Monday, January 14, 2013

ULAYA: BARCA YAZIDI KUPAA YAMALIZA MZUNGUKO WA KWANZA BILA KUFUNGWA , JUVE YANASA, YAKARIBIWA NA LAZIO & NAPOLI ,BPL MAN U NA MAN CITY BALAAA WASHINDA DARBY KUBWA JANA!

BARCA_v_REALSERIE A
MATOKEO:
Jumapili Januari 13
Torino FC 3 Siena 2
SS Lazio 2 Atalanta 0
Parma 1 Juventus 1
Udinese 3 Fiorentina 1
Napoli 3 Palermo 0
Cagliari 2 Genoa 1
Catania 1 AS Roma 0
Sampdoria 0 AC Milan 0

Wakati Mabingwa watetezi na Vinara wa Serie A, Juventus, wakitoka sare, Lazio na Napoli zilishinda Mechi zao na kuisogelea Juventus.

MSIMAMO-Timu za JUU:
[Kila Timu imecheza Mechi 20]
1 Juventus Pointi 45
2 Lazio 42
3 Napoli 40
4 Inter Milan 38
5 Fiorentina 35
6 AS Roma 32
7 AC Milan 31

Juventus, wakicheza ugenini, walifunga Bao kwanza kwa frikiki ya Andrea Pirlo lakini Nicola Sansone akaisawazishia Parma na Mechi kumalizika 1-1.
Lazio waliifunga Atalanta Bao 2-0 na kujichimbia nafasi ya pili wakiwa Pointi 3 nyuma ya Juventus.
Bao za Lazio zilifungwa na Sergio Floccari na Davide Brivio, aliejifunga mwenyewe, na vile vile Atalanta kumaliza Mechi hiyo wakiwa Mtu 10 baada ya Beki Carlos Carmona kupewa Kadi za Njano mbili na kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Napoli waliichapa Palermo 3-0 kwa Bao za Christian Maggio, Gokhan Inler na Lorenzo Insigne.
LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Januari 13
Real Betis 2 Levante 0
Real Sociedad 1 Deportivo La Coruna 1
Atletico de Madrid 2 Real Zaragoza 0
Malaga CF 1 FC Barcelona 3
Jumatatu Januari 14
Getafe CF v Granada CF

Lionel Messi aliifungia Barcelona Bao la Kwanza katika Dakika ya 27 na kumtengenezea Cesc Fabregas, aliefunga Bao la Pili na Thiago kufunga la tatu, na kuwapa Barcelona ushindi wa Bao 3-1 dhidi ya Malaga ambao walifunga Bao lao pekee Dakika ya mwisho ya mchezo kupitia Diego Buonanotte.
Ushindi huo umewafanya Barca wawe Pointi 11 mbele ya Timu ya Pili Atletico Madrid ambao nao waliifunga Real Zaragoza 2-0 na kujivuta kuwa Pointi 7 mbele ya Timu ya 3 Real Madrid ambao Jumamosi walitoka 0-0 na Osasuna.
Bao za Atletico Madrid zilifungwa na Tiago na Radamel Falcao kwa Penati.
 
ARSENAL 0 MAN CITY 2
MANCINI_n_WENGERKwa mara ya kwanza katika Miaka 37, Manchester City wamefanikiwa kuifunga Arsenal nyumbani kwao na kuwakaribia Vinara wa Ligi Manchester United na kuwa Pointi 7 nyuma yao baada ya kushinda 2-0 katika Mechi ambayo Arsenal walibakia Mtu 10 kuanzia Dakika ya 10.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 22 isipokuwa inapotajwa]
1 Man United Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 27] Pointi 55
2 Man City  [Tofauti ya Magoli 24] Pointi  48
3 Chelsea  Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 24] Pointi 41
4 Tottenham [Tofauti ya Magoli 22] Pointi 40
5 Everton [Tofauti ya Magoli 22] Pointi 37
6 Arsenal Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 16] Pointi 34
7 West Brom [Tofauti ya Magoli 1] Pointi 33
8 Liverpool [Tofauti ya Magoli 7] Pointi 31
9 Swansea [Tofauti ya Magoli 5] Pointi 30
10 Stoke [Tofauti ya Magoli -3] Pointi 29

