Saturday, October 20, 2012

BPL: Wachezaji gani kukosekana kila Timu kwa Mechi Wikiendi hii!


BPL_LOGOIfuatayo ni Taarifa fupi kutoka Kambi ya kila Timu ya Ligi Kuu England, BPL, kuhusu hali za Wachezaji wao na yupi atakosekana kwa Mechi za Ligi Wikiendi hii:
JUMAMOSI Oktoba 20
Tottenham v Chelsea
Uwanja: White Hart Lane Saa: 8 Dakika 45 Mchana
Kwa Tottenham Scott Parker (Kifundo cha Mguu) hatacheza lakini Jake Livermore na Kyle Naughton wanaweza kuwemo Kikosini.
John Terry anaanza kutumikia Kifungo cha Mechi 4 kwa Chelsea kuanzia Mechi hii.
Refa: M Dean
Fulham v Aston Villa
Uwanja: Craven Cottage Saa: 11 Jioni
Dimitar Berbatov, aliekuwa akijiuguza paja, na Mladen Petric ,mguu, wote wamepona na wanaweza kuichezea Fulham pamoja na Mahamadou Diarra, aliepona goti, lakini Bryan Ruiz, maumivu ya nyonga, huenda asicheze.
Aston Villa hawana matatizo.
Refa: C Foy
Liverpool v Reading
Uwanja: Anfield Saa: 11 Jioni
Liverpool huenda wakamkosa Kipa wao Pepe Reina, alieumia musuli ya Mguu akiwa na Spain, na pia Straika Fabio Borini, alievunjika mguu, hatacheza lakini Jonjo Shelvey anarudi Kikosini baada ya kutumikia Kifungo.
Reading wanasubiri Madaktari waamue kama Noel Hunt, aliekuwa kaumia Kifundo cha Mguu, kama anweza kucheza lakini Mikele Leigertwood tayari ameruhusiwa na Madaktari.
Refa: R East
Man United v Stoke
Uwanja: Old Trafford Saa: 11 Jioni
Winga Ashley Young (Goti) amepona na anaweza kuichezea Manchester United baada ya kuwa nje kwa Miezi miwili lakini Chris Smalling bado kuwa fiti kwa Mechi. Stoke wana wasiwasi juu ya Glenn Whelan, Mguu, na Michael Owen, nyonga lakini Andy Wilkinson amepona.
Refa: A Taylor
Swansea v Wigan
Uwanja: Liberty Saa: 11 Jioni
Swansea hawana matatizo lakini Wigan watawakosa Antolin Alcaraz na Albert Crusat.
Refa: M Jones
West Brom v Man City
Uwanja: The Hawthorns Saa: 11 Jioni
Wasiwasi kwa West Bromwich Albion ni juu ya Youssouf Mulumbu na Manchester City watawakosa Viungo David Silva na Jack Rodwell, wote wakiwa na maumivu ya musuli za pajani pamoja na Javi Garcia, paja, na Maicon, mguu.
Refa: M Clattenburg
West Ham v Southampton
Uwanja: Upton Park Saa: 11 Jioni
West Ham watamkosa Ricardo Vaz Te alieteguka bega huku Winston Reid, mgongo, na Guy Demel, paja, wakingonja kupasishwa kuwa fiti. Gaston Ramirez na Frazer Richardson ni majeruhi na hawataichezea Southampton.
Refa: N Swarbrick
Norwich v Arsenal
Uwanja: Carrow Road Saa: 1 na Nusu Usiku
Norwich wako poa lakini Arsenal watawakosa Laurent Koscielny, mgongo, Kieran Gibbs, paja, na Theo Walcott, kifua. Jack Wilshere na Emmanuel Frimpong huenda wakawemo Kikosini baada ya kupona maumivu ya muda mrefu.
Refa: L Probert
JUMAPILI Oktoba 21
Sunderland v Newcastle
Uwanja: Staium of Light Saa: 9 na Nusu Mchana
Sunderland watamkosa Titus Bramble, maumivu ya paja na Lee Cattermole ambae amefungiwa. Hawana matatizo baada ya kupona Fabricio Coloccini na Steven Taylor.
Refa: M Atkinson
QPR v Everton
Uwanja: Loftus Road Saa: 12 Jioni
QPR wana wasiwasi na Armand Traoré na Fabio bado majeruhi lakini Samba Diakité amepona. Everton watacheza bila ya Marouane Fellaini alieumia goti.
Refa: J Moss


Kiongozi FIFA ataka ‘Wabaguzi’ Serbia wafungiwe, Terry bado Kepteni Chelsea, Shabiki amtwanga Kipa Uwanjani!


