Friday, January 11, 2013

DAKAR RALLY: AL-ATTIYAH AMZIDI MBIO PETERHANSEL KATIKA HATUA YA SITA.


DEREVA Nasser al-Attiyah wa Qatar amefanikiwa kumpita bingwa mara 10 wa mashindano ya Dakar Rally Stephane Peterhansel kwa zaidi ya dakika nane jana na kuibuka mshindi katika hatua ya sita ya mashindano hayo. Al-Attiyah ambaye alikuwa bingwa wa jumla wa mbio hizo mwaka 2011 alianza mbio hizo jana akiwa nyuma ya bingwa mtetezi wa mbio hizo Peterhansel lakini alifanikiwa kumaliza wa kwanza katika mbio hizo za jana zilizokuwa na kilometa 438 ukiwa ni ushindi wa tatu. Dereva huyo wa Qatar aliyekuwa akitumia gari aina Buggy alitumia muda wa saa 4 na dakika 52 huku Peterhansel anayetumia gari la Mini akikamata nafasi ya pili na nafasi ya tatu ilishikwa na Mmarekani Robby Gordon anayetumia NASCAR. Mbio hizo za Dakar Rally zinafanyika Amerika Kusini katika nchi za Peru na Chile baada ya kuhamishwa kutoka Kaskazini mwa Afrika mwaka 2009 kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea huko.

No comments:

Post a Comment