Monday, October 8, 2012

KOMBE la DUNIA 2014: FIFA yaipora Sudan Pointi Mechi iliyoifunga Zambia!

Jumanne, 09 Oktoba 2012 08:55
   
>>FA Sudan Faini Dola 6,340!
BRAZIL_2014_BESTFIFA imeinyang’anya Sudan ushindi wake wa Bao 2-0 walioifunga Zambia kwenye Mechi ya Kundi D ya Mechi za Mchujo kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil baada ya kumchezesha Mchezaji mmoja ambae hakustahili kucheza Mechi hiyo.


Kamati ya Nidhamu ya FIFA imeamua kuwa Mchezaji Saif Ali hakutakiwa kucheza Mechi hiyo waliyoshinda Sudan Mjini Khartoum hapo Juni 2 Mwaka huu baada ya kuwa na Kadi za Njano alizopata katika Mechi za nyuma ikiwemo ile ambayo Zambia waliichapa Sudan kwenye Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2012, iliyochezwa huko Gabon na Equatorial Guinea.


FIFA imeamua sasa kuipa Pointi 3 Zambia na goli 3-0 na pia kukitwanga Faini ya Dola 6,340 Chama cha Soka cha Sudan.


Uamuzi huu wa FIFA unaifanya Zambia sasa iongoze Kundi D ikiwa na Pointi 6 kwa Mechi mbili ikifuatiwa na Ghana wenye Pointi 3, Sudan nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 1 na Lesotho wako mkiani wakiwa na Pointi 1.


MSIMAMO KUNDI D:
1 Zambia Mechi 2 Pointi 6
2 Ghana Mechi 2 Pointi 3
3 Sudan Mechi 2 Pointi 1
4 Lesotho Mechi 2 Pointi 1


RATIBA/MATOKEO:
01/06/12: Ghana 7-0 Lesotho
02/06/12: Sudan 2-0 Zambia [Matokeo yamefutwa sasa ni Sudan 0 Zambia 3]
12/06/12: Zambia 1-0 Ghana
10/06/12: Lesotho 0 Sudan 0
22-26/03/13: Ghana v Sudan; Lesotho v Zambia
07-11/06/13: Sudan v Ghana; Zambia v Lesotho
14-18/06/13: Lesotho v Ghana; Zambia v Sudan
06-10/09/13: Ghana v Zambia; Sudan v Lesotho

VPL: Yanga yafa Kagera!

Jumatatu, 08 Oktoba 2012 20:11
   
>>KIPIGO CHAIPOROMOSHA HADI NAFASI YA 8!!
MATOKEO:
Jumatatu Oktoba 8
Kagera Sugar 1 Yanga 0 (Uwanja wa Kaitaba, Bukoba)
++++++++++++++++++++++++++
VPL_LOGOYanga leo huko Uwanja wa Kaitaba, Bukoba walipigwa bao 1-0 na Kagera Sugar na kuporomoshwa hadi nafasi ya 8 katika Mechi pekee ya Ligi Kuu Vodacom huku ushindi huo ukiupaisha Kagera Sugar hadi nafasi ya 3 kwa kufikisha Pointi 10 wakiwa nyuma ya Azam wenye Pointi 13 na vinara Simba wenye 16.

 Bao la ushindi kwa Kagera Sugar lilifungwa katika Dakika ya 68 na Themi Felix.

Mechi hii ya Kagera Sugar na Yanga ilikuwa ichezwe jana lakini kutokana na Uwanja wa Kaitaba kuwa na shughuli nyingine za kijamii ikaahirishwa hadi leo.


Mechi ifuatayo kwa Yanga ni huko Mwanza dhidi ya Toto Africans Siku ya Alhamisi Oktoba 11.


