VPL: Yanga yatoka nyuma 2-0, yashinda 3-2!
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 20
Yanga 3 Ruvu Shootings 2
Coastal Union 3 Mtibwa Sugar 1
++++++++++++++++++++++
Katika mfululizo wa Mechi za Ligi Kuu
Vodacom zilizochezwa leo, Yanga, ikicheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
ilijikuta iko nyuma kwa bao 2-0 ndani ya Dakika 9 za kwanza walipocheza
na Ruvu Shooting lakini wakazinduka na kushinda bao 3-2.
Ruvu Shooting walipiga bao zao 2 kupitia Seif Abdallah katika Dakika ya 2 na ya 9.
Bao za Yanga zilifungwa na Mbuyu Twite, Dakika ya 20, Jerry Tegete, Dakika ya 35 na Didier Kavumbagu katika Dakika ya 65.
Katika Mechi nyingine ya VPL iliyochezwa huko Mkwakwani, Jijini Tanga, wenyeji Coastal Union waliifunga Mtibwa Sugar bao 3-1.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumapili.
++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili Oktoba 21
JKT Ruvu v JKT Oljoro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mgambo JKT v Simba [Mkwakwani, Tanga]
Tanzania Prisons v Toto Africans [Sokoine, Mbeya]
++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO VPL:
1 Simba Mechi 8 Pointi 18
2 Azam FC Mechi 7 Pointi 17
3 Yanga SC Mechi 8 Pointi 14
4 Coastal Mechi 8 Pointi 13
5 JKT Oljoro Mechi 8 Pointi 13
6 Kagera Mechi 8 Pointi 12
7 JKT Ruvu Mechi 8 Pointi 10
8 Prisons Mechi 7 Pointi 9
9 Ruvu Shooting Mechi 8 Pointi 9
10 JKT Mgambo Mechi 8 Pointi 9
11 Mtibwa Sugar Mechi 7 Pointi 8
12 Toto African Mechi 8 Pointi 7
13 African Lyon Mechi 8 Pointi 7
14 Polisi Moro Mechi 8 Pointi 2
Man United safi, Mtu 10 Man City poa, Liverpool yashinda!
>>’KINDA’ Rahim Sterling aipa ushindi Liverpool!
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 20
Fulham 1 Aston Villa 0
Liverpool 1Reading 0
Man United 4 Stoke 2
Swansea 2 Wigan 1
West Brom 1 Man City 2
West Ham 4 Southampton 1
[SAA 1 na Nusu Usiku]
Norwich v Arsenal
=============================
Man United 4 Stoke 2
Manchester United, wakicheza kwao Old
Trafford, walitoka nyuma kwa bao 1-0 alilojifunga mwenyewe Wayne Rooney
na kuichapa Stoke City kwa bao 4-2.
++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Man United= 4 Rooney 27′, 65′ Van Persie 44′ Welbeck 46′ .
Stoke= 2 Rooney 11′ (Kajifunga mwenyewe) Kightly 58′ .
++++++++++++++++++++
Ushindi huu umeifanya Man United
iendelee kukamata nafasi ya pili wakiwa na Pointi 18 na wapo nyuma ya
vinara Chelsea kwa Pointi 4 huku Mechi inayofuata ni safari ya kwenda
huko Stamford Bridge kupambana na Chelsea Wiki ijayo.
VIKOSI:
Man United: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Evans, Evra, Valencia, Scholes, Carrick, Welbeck, van Persie, Rooney
Akiba: Lindegaard, Anderson, Giggs, Hernandez, Nani, Powell, Wootton.
Stoke: Begovic, Cameron, Huth, Shawcross, Wilson, Nzonzi, Whitehead, Walters, Adam, Kightly, Crouch
Akiba: Sorensen, Palacios, Jones, Owen, Upson, Etherington, Wilkinson.
Refa: Anthony Taylor
+++++++++++++++++++++++++++++++
Fulham 1 Aston Villa 0
Bao la Dakika ya 84 la Chris Baird
limewapa Fulham ushindi wa bao 1-0 wakiwa nyumbani kwao Craven Cottage
walipocheza na Aston Villa.
VIKOSI:
Fulham: Schwarzer, Riether, Hughes, Hangeland, Riise, Sidwell, Baird, Richardson, Rodallega, Berbatov, Petric
Akiba: Stockdale, Senderos, Kasami, Karagounis, Diarra, Dejagah, Kacaniklic.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Bennett, Ireland, El Ahmadi, Delph, Holman, Bent, Agbonlahor
Akiba: Given, N'Zogbia, Albrighton, Benteke, Bannan, Weimann, Lichaj.
