Friday, January 11, 2013

AUSTRALIA OPEN DRAW: DJOKOVIC, MURRAY KUKUTANA FAINALI KAMA WAKIFANIKIWA KUFIKA HUKO.


MCHEZAJI nyota anayeshika namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic na Andy Murray ambaye ni bingwa wa michuano ya US Open wamepangwa tofauti katika ratiba ya michuano ya wazi ya Australia inayotarajiwa kuanza jijini Melbourne Jumatatu ijayo. Katika ratiba rasmi iliyopangwa mapema leo, Djokovic anaweza kukutana katika nusu fainali na David Ferrer anayeshika namba nne wakati bingwa mara 17 wa mataji ya Grand Slam Roger Federer anaweza kukutana na Murray anayeshika namba tatu katika hatua kama hiyo. 
Djokovic ataingia katika mashindano hayo akitaka kunyakuwa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kumfunga Rafael Nadal na kunyakuwa taji hilo mwaka jana ambapo anatarajiwa kuanza kampeni zake kwa kucheza na Paul-Henry Mathieu wa Ufaransa. Federer anayeshika nafasi ya pili kwa ubora anatarajia kuanza kampeni zake za kutafuta taji la tano la michuano hiyo kwa kupambana na Benoit Paire pia wa Ufaransa wakati Murray ataanza na Robin Haase wa Uholanzi.

No comments:

Post a Comment