MSIMAMO:
1 Simba Mechi 6 Pointi 16
2 Azam FC Mechi 5 Pointi 13
3 Kagera Sugar Mechi 6 Pointi 10
4 Prisons Mechi 6 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 1]
5 Coastal Mechi 6 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 0]
6 JKT Oljoro Mechi 6 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 0]
7 Mtibwa Sugar Mechi 5 Pointi 8 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Yanga SC Mechi 6 Pointi 8 [Tofauti ya Magoli 1]
9 Toto African Mechi 6 Pointi 7 [Tofauti ya Magoli 0]
10 Ruvu Shooting Mechi 6 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -2]
11 African Lyon Mechi 6 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -5]
12 JKT Ruvu Mechi 6 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -7]
13 JKT Mgambo Mechi 6 Pointi 3
14 Polisi Moro Mechi 6 Pointi 2

FALCON, JAMHURI zajitoa Michuano ya CAF 2013!

Jumatatu, 08 Oktoba 2012 19:50
   
>>RIPOTI na Ally Mohammed, COCONUT FM 88.2, Zenji
Wawakilishi wa Zanzibar katika Michuano ya Kimataifa kwa Vilabu Barani Afrika kwa Mwaka 2013, Falcon na Jamhuri, wamejitoa katika michuano hiyo.


Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Visiwani Zanzibar, ZFA, Aman Ibrahim Makungu, ni kuwa Timu ya Super Falcon ambao ni Mabingwa watetezi katika Ligi Kuu ya Zanzibar, ambao walikuwa waiwakilishe Zanzibar katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Mwakani pamoja na Timu ya Jamhuri ambao ni Makamo Bingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar na ambao walikuwa waiwakilishe Zanzibar katika Kombe la Shirikisho hapo mwakani kwa pamoja wameamua kujitoa katika michuano hiyo.
Chanzo cha Timu hizo kujitoa inasemekana ni ukata wa fedha, ambapo kila timu ilihitaji Dola 30,000 kwa ajili ya maandalizi ya ushiriki wa michuano hiyo.


Kufuatia hatua hiyo ZFA, iko katika mazungumzo na baadhi ya Vilabu vya Ligi Kuu ili kuona kama kuna uwezekano wa kupata Timu zitakazochukua nafasi hizo.


Mwaka huu Zanzibar iliwakilishwa na timu ya Mafunzo katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, huku Jamhuri wakipata nafasi ya kushirki katika Kombe la Shirikisho.


Hata hivyo Timu zote zilishindwa kufanya vizuri baada ya kuondolewa katika hatua ya mwanzo katika michuano hiyo.

MECHI za KIMATAIFA: Kurindima kuanzia Ijumaa!!

Jumatatu, 08 Oktoba 2012 19:31
 
BRAZIL_2014_BEST>>ULAYA na kwingineko ni MCHUJO KOMBE la DUNIA 2014
>>AFRIKA ni kuwania Fainali AFCON 2013 huko Afrika Kusini!!
Ijumaa Oktoba 16, Mechi za Kimataifa zitaanza kuchezwa na Barani Ulaya, Marekani ya Kusini na kwingineko ni Mechi za Mchujo kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil lakini kwa Afrika, hapo Jumamosi na Jumapili, kutakuwa na Mechi za marudiano za Raundi ya Mwisho ya Mchujo kupata Timu 15 zitakazoungana na Wenyeji Afrika Kusini kucheza Fainali za AFCON 2013, Kombe la Mataifa ya Afrika, Januari 2013.


RATIBA MECHI ZOTE:
ULAYA-Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014
[Saa za Bongo]
Ijumaa Oktoba 12
1800 Russia v Portugal
1830 Finland v Georgia
1900 Armenia v Italy
1900 Faroe Islands v Sweden
1900 Kazakhstan v Austria
2000 Albania v Iceland
2000 Czech Republic v Malta
2030 Liechtenstein v Lithuania
2030 Turkey v Romania
2100 Belarus v Spain
2100 Bulgaria v Denmark
2100 Moldova v Ukraine
2115 Slovakia v Latvia
2130 Estonia v Hungary
2130 Netherlands v Andorra
2130 Serbia v Belgium
2145 Greece v Bosnia-Hercegovina
2145 Rep of Ireland v Germany
2145 Wales v Scotland
2200 England v San Marino
2200 Luxembourg v Israel
2230 Macedonia v Croatia
2230 Switzerland v Norway
2245 Slovenia v Cyprus