Refa: Chris Foy
+++++++++++++++++++++++++++++++
West Ham 4 Southampton 1
West ham leo wameichapa Southampton bao 4-1 kwa bao za Mark Noble, bao mbili, Kevin Nolan na Modibo Maiga.
Bao pekee la Southampton lilifungwa na Adam Lallana.
VIKOSI:
West Ham: Jaaskelainen, Tomkins, Collins, Reid, McCartney, Noble, Diame, Benayoun, Nolan, Jarvis, Carroll
Akiba: Spiegel, Cole, Maiga, Spence, O'Neil, Chambers, Hall.
Southampton: Boruc, Clyne, Hooiveld, Fonte, Yoshida, Puncheon, Schneiderlin, Steven Davis, Lallana, Rodriguez, Do Prado
Akiba: Kelvin Davis, Lambert, Ward-Prowse, Mayuka, Seaborne, Chaplow, Reeves.
Refa: Neil Swarbrick
+++++++++++++++++++++++++++++++
Liverpool 1 Reading 0
Bao pekee la Kinda Raheem Sterling
limewapa Liverpool ushindi wao wa kwanza Uwanjani kwao Anfield chini ya
Meneja Brendan Rodgers.
VIKOSI:
Liverpool: Jones, Wisdom, Skrtel, Agger, Johnson, Gerrard, Allen, Sahin, Fernandez Saez, Suarez, Sterling
Akiba: Gulacsi, Jose Enrique, Assaidi, Henderson, Downing, Carragher, Shelvey.
Reading: McCarthy, Cummings, Gorkss, Mariappa, Shorey, Kebe, Guthrie, Leigertwood, Karacan, McAnuff, Pogrebnyak
Akiba: Stuart Taylor, Gunter, Pearce, Le Fondre, McCleary, Robson-Kanu, Roberts.
Refa: Roger East
+++++++++++++++++++++++++++++++
Swansea 2 Wigan 1
Wachezaji kutoka Spain, Pablo Hernandez
na Miguel Michu, leo wamepiga bao na kuipa Swansea ushindi wa bao 2-
1 dhidi ya Wigan.
Bao la Wigan lilifungwa na Emmerson Boyce.
VIKOSI:
Swansea: Vorm, Rangel, Chico, Williams, Davies, Routledge, de Guzman, Ki, Britton, Hernandez, Michu
Akiba: Tremmel, Graham, Dyer, Monk, Shechter, Moore, Tiendalli.
Wigan: Al Habsi, Caldwell, Figueroa, Ramis, McCarthy, McArthur, Boyce, Beausejour, Kone, Maloney, Di Santo
Akiba: Pollitt, Jones, Watson, Gomez, McManaman, Boselli, Miyaichi.
Refa: Mike Jones
+++++++++++++++++++++++++++++++
West Brom 1 Man City 2
Dakika moja toka aingingizwe kutoka
benchi Edin Dzeko aliwaokoa Mabingwa Manchester City, waliokuwa
wakicheza Mtu 10 baada ya James Milner kupewa Kadi Nyekundu, kutoka
kwenye kipigo kwa kusawazisha bao katika Dakika ya 80 na kufunga bao la
pili na la ushindi katika Dakika ya 90.
++++++++++++++++++++
MAGOLI:
WBA= 1 Shane Long, 67
Man City= 2 Edin Dzeko 80 na 90
++++++++++++++++++++
Ushindi huu umewafanya Man City wabakie
nafasi ya 3 kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa na Pointi 18 sawa na Timu ya
pili Man United ambayo imewazidi kwa ubora wa mabao na vinara bado ni
Chelsea wenye Pointi 22.
VIKOSI:
West Brom: Foster, Ridgewell, Olsson, McAuley, Tamas, Yacob, Mulumbu, Dorrans, Morrison, Fortune, Long
Akiba: Luke Daniels, Popov, Rosenberg, Jara Reyes, Lukaku, Gera, Odemwingie.
Man City: Hart, Clichy, Lescott, Kompany, Richards, Milner, Barry, Nasri, Toure, Balotelli, Tevez
Akiba: Pantilimon, Zabaleta, Dzeko, Sinclair, Kolarov, Aguero, Toure.
