PLATINI AMPONGEZA PRINCE BOATENG.
RAIS wa Shirikisho la
Soka arani Ulaya, Michel Platini ametofautiana na rais wa Shirikisho la
Soka la Dunia Sepp Blatter kuhusu suala la Kevin-Prince Boateng
kuwaongoza wachezaji wenzake wa AC Milan kutoka uwanjani baada ya
kufanyiwa vitendo vya kibaguzi mapema mwezi huu. Blatter
amesema wachezaji hawapaswi kujichukuliwa sheria mkononi ingawa alidai
kuwa mashabiki wanaokutwa na hatia ya kufanya vitendo hivyo wanapaswa
kuchuliwa hatua aidha kwa klabu kukatwa alama au kufungiwa kabisa. Hatahivyo,
Platini aliiambia radio moja nchini Ufaransa kuwa anakiunga mkono
kitendo kilichofanywa na nyota huyo wa kimataifa kutoka Ghana kwani
tatizo hilo linaonekana kuota mizizi katika siku za karibuni. Platini
mwenye umri wa miaka 57 amesema ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa
uliofanywa na wachezaji wa Milan na baada ya tukio hilo aliwapigia simu
na kuwapongeza.
No comments:
Post a Comment