Jumanne Oktoba 16
Albania v Slovenia
Andorra v Estonia
Belarus v Georgia
Belgium v Scotland
Bosnia-Hercegovina v Lithuania
Czech Republic v Bulgaria
Hungary v Turkey
Iceland v Switzerland
Israel v Luxembourg
Latvia v Liechtenstein
Macedonia v Serbia
Portugal v Northern Ireland
Romania v Netherlands
Russia v Azerbaijan
San Marino v Moldova
Slovakia v Greece
Spain v France
Ukraine v Montenegro
2000 Cyprus v Norway
2100 Faroe Islands v Rep of Ireland
2130 Austria v Kazakhstan
2130 Croatia v Wales
2145 Germany v Sweden
2145 Italy v Denmark
2200 Poland v England


FAHAMU:
-ULAYA yapo Makundi 9
-Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.
++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013=Kombe la Mataifa ya Afrika
[Fainali Afrika Kusini-Januari 2013]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za kwanza]


Jumamosi Oktoba 13
Malawi v Ghana [0-2]
Botswana v Mali [0-3]
Nigeria v Liberia [2-2]
Uganda v Zambia [0-1]
E.Guinea v Congo DR [0-4]
Senegal v Cote d'Ivoire [2-4]
Tunisia v Sierra Leone [2-2]
Morocco v Mozambique [0-2]


Jumapili Oktoba 14
Algeria v Libya [1-0]
Cameroon v Cape Verde [0-2]
Togo v Gabon [1-1]
Angola v Zimbabwe [1-3]
Niger v Guinea [0-1]
Ethiopia v Sudan [3-5]
Burkina Faso v Central African Republic [0-1]
FAHAMU: Washindi 15 wa Mechi hizi watajumuika na Wenyeji Afrika Kusini kwenye Fainali zitakazochezwa Afrika Kusini Januari 2013.
++++++++++++++++++++++++++++++
MAREKANI ya KUSINI-Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014


MSIMAMO:
1 Argentina Mechi 7 Pointi 14
5 Colombia Mechi 7 Pointi 13
3 Ecuador Mechi 7 Pointi 13
4 Uruguay Mechi 7 Pointi 12
2 Chile Mechi 7 Pointi 12
6 Venezuela Mechi 8 Pointi 11
7 Peru Mechi 7 Pointi 7
8 Bolivia Mechi 7 Pointi 4
9 Paraguay Mechi 7 Pointi 4


FAHAMU: Timu 4 za juu zinatinga Fainali Brazil moja kwa moja na ile ya 5 itaenda Mechi ya Mchujo.


Ijumaa Oktoba 12
Colombia v Paraguay
Ecuador v Chile
Bolivia v Peru
Argentina v Uruguay


Jumanne Oktoba 16
Bolivia v Uruguay
Venezuela v Ecuador
Paraguay v Peru
Chile v Argentina
++++++++++++++++++++++++++++++
CONCACAF [Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean]- Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014==RAUNDI ya 3
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUNDI A
-USA
-Guatemala
-Jamaica
-Antigua and Barbuda

KUNDI B
-Mexico
-El Salvador
-Costa Rica
-Guyana

KUNDI C
-Panama
-Honduras
-Canada
-Cuba



FAHAMU:
-Mshindi wa kila Kundi na Mshindi wa Pili wataingia Raundi ya 4 ambayo ni ya mwisho itayochezwa kwa mtindo wa Ligi ili kutoa Timu 3 zitakazoenda Fainali za Kombe la Dunia moja kwa moja na ya 4 itapelekwa Mechi ya Mchujo.
-Kundi B: Mexico wamefuzu kuingia Raundi ya 4 kwa vile tayari wana Pointi 12 wakifuatiwa na El Salvador wenye 5, Costa Rica 4 na Guyana 1 huku kila Timu imebakiza Mechi 2.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++


RATIBA:
Ijumaa Oktoba 12
Antigua and Barbuda v USA
El Salvador v Costa Rica
Canada v Cuba
Guatemala v Jamaica
Guyana v Mexico
Panama v Honduras


Jumanne Oktoba 16
Honduras v Canada
Cuba v Panama
USA v Guatemala
Jamaica v Antigua and Barbuda
Costa Rica v Guyana
Mexico v El Salvador

BPL: Likizoni hadi Oktoba 20!

