Monday, January 21, 2013

PINGAMIZI DHIDI YA WAGOMBEA TFF ZAITWA HARAKA ILI KUTOA DOSARI KUELEKEA KATIKA UCHAGUZI FEB 24


 
BAADA ya kupitia fomu za waombaji uongozi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho hilo leo inaanza mchakato wa pingamizi dhidi ya wagombea.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba, leo saa 10:00 jioni Kamati ya Uchaguzi itabandika kwenye ubao wa matangazo wa TFF majina ya waombaji ili kutoa fursa kwa kipindi cha pingamizi.
Wambura amesema mwisho wa kupokea pingamizi dhidi ya waombaji uongozi ni Januari 26, mwajka huu saa 10:00 jioni.
Jumla ya watu 50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa TFF utakaofanyika Februari 24, mwaka huu wamerejesha fomu hizo.
Waombaji ambao hawakurejesha fomu ni Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha kamili ya wagombea waliorejesha fomu ni Athumani Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura wanaogombea Urais, nafasi inayoachwa wazi na Leodegar Tenga anayeng’atuka, Michael Wambura, Ramadhani Nassib na Wallace Karia wanaogombea Makamu wa Rais, nafasi inayoachwa wazi na Nyamlani, anayehamia kwenye Urais.
Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
Aidha, waombaji wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha fomu.
Kwa upande wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph Manji wa Yanga wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.
Nafasi mbili za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza zimeombwa na watu watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa Moro United, Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu Mwindadi.

No comments:

Post a Comment