Refa: Mark Clattenburg
+++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA
Jumapili Oktoba 21
[SAA 9 na Nusu Mchana]
Sunderland v Newcastle
[SAA 12 Jioni]
QPR v Everton
BPL: Chelsea yaidunda Spurs wazidi kupaa kileleni!
Chelsea
leo wamepata ushindi wao wa kwanza Uwanja wa White Hart Lane tangu
Mwaka 2005 walipoibonda Tottenham mabao 4-2 katika Mechi ya Ligi Kuu
England iliyoanza mapema na ushindi huo umewafanya Chelsea waendelee
kuongoza Ligi wakiwa na Pointi 22 kwa Mechi 8.
Chelsea ndio walitangulia kufunga bao katika Dakika ya 17 mfungaji akiwa Gary Cahill na bao hilo kudumu hadi mapumziko.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Tottenham 2= Gallas 47′ Defoe 54′ .
Chelsea 4= Cahill 17′ Mata 66′, 69′ Sturridge 90′
+++++++++++++++++++++++++++++++
Kipindi cha Pili, Spurs walizinduka na kufunga bao mbili kupitia William Gallas na Jermain Defoe.
Hata hivyo, Chelsea waliendelea kutawala
na Juan Mata akasawazisha na kupiga bao jingine na kuwafanya waongoze
kwa bao 3-2 kabla Mchezaji alietoka benchi Daniel Sturridge kupiga bao
la 4.
Haya ni matokeo ya kumvunja nguvu Meneja
wa Tottenham manager Andre Villas-Boas ambae alikuwa kisimamia Mechi
yake ya kwanza dhidi ya Chelsea ambayo ilimfukuza mwanzoni mwa Mwaka
huu.
=============================
VIKOSI:
Tottenham: Friedel, Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen, Huddlestone, Sandro, Lennon, Sigurdsson, Dempsey, Defoe
Akiba: Lloris, Adebayor, Naughton, Dawson, Falque, Livermore, Townsend.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Ramires, Mikel, Oscar, Hazard, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Lampard, Moses, Sturridge, Azpilicueta, Bertrand.
Refa: Mike Dean (Wirral)
=============================
>>LEO ni ‘ALMASI’ au ‘MAWINGA’??
Ingawa Sir Alex Ferguson ametoboa kuwa
atakuwa akibadilisha Mifumo ya Uchezaji ya Timu yake ya Manchester
United kutoka Fomesheni ya ‘Almasi’ na wakati mwingine kutumia Mfumo
wenye Mawinga kama ilivyozoeleka kwa Kikosi chake lakini kwa ajili ya
Mechi yao ya leo ya Ligi Kuu England itakayochezwa Uwanjani Old Trafford
dhidi ya Stoke City, Meneja huyo amekataa kuthibitisha nini kitatumika.
Akichezesha Kikosi cha bila ya Mawinga,
kwa kutumia Mfumo wa ‘Almasi’, Wayne Rooney hurudishwa kwenye Kiungo na
kucheza nyuma ya Mastraika Robin van Persie na Danny Welbeck mtindo
ambao waliutumia walipoifumua Newcastle bao 3-0 kwenye Mechi yao ya
mwisho ya Ligi.
Lakini kwa Mechi ya leo, na hasa baada
kupona kwa Ashley Young, na pia kuwepo kwa Nani na Valencia, huenda Sir
Alex akawatumia Wachezaji hao kucheza kwenye Wingi.
Sir Alex Ferguson amesema: “Ni ngumu
kupanga Timu. Nadhani wakati mwingine Fomesheni ya Almasi inafanya kazi
vizuri, wakati mwingine tunahitaji Mawinga. Tunaweza kucheza yeyote.
Tony Pulis [Meneja wa Stoke City] atakuwa akijiuliza tutacheza Fomesheni
ipi lakini pia naweza kutumia vyote, Almasi na Mawinga, na kuwa na
Walinzi wawili tu!”
Hata hivyo Stoke City ni Timu ya kipekee
kwenye Ligi Kuu inayotumia nguvu na mipira mirefu, hasa ya kurusha,
wakimlenga ‘Ngongoti’ Peter Crouch lakini Sir Alex Ferguson amesema hilo
watalidhibiti na haliwasumbii.
Amesisitiza: "Cheza mchezo wako huna
haja ya kuogopa au kufikiria sana wao watacheza vipi. Tunajua watapata
frikiki, tunajua watatumia mipira mirefu kuingiza ndani ya boksi letu na
watatumia mipira mirefu kwa Peter Crouch."