Sentahafu wa Arsenal Laurent Koscielny alitolewa nje katika Dakika ya 10 kwa kumshika Edin Dzeko ambae alipiga Penati ya kosa hilo lakini Kipa Szczesny aliokoa baada ya mpira kupiga posti.
Kosa kosa hiyo ilizidisha munkari wa Man City ambao walizidisha presha na James Milner kuwafungia Bao la kwanza Dakika ya 21 na Dzeko kuongeza la pili Dakika ya 32.
Kipindi cha Pili Nahodha wa Man City Vincent Kompany alipewa Kadi Nyekundu na Refa Mike Dean kwa kumrukia miguu miwili Jack Wilshere.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Koscielny, Vermaelen, Gibbs, Diaby, Wilshere, Cazorla, Oxlade-Chamberlain, Podolski, Walcott
Akiba: Mannone, Mertesacker, Andre Santos, Giroud, Ramsey, Coquelin, Jenkinson.
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Javi Garcia, Barry, Milner, Silva, Tevez, Dzeko
Akiba: Pantilimon, Lescott, Sinclair, Kolarov, Suarez, Rekik, Balotelli.
Refa: Mike Dean

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumatano Januari 16
[SAA 4 DAK 45 Usiku]
Chelsea v Southampton
Jumamosi Januari 19
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Norwich
Man City v Fulham
Newcastle v Reading
Swansea v Stoke
West Ham v QPR
Wigan v Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom v Aston Villa
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United
  MANCHESTER UNITED 2 LIVERPOOL 1
>>UNITED WAKO POINTI 10 MBELE, KILELENI!
BPL_LOGOManchester United leo wamezidi kupaa kileleni baada ya kuwachapa Mahasimu wao wakubwa Liverpool Bao 2-1 Uwanjani Old Trafford na kukwea juu kileleni mwa BPL, Barclays Premier League, wakiwa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Man City ambao muda mfupi baadae leo wana kibarua kigumu Uwanjani Emirates watakapoivaa Arsenal.RVP-BAO_NA_LIVERPOOL

MAGOLI:
Man United 2
-Van Persie Dakika ya 19
-Vidic 54
Liverpool 1
-Sturridge Dakika ya 57

Man United, ambao walitawala kabisa Kipindi cha Kwanza, walifunga Bao lao la kwanza kupitia Robin van Persie kufuatia pasi murua kati ya Danny Welbeck, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Patrice Evra kumtilia pasi ya chini Van Persie aliepachika wavuni kiakili.
Frikiki ya Robin van Persie iliunganishwa kwa kichwa na Patrice Evra na kumparaza Nemanja Vidic na kutinga wavuni na kuwapa Man United Bao la Pili.
Lakini, Dakika chache baadae, makosa ya Man United yaliwapa Liverpool Bao laini baada ya shuti la Steven Gerrard kutemwa na Kipa David De Gea na kutua njiani kwa Mchezaji mpya Daniel Sturridge alieunganisha vizuri na kufunga Bao lake la kwanza kwenye BPL kwa Timu yake mpya na Bao lake la pili baada ya pia kuifungia kwenye FA CUP walipoichapa Mansfield 2-1 kwenye Mechi yake ya kwanza kabisa hivi majuzi.
VIKOSI:
Manchester United: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Cleverley, Young, Kagawa, Welbeck, van Persie
Akiba: Amos, Jones, Valencia, Anderson, Giggs, Smalling, Hernandez.
Liverpool: Reina, Wisdom, Skrtel, Agger, Johnson, Lucas, Downing, Gerrard, Allen, Sterling, Suarez
Akiba: Jones, Henderson, Sturridge, Carragher, Borini, Shelvey, Robinson.
Refa: Howard Webb

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumapili 13 Januari 2013
[SAA 1 Usiku]
Arsenal v Man City
Jumatano Januari 16
[SAA 4 DAK 45 Usiku]
Chelsea v Southampton
Jumamosi Januari 19
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Norwich
Man City v Fulham
Newcastle v Reading
Swansea v Stoke
West Ham v QPR
Wigan v Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom v Aston Villa
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United

No comments:

Post a Comment