Friday, January 11, 2013

WARATIBU WA MASHINDANO YA DAKARA WASEMA WAWILI WAFA DAKAR RALLY.


WARATIBU wa mashindano ya Dakar Rally wamesema kuwa watu wawili wamekufa na wengine saba wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu katika mashindano hayo karibu na mpaka wa Peru na Chile. Ajali hiyo ilitokea wakati ambapo gari moja ya mashindano ilipoligonga gari la kutoa msaada wakati gari nyingine ilipinduka wakati dereva wake akijaribu kukwepa magari hayo yaliyogongana. Tukio hilo lilipekea watu wawili katika gari ndogo ya kwanza akiwemo dereva na msaidizi wake kufa na saba wengine wanne wakiwa raia wa Peru na watatu Waingereza waliokuwepo katika gari ya kutoa msaada waliumia. Waingereza waliojeruhiwa ambao walikuwa katika Land Rover ya kutoa msaada walikuwa wanatoka timu ya Race2Recovery ambao shughuli yao kubwa ni kutoa msaada kwa madereva wanaopata matatizo njiani. Kiongozi wa Race2Recovery, Tony Harris alituma salamu za rambirambi kwa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo mbaya na kusema majeruhi walichukuliwa na kusafirishwa na helikopta kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu zaidi. Mpaka sasa watu wapatao 59 wakiwemo mashabiki 20 wamepoteza maisha katika mbio za Dakar Rally katika miaka ya karibuni lakini waratibu wa mashindano hayo wamekuwa wagumu kuongesha tahadhari za usalama katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment