Friday, January 11, 2013

KOCHA WA BLACK STARS KWESI APPIAH ANNAN YUKO FITI


KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah amedai kuwa mchezaji nyota wa timu hiyo Anthony Annan alitolewa nje wakati wa kujipima nguvu dhidi ya Misri kwa tahadhari lakini mchezaji huyo atarejea tena uwanjani baada ya siku moja au mbili. Annan ambaye alikuwa nahodha katika mchezo huo aliteleza na kuanguka vibaya kabla ya kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Derek Boateng lakini Appiah amesema hakupatwa na madhara makubwa sana katika tukio hilo. Appiah amesema wachezaji wake wote wako fiti na ni Annan pekee ambaye bado anaonekana kuwa na tatizo lakini amehakikishiwa na daktari kwamba tatizo lake sio kubwa na atarejea katika hali ya kawaida muda mfupi ujao. Annan amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Ghana toka alipoitwa katika michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2008 na kwasasa mchezaji huyo anacheza katika klabu ya Osasuna ya Hispania ambayo imempeleka kwa mkopo katika klabu ya Schalke 04 ya Ujerumani.

No comments:

Post a Comment