa Manchester United, katika Dakika ya 9 baada ya krosi ya Szabolcs Huszti
Juzi Jumanne, Bayern Munich, Mainz, Freiburg na Timu ya Daraja la Tatu Kickers Offenbach nao waliingia Robo Fainali.
GERMAN CUP
MATOKEO:
Jumanne Desemba 18
Schalke 1 Mainz 2
Karlsruher 0 Freiburg
Kickers Offenbach 2 Fortuna Dusseldorf 0
Augsburg 0 Bayern Munich 2
Jumatano Desemba 19
Bochum 3 1860 Munich 0
Wolfsburg 2 Bayer Leverkusen 1
Borussia Dortmund 5 Hannover 1
Stuttgart 2 FC Cologne 1

Wilshere, Vijana 4 wengine, wasaini Mikataba mipya!

>>NI YA MUDA MREFU, WENGINE NI Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Gibbs, Jenkinson!!
>>BPL: ARSENAL v WEST HAM DESEMBA26 YAAHIRISHWA!!
WALCOTT_WILSHERE_OXKlabu ya Arsenal imetangaza kuwa imefanikiwa kuwafunga Wachezaji wao watano Chipukizi wenye asili ya Kiingereza kwa muda mrefu na pia kutangaza kuwa Mechi yao ya Ligi Kuu England iliyopangwa kuchezwa Desemba 26 dhidi ya West Ham imeahirishwa kwa sababu ya Mgomo wa Wafanyakazi wa Treni za chini kwa Chini, London Underground, Siku hiyo.
Habari njema kwa Arsenal ni kule kuweza kuwafunga Wachezaji wao Nyota Chipukizi kwa Mikataba ya muda mrefu hasa baada ya hivi karibuni kuwapoteza Mastaa kama vile Robin van Persie alieenda Manchester United na Cesc Fabregas aliekwenda Barcelona.
Wote watano waliopata Mikata mipya ni Vijana ambapo Wishere ana Miaka 20, Gibbs, 23, Ramsey, 21, Oxlade-Chamberlain, 19, na Jenkinson, 20.
Wilshere na Gibbs wameanzia Arsenal tangu watoto na Ramsey alijiunga Mwaka 2008 wakati Oxlade-Chamberlain, alitokea Southampton Mwaka 2011 na Jenkinson alitokea Charlton.
WAKATI HUO HUO, Klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa Mechi yao ya Ligi hapo Desemba 26 na West Ham imeahirishwa baada ya kuthibitika kutakuwa na mgomo Siku hiyo hiyo unaohusisha Wafanyakazi wa Treni za chini kwa chini za Jijini London, London Underground.
++++++++++++++++++++++++++++
PATASHIKA ARSENAL LIGI KUU ENGLAND:
DESEMBA 2012:
Desemba 17: Reading v Arsenal
Desemba 22: Wigan v Arsenal
Desemba 26: Arsenal v West Ham [IMEAHIRISHWA]
Desemba 29: Arsenal v Newcastle
JANUARI 2013:
Januari 1: Southamton v Arsenal
Januari 6: Swansea v Arsenal
Januari 13: Arsenal v Man City
Januari 20: Chelsea v Arsenal
Januari 30: Arsenal v Liverpool
++++++++++++++++++++++++++++
Mwaka jana, Mechi ya Arsenal ya Desemba 26 pia iliahirishwa kwa sababu hii hii.
Mechi hii sasa itachezwa Jumatano Januari 23 au Jumamosi Januari 26.
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 22 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Wigan v Arsenal
[SAA 12 Jioni]
Man City v Reading
Newcastle v QPR
Southampton v Sunderland
Tottenham v Stoke
West Brom v Norwich
West Ham v Everton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Liverpool v Fulham
Jumapili 23 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea v Man United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Aston Villa

