Friday, January 11, 2013

CHELSEA KWANUKA MASHABIKI CHELSEA KUGOMEA MECHI KUMPINGA BENITEZ??

BENITEZ-CHELSEABAADHI ya MASHABIKI wa Chelsea wameamua kugomea Mechi za Klabu hiyo hadi Meneja wao, Rafael Benitez, atakapoondolewa.
Mara baada ya kupigwa 2-0 na Swansea City Uwanjani Stamford Bridge Jumatano Usiku katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP, hasira zilipamba moto miongoni mwa Mashabiki na Kiongozi wa Kundi rasmi la Mashabiki wa Chelsea, Chelsea Supporters’ Group, aitwae Trizia Fiorellino, alitamka: “Tupo kwenye hali ya machafuko na ipo hatari Klabu itapoteza Roho yake. Najua wapo Mashabiki wasiotaka kuiangalia Chelsea hadi Benitez aondoke. Na kwa uzoefu wangu Mashabiki wanaosusa kuitazama Klabu hawarudi tena!”
Mara baada ya kipigo cha Swansea, Mashabiki walimshushia matusi Mwenyekiti wa Chelsea, Bruce Buck, huku wakiimba na kutaja Majina ya Mameneja waliopita wa Chelsea, Jose Mourinho na Roberto Di Matteo.
Fiorellino alisema: ‘Kuzomewa kwa Bruce Buck kuliungwa mkono na kila mmoja. Tunashukuru kwa yote anayofanya Roman Abramovich kwa Klabu hii lakini kumleta Benitez si sawa kwa Chelsea. Ameletwa ili ‘kumfufua’ Fernando Torres lakini sasa mambo yanazidi kuwa mabovu. Mashabiki wengi hawana imani tena na mwendo wa Klabu na hili linaibomoa Klabu.”
Vile vile, Mashabiki hao wamekasirishwa na jinsi Klabu inavyomtendea Kiungo Nguli Frank Lampard ambae ameshaambiwa hatapewa Mkataba mpya na yuko huru kuondoka.
Fiorellino amesema: “Uamuzi huo hauungwi mkono na sasa John Terry atafuatia!”
Mmiliki Abramovich, ambae yuko Vakesheni huko Visiwa vya Caribbean, ameshajulishwa kuhusu hasira za Mashabiki mara baada ya kufungwa na Swansea City.

No comments:

Post a Comment