Tuesday, January 1, 2013

UCHAGUZI MKUU WA TAFCA MKOA WA TABORA KUFANYIKA JANUARY 10 MWAKA HUU 2013



Uchaguzi  wa TAFCA mkoani Tabora unatarajia kufanyika tarehe 10 mwezi wa kwanza mwaka huu wa 2013 .Nafasi zinazowaniwa ni nafasi ya Uenyekiti,Makamu mwenyekiti,Katibu mkuu, ,Katibu msaidizi,Mweka hazina,,Mjumbe anayewakilisha TAFCA,kwenye mkutano mkuu wa TAFCA Taifa,na Wajumbe 3 wa kamati ya utendaji waliochaguliwa na Mkutano Mkuu.

Fomu zimeanza kutolewa leo kwa katibu wa kamti ya uchaguzi ya TAFCA TTC kwa mwalimu kapaya kuanzia leo terehe 1.1.2013 na mwisho w akurudisha fomu itakuwa tarehe 05/1/2013 saa kumi alasiri.

Kwa nafasi ya Uenyekiti ,Makamu mwenyekiti,Katibu ni shilingi 10,000/= na nafasi za ujumbe wowote ni shilingi elfu tano 5000 pia mwombaji atatakiwa na TAFCA kujaza fomu moja na atatia saini yake pamoja na maelezo ya chama chake.

Pia kila mgombea atalazimika kurudisha fomu hiyo kwa katibu kamati ya uchaguzi ya TAFCA ikiwa na vielelezo vyenye kuthibitisha sifa yake na picha 2 za passport size .tarehe ya usaili katika uchaguzi huo itakuwa ni siku ya tarehe 07/01/2013 kuanzia saa kumi kamili jioni kwenye ukumbi utakaojulikana hapo badae na tarehe ya uchaguzi utakuwa tarehe 10/1/2013 saa nne asubuhi

No comments:

Post a Comment