Jumatatu, 08 Oktoba 2012 17:55
 
>>KILELENI BADO Chelsea, Man United!
>>BAADA ‘VAKESHENI’ Timu kukabiliwa na CHAMPIONS LIGI & CAPITAL ONE CUP!!
BPL_LOGOLigi Kuu England, rasmi kama Barclays Premier League, BPL, inaenda ‘vakesheni’ kupisha Mechi za Kimataifa ambazo zipo kwenye Kalenda ya FIFA zitakazochezwa Oktoba 12 na 16 na Ligi hii itarejea tena dimbani hapo Oktoba 20.


Hadi Ligi hii inasimama, Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, ndio wapo kileleni wakiwa na Pointi 19 na hawajapoteza hata Mechi moja katika 7 huku wakiwa wametoka sare Mechi moja tu.


Timu iliyo nafasi ya pili ni Manchester United yenye Pointi 15 wakifuatia Mabingwa watetezi Manchester City ambao pia wana Pointi 15 lakini wamezidiwa kwa ubora wa magoli.
Mkiani wapo QPR ambao wana Pointi 2 tu.
+++++++++++++++++++++++++++++
MECHI ZINAZOFUATA ZA TIMU VIGOGO KWA MASHINDANO YOTE:
++NI LIGI KUU ENGLAND ISIPOKUWA INAPOTAJWA.
CHELSEA MAN CITY MAN UNITED ARSENAL
Oktoba 20
Spurs v Chelsea
Oktoba 23
Shakhtar v Chelsea [UCL]
Oktoba 28
Chelsea v Man Utd
Oktoba 31
Chelsea v Man Utd
[COC]
Novemba 3
Swansea v Chelsea
Novemba 11
Chelsea v L’pool


Oktoba 20
WBA v Man City
Oktoba 24
Ajax v Man City [UCL]
Oktoba 27
M City v Swansea
Novemba 3
West Ham v M City
Novemba 11
M City v Spurs
Oktoba 20
Man United v Stoke
Oktoba 23
Man U v Braga [UCL]
Oktoba 28
Chelsea v Man Utd
Oktoba 31
Chelsea v Man Utd
[COC]
Novemba 3
Man U v Arsenal
Novemba 10
Villa v Man United
Oktoba 20
Norwich v Arsenal
Oktoba 24
Arsenal v Schalke [UCL]
Oktoba 27
Arsenal v QPR
Oktoba 30
Reading v Arsenal
[COC]
Novemba 3
Man U v Arsenal
Novemba 10
Arsenal v Fulham
++UCL==UEFA CHAMPIONZ LIGI
++COC==CAPITAL ONE CUP
+++++++++++++++++++++++++++++
BPL:
MSIMAMO:
BPLSTAND08OCT12
BPL:
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi, Oktoba 20, 2012
[Saa za Bongo]


[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Tottenham Hotspur v Chelsea [White Hart Lane]
[Saa 11 Jioni]
Fulham v Aston Villa [Craven Cottage]
Liverpool v Reading [Anfield]
Manchester United v Stoke City [Old Trafford]
Swansea City v Wigan Athletic [Liberty Stadium]
West Bromwich Albion v Manchester City [The Hawthorns]
West Ham United v Southampton [Upton Park]


[Saa 1 Dak 30 Usiku]
16:30  Norwich City v Arsenal [Carrow Road]
Jumapili, Oktoba 21, 2012
[Saa 9 Dak 30 Mchana]
12:30  Sunderland v Newcastle United [Stadium of Light]
[Saa 12 Jioni]
15:00  Queens Park Rangers v Everton [Loftus Road]

No comments:

Post a Comment