MESSI ANASTAHILI BALLON D'OR - IBRAHIMOVIC.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSV, Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa Lionel Messi anastahili tuzo ya Ballon d’Or pamoja na kwamba mshambuliaji huyo wa Barcelona ameshashinda tuzo hiyo mara tatu mfululizo. Akihojiwa na gazeti moja nchini Ufaransa Ibrahimovic alimsifu Messi na kumfananisha kama mchezaji wa kwenye michezo ya luninga inayojulikana kama PlayStation na kudai kuwa anayeponda uwezo wa mchezaji huyo hajui mchezo wa soka. Ibrahimovic pia alisifu uwezo kiungo nyota wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuwa ni wa kipekee kwani pindi anapoingia uwanjani wachezaji wenzake wote hubadilika na kucheza vyema na kupelekea timu yao kupata matokeo mazuri. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alifika mbali na kudai kuwa hadhani kama kutatokea mchezaji wa aina ya Zidane huko mbele katika ulimwengu wa soka. 
 

CAPITAL ONE CUP: DROO NUSU FAINALI YAFANYIKA!

CAPITAL_ONE_CUP-BEST>>VILLA v BRADFORD & CHELSEA v SWANSEA!!
Baada ya kuitwanga Arsenal, Timu ya Daraja la chini, Ligi 2, Bradford City imepangiwa kucheza na Aston Villa kwenye Nusu Fainali na Chelsea watakutana na Swansea City.
Nusu Fainali za Mashindano haya huchezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na Mechi za kwanza zitachezwa Januari 7 na marudiano Wiki mbili baadae.
+++++++++++++++++++++
DONDOO za LIGI CUP:
-Aston Villa wameshinda Kombe hili mara 5 mara ya mwisho ni 1996
-Chelsea wameshinda mara 5 ikiwa ni pamoja na 2005 na 2007
-Bradford na Swansea hawajawahi kutwaa Kombe hili.
+++++++++++++++++++++
LEEDS UNITED 1 CHELSEA 5
Chelsea wametinga Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP baada ya kutoka nyuma kwa Goli moa Uwanjani Elland Road na kushinda Bao 5-1 katika Mechi ya Robo Fainali iliyokuwa imebakia kuchezwa kwa vile Chelsea walikuwa huko Japan kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani.
+++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Leeds United 1
-Becchio Dakika ya 37.
Chelsea 5
-Mata Dakika ya 47
-Ivanovic 64
-Moses 66
-Hazard 81
-Torres 84
+++++++++++++++++++++
Leeds United ndio walitangulia kupata Bao Kipindi cha Kwanza lakini Kipindi cha Pili Chelsea walicharuka na kupiga bao 5.
VIKOSI:
LEEDS: Ashdown, Byram, Lees, Pearce, Peltier, Tonge, Green, Brown, Thomas, Becchio, Diouf.
Akiba: Kenny, Varney, White, Norris, Gray, Somma, McCormack.
CHELSEA: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Bertrand, Lampard, Oscar, Moses, Mata, Marin, Torres.
Akiba: Turnbull, Cole, Hazard, Ferreira, Piazon, Saville, Ake.
Refa: Andre Marriner,
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP-Robo Fainali:
MATOKEO:
Jumanne Desemba 11
Norwich 1 Aston Villa 4
Bradford 1 Arsenal 1 [Bradford yasonga Penati 3-2]
Jumatano Desemba 12
Swansea 1 Middlesbrough 0
Jumatano Desemba 19
Leeds United 1 Chelsea 1
+++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU za CAPITAL ONE CUP:
-KABLA LILIKUWA ni Carling Cup na Bingwa Mtetezi alikuwa ni Liverpool.
-Linaitwa CAPITAL ONE CUP kwa sababu Mdhamini wake ni Kampuni ya masuala ya Fedha, Capital One.
-Linashirikisha Timu za Ligi za juu England 92 kwa mtindo wa Mtoano [Timu 20 toka Ligi Kuu na 24 kila moja kutoka Madaraja ya Npower, Ligi 1 na 2.
-FAINALI itafanyika Uwanja wa Wembley Tarehe 24 Februari 2013
-Bingwa wa michuano hii hucheza EUROPA LIGI Msimu unaofuata kuanzia Raundi ya Tatu ya Mtoano.
 

No comments:

Post a Comment