Amemalizia: “Matayarisho ni rahisi tu.
Tunajua kile watakachokifanya. Mara nyingine unacheza na Timu hujui
watafanya nini. Dhidi ya Stoke tunajua kila kitu watakachofanya. Wacha
tu tucheze gemu yetu wenyewe. Pengine hilo litafanya kazi vyema kwetu.”
Kiongozi FIFA ataka ‘Wabaguzi’ Serbia wafungiwe, Terry bado Kepteni Chelsea, Shabiki amtwanga Kipa Uwanjani!
Kufuatia
vitendo vya Mashabiki wa Serbia vilivyokithiri vya Ubaguzi, Kiongozi wa
juu wa FIFA ameitaka Nchi hiyo ifungiwe na huko Stamford Bridge,
Chelsea imetamka John Terry atabaki kuwa Kepteni licha ya kusulubiwa kwa
Ubaguzi wakati huko Uwanja wa Hillsborough Shabiki mmoja alivamia
Uwanjani na kumpiga Kipa hadi akamwangusha chini.
UBAGUZI Serbia v England: Makamu Rais FIFA, Jim Boyce, aitaka Serbia ifungiwe!
Makamu wa Rais wa FIFA, Jim Boyce,
ameitaka UEFA ifikirie kuifungia Serbia katika Mashindano yajayo
kufuatia tuhuma za Ubaguzi wa Washabiki wao zilizotokea kwenye Mechi ya
kuwania kuingia Fainali za EURO 2013 kwa Vijana wa Chini ya Miaka 21
iliyochezwa huko Nchini Serbia Jumanne iliyopita na England kufuzu
kwenda Fainali baada ya kushinda Mechi zote mbili kwa bao 1-0 kila moja.
Tayari UEFA imeshaifungulia Serbia
Mashitaka ya Ubaguzi na pia kushindwa kudhibiti Wachezaji wake kosa
ambalo pia FA ya England imeshitakiwa.
Kuhusu shutuma za Ubaguzi, Jim Boyce,
ametamka: “Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya FA ya Serbia!
Wafungiwe Viwanja vyao na pia uangaliwe uwezekano wa kutowashirikisha
Mashindano yajayo.”
Boyce pia alidai vitendo vya Ubaguzi vya Serbia si mara ya kwanza na inabidi hatua kali zichukuliwe kuvikomesha.
Terry abakishwa Kepteni Chelsea
Licha ya kusulubiwa kwa Ubaguzi na FA
pamoja na Klabu yake mwenyewe, Nahodha wa Chelsea, John Terry,
ataendelea kubaki kama Kepteni wa Timu hiyo kufuatia uamuzi huo
kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Bruce Buck.
Terry amefungiwa na FA Mechi 4 na pia
kupigwa Faini Pauni 220,000 na pia Chelsea imethibitisha kumpiga ‘Faini
kubwa.’ kwa kosa la kumkashifu Kibaguzi Beki wa QPR Anton Ferdinand
kwenye Mechi iliyochezwa Loftus Road hapo Oktoba 23, 2011.
Kipa Chris Kirkland apigwa Uwanjani na Shabiki wa Leeds!
Kipa wa Sheffield Wednesday Chris
Kirkland hapo jana alivamiwa Uwanjani wakati wa Mechi ya Timu yake na
Leeds United na kushambuliwa na Shabiki wa Leeds kwa nguvu kubwa na
kumfanya aanguke chini na kuhitaji matibabu.
Hata hivyo, Kipa huyo wa zamani wa
Liverpool mwenye Miaka 31, na ambae pia aliwahi kuichezea England Mechi
moja, aliweza kuendelea na kumaliza Mechi hiyo iliyokwisha matokeo
yakiwa 1-1.
Akiongelea tukio hilo, Meneja wa
Sheffield Wednesday, Dave Jones, alisema: “Hawa ni kama Wanyama. Wapigwe
marufuku kwenye Viwanja vyote vya ugenini ikiwa tabia yao ni hii!”
Kwenye Mechi hiyo waliyocheza ugenini, Leeds ilikuwa na Mashabiki 5,300 kati 28,582 waliokuwepo Uwanjani.
Mara baada ya Mechi hiyo Klabu ya Leeds
iliomba radhi kwa tukio hilo na kusema itashirikiana na Polisi ili
kumtambua Shabiki huyo.
No comments:
Post a Comment