Wednesday, January 2, 2013

LEO CHELSEA, EVERTON, LIVERPOOL, QPR, SUNDERLAND & NEWCASTLE UWANJANI!!

BENITEZ-CHELSEALEO Timu 6 za BPL, Barclays Premier League, zitashuka dimbani kucheza Mechi zao za kwanza za Mwaka mpya 2013 na zifuatazo ni DONDOO MUHIMU za MECHI HIZO ZIKIWEMO HALI ZA WACHEZAJI na REKODI ZAO za USO KWA USO:
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton
CHELSEA v QPR
Hali za Wachezaji
Kipa wa Chelsea Petr Cech ataikosa Mechi hii baada ya kuumia nyonga juzi walipocheza na Everton na nafasi yake itashikwa na Turnbull
Nae Nahodha wa Chelsea John Terry bado yupo nje akiwa ni majeruhi.
Bosi wa QPR Harry Redknapp amesema atawakosa Wachezaji watatu au wanne walioumia walipocheza juzi na Liverpool lakini amekataa kutaja Majina yao.
Uso kwa Uso
-Katika Mechi 11 za Ligi Kuu England walizokutana, QPR wameshi 2 na Chelsea 5.    -QPR hawajashinda Stamford Bridge tangu walipopata ushindi wa 2-0 Aprili 1983.
LIVERPOOL v SUNDERLAND
Hali za Wachezaji
Liverpool watamkosa Beki wao wa kushoto Jose Enrique ambae ameumia musuli za pajani na huenda Winga wao Stewart Downing akalazimika kucheza nafasi hiyo.
Beki wa Sunderland John O'Shea hatacheza baada ya kuumia walipocheza na Spurs Jumamosi iliyopita lakini Fulbeki Danny Rose atarudi kilingeni baada ya kuzuiwa kucheza dhidi ya Spurs kwa vile ndio Klabu yake na yeye yupo Sunderland kwa Mkopo.
Uso kwa Uso
-Sunderland hawajahi kuifunga Liverpool Uwanjani Anfield tangu Ligi Kuu England ianzishwe na wameshacheza Mechi 11 za Ligi hiyo.
- Sunderland wameifunga Liverpool mara 3 tu katika Mechi za Ligi Kuu England katika Mechi 23 walizocheza kati yao.
NEWCASTLE v EVERTON
Hali za Wachezaji
Newcastle hawatakuwa nae Danny Simpson alievunjika kidole cha mguu walipocheza na Arsenal hivi majuzi na ingawa Kiungo Yohan Cabaye na Beki Steven Taylor wameshaanza mazoezi baada ya kuwa majeruhi kwa kipindi sasa lakini Mechi hii ni mapema kwao kuingia dimbani.
Everton wanamkaribisha Nyota wao na Mfungaji wao Bora Marouane Fellaini ambae amemaliza Kifungo chake cha Mechi 3 lakini watamkosa Kiungo Darron Gibson ambae atakuwa nje kwa Mwezi mmoja baada ya kuumia paja.
Uso kwa Uso
-Katika Mechi 163 kati yao, kila moja imeshinda Mechi 64 na sare 35.
-Everton wameshinda Mechi 1 tu kati ya 10 walizocheza mwisho Uwanja wa St James Park nyumbani kwa Newcastle.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO_Timu za Juu:
1 Man Utd Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 26] Pointi 52
2 Man City Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 22] Pointi 45
3 Tottenham Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 12] Pointi 39
4 Chelsea Mechi 19 [Tofauti ya Magoli 21] Pointi 38
5 Arsenal Mechi 20 [Tofauti ya Magoli 18] Pointi 34
6 Everton Mechi 20 [Tofauti ya Magoli 8] Pointi 33
7 West Brom Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 2] Pointi 33
8 Swansea Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 5] Pointi 29
9 Stoke Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 1] Pointi 29
10 Liverpool Mechi 20 [Tofauti ya Magoli 5] Pointi 28
11 West Ham Mechi 20 [Tofauti ya Magoli 0] Pointi 26
12 Norwich Mechi 21 [Tofauti ya Magoli -10] Pointi 25
13 Fulham Mechi 21 [Tofauti ya Magoli -5] Pointi 24
14 Sunderland Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -5] Pointi 22
15 Newcastle Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -11] Pointi 20
16 Aston Villa Mechi 21 [Tofauti ya Magoli -24] Pointi 19
17 Southampton Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -11]  Pointi 18
18 Wigan Mechi 21 [Tofauti ya Magoli -17] Pointi 18
19 Reading Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -17] Pointi 13
20 QPR Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -20] Pointi 10
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:  
**WIKIENDI YA JANUARI 5 MECHI ZA RAUNDI YA 3 FA CUP
Jumamosi 12 Januari 2013
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa V Southampton
Everton V Swansea
Fulham V Wigan
Norwich V Newcastle
Reading V West Brom
Stoke V Chelsea
Sunderland V West Ham
Jumapili 13 Januari 2013
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man United V Liverpool
[SAA 1 Usiku]
Arsenal V Man City
Jumatatu 14 Januari 2013
[SAA 5 Usiku]
QPR V Tottenham
Jumamosi 19 Januari 2013
[SAA 12 Jioni]
Liverpool V Norwich
Man City V Fulham
Newcastle V Reading
Swansea V Stoke
West Ham V QPR
Wigan V Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom V Aston Villa
Jumapili 20 Januari 2013
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea V Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham V Man Utd
Jumatatu 21 Januari 2013
[SAA 5 Usiku]
Southampton V Everton
Jumatano 23 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal V West Ham
**WIKIENDI YA JANUARI 26 MECHI ZA RAUNDI YA 4 FA CUP
Jumanne 29 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Aston Villa V Newcastle
Norwich V Tottenham
QPR V Man City
Stoke V Wigan
Sunderland V Swansea
[SAA 5 Usiku]
Reading V Chelsea
Jumatano 30 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal V Liverpool
Everton V West Brom
Fulham V West Ham
[SAA 5 Usiku]
Man United V Southampton

No comments:

Post a Comment