Friday, January 11, 2013

WERE AJIUZA KWA MABAO YAKE KOMBE LA MAPINDUZI



MSHAMBULIAJI wa mabingwa wa Kenya, Tusker FC, Jesse Were anaelekea kuwa mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajiwa kufikia tamati kesho kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa.
Were amefunga mabao manne hadi sasa katika mechi nne alizocheza kwenye mashindano haya na kesho atakuwa na nafasi ya kuongeza mabao akiiongoza timu yake katika fainali dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Azam FC.
Mkenya huyo, anafuatiwa kwa karibu na Adeyum Saleh Mohamed wa Miembeni mwenye mabao matatu, ambaye hata hivyo timu yake jana imetolewa.
Kwa mantiki hiyo, kuelekea mchezo wa kesho wa fainali, mpinzani haswa wa Were kwenye kiatu cha dhahabu cha mashindano haya anabaki kuwa beki Joackins Atudo, Mkenya anayechezea Azam FC.
Atudo atatakiwa kufunga mara tatu kwenye mchezo wa kesho na huku akimuombea dua mbaya Were asizione nyavu ili ampiku Mkenya mwenzake huyo.
Wengine wenye mabao mawili kila mmoja ni Michael Olunga wa Tusker, Haruna Chanongo wa Simba SC, ambaye timu yake imetolewa na Azam katika Nusu Fainali na Mfanyeje Mussa wa Jamhuri, iliyotolewa mapema tu katika hatua ya makundi.
WAFUNGAJI WA MABAO:
Jesse Were                    Tusker FC    3
Adeyum Saleh                Miembeni     3
Joackins Atudo               Azam FC      2
Haruna Chanongo          Simba SC     2
Mfanyeje Mussa             Jamhuri        2

Michael Olunga              Tusker FC    2

No comments:

Post a Comment