Thursday, January 3, 2013

AZAM, COASTAL HAKUNA MBABE MAPINDUZI


Beki wa Coastal Union akiupitia mpira kwenye miguu ya mshambuliaji wa Azam, Seif Abdallah usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi. timu hizo zilitoka 0-0.

AZAM FC na Coastal Union ya Tanga zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Coastal leo ndio waliotawala mchezo na kupoteza nafasi kama tatu za wazi za kufunga mabao, kutokana na umakini mdogo kila walipopata nafasi hizo.
Azam walipata nafasi moja nzuri kipindi cha pili, lakini walinzi wa Coastal walisimama imara na kuondosha kwenye hatari jaribio hilo.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Salum Abubakar, Humphrey Mieno, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche/Brian Umony dk 24 na Hamisi Mcha ‘Vialli’/Seif Abdallah dk 66. 
Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis ‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Hussein Twaha dk 50, Jerry Santo, Mohamed Mtindi, Soud Othman/Razack Khalfan dk90 na Danny Lyanga/Joseph Mahundi dk 90. 
Katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Miembeni iliitandika mabao 4-1 Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa mao Dze Tung.
Mabao ya Miembeni yalitiwa kimiani Adeyum Saleh Ahmed dakika ya 41 na 72, Mohamed Hamdani na Rashid Roshwa dakiaka ya 74, wakati la Mtibwa la kufutia machozi lilifungwa na Juma Mpakala dakika ya 10. 


Kiungo wa Coastal Union ya Tanga, Jerry Santo akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Azam FC ya Dar es Salaam, Salum Abubakar katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku huu. Timu hizo zilitoka 0-0.

Hatari langoni mwa Coastal

Suleiman Kassim 'Selembe' akimuacha chini Khamis Mcha 'Vialli'

Kipre Balou akiuwahi mpira mrefi dhidi ya Jerry Santo wa Coastal

Himid Mao wa Azam na Mohamed Mtindi wa Coastal Union wakigombea mpira

Himid Mao na Salum Abubakar wakishirikiana kumpokonya mpira mchezaji wa Coastal

Suleiman Kassim 'Selembe' akimtoka kiungo wa Azam, Khamis Mcha 'Vialli'

Juma Mpongo amedaka mbele ya mshambuliaji wa Azam, Gaudence Mwaikimba 

Brian Umony wa Azam akiwa amemuangukia mchezaji wa Coastal

Hamisi Shengo wa Coastal Union, akitafuta mbinu za kumtoka Humphrey Mieno wa Coastal Union 

Hamisi Shengo wa Coastal Union, akitafuta mbinu za kumpokonya mpira Humphrey Mieno wa Azam 


Kikosi cha Azam leo

Manahodha Jerry Santo wa Coastal Union na Himid Mao wa Azam FC kulia

Kikosi cha Coastal Union leo

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Bihindi Hamad Khamis akisalimiana na kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar kabla ya mechi ya Kundi B ya Kombe la Mapinduzi kati yao na Coastal Union kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Rais wa ZFA, Aman Ibrahim Makungu akisalimiana na beki wa Azam FC, Joackins Atudo kabla ya mechi ya Kundi B ya Kombe la Mapinduzi kati yao na Coastal Union kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar

No comments:

Post a Comment