FREDINAND-TERRY_MKNO_HAMNAKufuatia vitendo vya Mashabiki wa Serbia vilivyokithiri vya Ubaguzi, Kiongozi wa juu wa FIFA ameitaka Nchi hiyo ifungiwe na huko Stamford Bridge, Chelsea imetamka John Terry atabaki kuwa Kepteni licha ya kusulubiwa kwa Ubaguzi wakati huko Uwanja wa Hillsborough Shabiki mmoja alivamia Uwanjani na kumpiga Kipa hadi akamwangusha chini.
UBAGUZI Serbia v England:  Makamu Rais FIFA, Jim Boyce, aitaka Serbia ifungiwe!
Makamu wa Rais wa FIFA, Jim Boyce, ameitaka UEFA ifikirie kuifungia Serbia katika Mashindano yajayo kufuatia tuhuma za Ubaguzi wa Washabiki wao zilizotokea kwenye Mechi ya kuwania kuingia Fainali za EURO 2013 kwa Vijana wa Chini ya Miaka 21 iliyochezwa huko Nchini Serbia Jumanne iliyopita na England kufuzu kwenda Fainali baada ya kushinda Mechi zote mbili kwa bao 1-0 kila moja.
Tayari UEFA imeshaifungulia Serbia Mashitaka ya Ubaguzi na pia kushindwa kudhibiti Wachezaji wake kosa ambalo pia FA ya England imeshitakiwa.
Kuhusu shutuma za Ubaguzi, Jim Boyce, ametamka: “Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya FA ya Serbia! Wafungiwe Viwanja vyao na pia uangaliwe uwezekano wa kutowashirikisha Mashindano yajayo.”
Boyce pia alidai vitendo vya Ubaguzi vya Serbia si mara ya kwanza na inabidi hatua kali zichukuliwe kuvikomesha.

Terry abakishwa Kepteni Chelsea
Licha ya kusulubiwa kwa Ubaguzi na FA pamoja na Klabu yake mwenyewe, Nahodha wa Chelsea, John Terry, ataendelea kubaki kama Kepteni wa Timu hiyo kufuatia uamuzi huo kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Bruce Buck.
Terry amefungiwa na FA Mechi 4 na pia kupigwa Faini Pauni 220,000 na pia Chelsea imethibitisha kumpiga ‘Faini kubwa.’ kwa kosa la kumkashifu Kibaguzi Beki wa QPR Anton Ferdinand kwenye Mechi iliyochezwa Loftus Road hapo Oktoba 23, 2011.

Kipa Chris Kirkland apigwa Uwanjani na Shabiki wa Leeds!
Kipa wa Sheffield Wednesday Chris Kirkland hapo jana alivamiwa Uwanjani wakati wa Mechi ya Timu yake na Leeds United na kushambuliwa na Shabiki wa Leeds kwa nguvu kubwa na kumfanya aanguke chini na kuhitaji matibabu.
Hata hivyo, Kipa huyo wa zamani wa Liverpool mwenye Miaka 31, na ambae pia aliwahi kuichezea England Mechi moja, aliweza kuendelea na kumaliza Mechi hiyo iliyokwisha matokeo yakiwa 1-1.
Akiongelea tukio hilo, Meneja wa Sheffield Wednesday, Dave Jones, alisema: “Hawa ni kama Wanyama. Wapigwe marufuku kwenye Viwanja vyote vya ugenini ikiwa tabia yao ni hii!”
Kwenye Mechi hiyo waliyocheza ugenini, Leeds ilikuwa na Mashabiki 5,300 kati 28,582 waliokuwepo Uwanjani.
Mara baada ya Mechi hiyo Klabu ya Leeds iliomba radhi kwa tukio hilo na kusema itashirikiana na Polisi ili kumtambua Shabiki huyo.


BPL: Chelsea yaidunda Spurs wazidi kupaa kileleni!


BPL_LOGOChelsea leo wamepata ushindi wao wa kwanza Uwanja wa White Hart Lane tangu Mwaka 2005 walipoibonda Tottenham mabao 4-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyoanza mapema na ushindi huo umewafanya Chelsea waendelee kuongoza Ligi wakiwa na Pointi 22 kwa Mechi 8.
Chelsea ndio walitangulia kufunga bao katika Dakika ya 17 mfungaji akiwa Gary Cahill na bao hilo kudumu hadi mapumziko.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Tottenham 2= Gallas 47′ Defoe 54′ .
Chelsea 4= Cahill 17′ Mata 66′, 69′ Sturridge 90′
+++++++++++++++++++++++++++++++
Kipindi cha Pili, Spurs walizinduka na kufunga bao mbili kupitia William Gallas na Jermain Defoe.
Hata hivyo, Chelsea waliendelea kutawala na Juan Mata akasawazisha na kupiga bao jingine na kuwafanya waongoze kwa bao 3-2 kabla Mchezaji alietoka benchi Daniel Sturridge kupiga bao la 4.
Haya ni matokeo ya kumvunja nguvu Meneja wa Tottenham manager Andre Villas-Boas ambae alikuwa kisimamia Mechi yake ya kwanza dhidi ya Chelsea ambayo ilimfukuza mwanzoni mwa Mwaka huu.
=============================
VIKOSI:
Tottenham: Friedel, Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen, Huddlestone, Sandro, Lennon, Sigurdsson, Dempsey, Defoe
Akiba: Lloris, Adebayor, Naughton, Dawson, Falque, Livermore, Townsend.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Ramires, Mikel, Oscar, Hazard, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Lampard, Moses, Sturridge, Azpilicueta, Bertrand.
Refa: Mike Dean (Wirral)
=============================

No comments:

Post a Comment