KIUNGO BORA WA BARCA INIESTA ASEMA ATAMALIZA ZAMA ZAKE ZA SOKA BARCELONA
KIUNGO nyota wa
kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Andres Iniesta amebainisha
kuwa hana mpango ya kuondoka katika klabu hiyo na kudai kuwa anataka
kutundika daruga akiwa hapo. Iniesta
mwenye umri wa miaka 28 ameshacheza mechi zaidi ya 400 katika kikosi
cha kwanza cha Barcelona toka alipotoka katika shule ya klabu hiyo na
anategemea kuendelea kuwepo zaidi hapo. Akihojiwa
Iniesta amesema nia yake ni kucheza mpaka atapostaafu akiwa katika
klabu hiyo na kitu pekee kinachoweza kubadilisha ni kiwango chake kwani
kama kitashuka na klabu kuamua kumuacha ndio anayoweza kuondoka. Nyota
pia alikiri kuwa timu hiyo inakabiliwa na wakati mgumu hivi sasa na
wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanarejea katika kiwango chao
haraka kabla ya mchezo wa Kombe la Mfalme dhidi ya Malaga.
No comments:
Post a Comment